Kuukimbilia msamaha wa Allah na Pepo yake aliyo waahidi Waumini, ni neema kubwa ya Allah ambayo humpa amtakaye.
Kushindana katika Kufanya matendo mema
Pepo si ya mwenye kuzuia hasira zake tu, bali ni ya mwenye kutoa katika wasaa na dhiki, na akawasamehe watu.
Njia za kupata radhi za Allah zipo katika matendo ya wema.
“Kimbilieni msamha wa Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, iliyo wekewa walio muamini Allah na Mitume wake. Hiyo ndiyo fadhila ya Allah, humpa amtakaye. Na Allah ni Mwenye fadhila kuu”. Surat Al-Hadid: 21.
Kuukimbilia msamaha wa Allah na Pepo yake aliyo waahidi Waumini, ni neema kubwa ya Allah ambayo humpa amtakaye.
Basi, ewe Muumini! Weka lengo lako kuu kuwa ni kufaulu kwa kufanya juhudi zitakazo kuwezesha kupata radhi za Allah na kupata msamaha wake.
Tunajifunza kuwa: Kukimbilia kheri ni njia ya kupata msamaha wa Allah.
Pepo ni kubwa kama mbingu na ardhi, wameandaliwa waumini, imejaa neema na rehma za Allah, ni zawadi kubwa kutoka kwa Allah kwa amtakae.
Pepo ni neema ya Allah.
“Na kimbilieni msamaha wa Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamungu. Ambao hutoa wanapo kuwa na wasaa na wanapo kuwa na dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu, na Allah huwapenda wafanyao wema”. Surat Aali-Imran: 133 – 134.
Pepo si ya mwenye kuzuia hasira zake tu, bali ni ya mwenye kutoa katika wasaa na dhiki, na akawasamehe watu.
Njia za kupata radhi za Allah zipo katika matendo ya wema.
Tunajifunza kuwa:
Huruma ni katika matendo ya wema.
Kukimbilia msamaha wa Allah na Pepo yake tukufu kwa kutoa, kusubiri, kuzuia hasira, ni miongoni mwa sifa za Wachamungu. Na mwenye kusamehe watu hupata mapenzi ya Allah.
Tunajifunza kuwa:
Kushikamana na tabia hizi njema ni njia ya kupata msamaha wa Allah na Pepo yake.
“Na Dhun-Nun alipoondoka hali ameghadhibika, na akadhani ya kwamba hatutakuwa na uwezo juu yake. Basi aliita katika giza: Hapana Mungu isipo kuwa Wewe, Umetakasika, hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu. Basi tukamwitikia na tukamwokoa kutokana na dhiki. Na hivyo ndivyo tunavyo waokoa Waumini”. Surat Al-Anbiyaa: 87 – 88.
Unapo pata dhiki ya maisha, na moyo kugubikwa na mazito, kumbuka dua aliyo iomba Dhun-Nun(Nabii Yunus) aliposema: Hapana Mungu isipo kuwa Wewe, Umetakasika, hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu.
Allah anamjibu kila mwenye kutakasa toba.
Tunajifunza kuwa:
Toba ni sababu ya kujibiwa dua.
Katika nyakati nzito kimaisha na dhiki, kumtegema Allah ndiyo suluhisho.
Kama alivyo mwokoa Dhun-Nun katika viza vya samaki, ndivyo anavyo mwokoa kila mwenye imani na kuomba msaada wake.
“Yeye ndiye anaye kuendesheni bara na baharini. Hata mnapo kuwa majahazini na yakawa yanakwenda nao kwa uPepo mzuri wakaufurahia, uPepo mkali ukawazukia, na yakawajia mawimbi kutoka kila upande, na wakaona wameshazongwa, basi hapo humwomba Allah kwa kumsafishia niya: Ukituokoa na haya bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanao kushukuru. Lakini akisha waokoa, mara wanafanya jeuri tena katika nchi bila ya haki. Enyi watu! Jeuri zenu zitakudhuruni wenyewe. Hii ni starehe ya maisha ya dunia tu. Kisha marejeo yenu ni kwetu, na hapo tutakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda”. Surat Yunus: 22 – 23.
Tunapopatwa na changamoto, na kumtegemea Allah kwa kumuomba Yeye kwa utakaso (Ikhlaswi), basi faraja yake huja haraka bila ya kutegemea.
Lakini jambo jema ni kutekeleza shukurani kwa kumuabudu Allah baada ya wokovu na kutozama katika uovu na ujeuri.
Tunajifunza kuwa:
Kutimiza wajibu ni kumshukuru Allah.
Wakati mawimbi yanapo zidi, na hali ya hewa ikawa mbaya baharini, huwa tunauona udhaifu wetu mbele ya uwezo wa Allah, na huwa tunamuelekea Yeye kwa kumuomba kwa ikhlaswi. Lakini balaa kubwa ni pale tunapo okolewa na kuwa salama, kuacha kuonesha shukurani zetu kwa Allah, jambo hili ni baya sana na lisilo faa kufanywa na Waumini wa kweli.
“Watu wamepambiwa kupenda matamanio ya wanawake, na watoto, na mirundikano ya dhahabu na fedha, na farasi asili, na mifugo, na mashamba. Hayo ni starehe ya maisha ya duniani, na kwa Allah ndio kwenye marejeo mema”. Surat Aali- Imran: 14.
Mapambo ya dunia hii yamezungukwa na mapenzi ya mali, watoto na kuwa na nguvu. Lakini vyote hivyo ni starehe yenye kuisha.
Kuhangaikia vilivyo kwa Allah ndiyo lengo kuu, na marejeo bora ya akhera na mafanikio makubwa.
Tunajifunza kuwa:
Akhera ni bora kuliko dunia isiyo dumu.
Matamanio huvutia nyoyo kupenda mali, watoto na vipambo vya dunia(wanawake nk) lakini vyote hivyo ni starehe ya muda tu.
Ama marejeo mema yapo kwa Allah kwa kila mwenye kutakasa niya na kufanya juhudi.
“Jueni ya kwamba maisha ya dunia ni mchezo, na pumbao, na pambo, na kujifakharisha baina yenu na kushindana kwa wingi wa mali na watoto. Mfano wake ni kama mvua ambayo huwafurahisha wakulima mimea yake, kisha hunyauka ukayaona yamepiga manjano kisha yakawa mabua. Na akhera kuna adhabu kali na msamaha kutoka kwa Allah na radhi. Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe ya udanganyifu”. Surat Al-Hadid: 20
Dunia si chochote ila ni mchezo, na upuuzi na mapambo wanayo jifakharisha nayo watu, na kukithirisha mali na watoto. Mfano wake ni kama mazao yanayo mea na kukauka na hatimaye mtu akajisahau na kujikuta hana kitu huko akhera.
Malipo ya huko, ima ni adhabu au msamaha na radhi kutoka kwa Allah.
Tunajifunza kuwa:
Dunia haidumu, na akhera ndio inayo dumu.
Maisha ya dunia yana onekana wazi kwa mambo ya kupumbaza na upuuzi. Lakini mwisho wake ni kama mwisho wa mazao ambayo huishia kuwa mabua!
Kumbuka!
Akhera ndio inayo dumu, ima kupata msamaha na radhi za Allah au kupata adhabu kali.
Tunajifunza kuwa:
Dunia ni starehe zenye kudanganya, na akhera ndio bora.
“Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu. Lakini hawapewi wema huu ila wanao subiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa”. Surat Fusswilat: 34 – 35.
Mema na maovu hayalingani.
Kuwa miongoni mwa wale ambao wanalipiza ubaya kwa wema. Huwenda adui yako akabadilika na kuwa rafiki yako kipenzi. Na haya hawayafikii ila walio na subira na wenye bahati kubwa.
Tunajifunza kuwa:
Wema na subira ni katika tabia njema za Uislamu.
Lipiza kwa njia iliyo bora zaidi, kwa hali yoyote ya dhuluma utakayo fanyiwa. Huwenda wema wako ukambadilisha adui yako na kuwa ni rafiki yako kipenzi.
Na tambua kuwa sifa hizi njema hawazipati isipo kuwa wale wenye subira katika maudhi na wenye bahati ya kuwafikiwa katika kheri.
“Na mnapo safiri katika nchi si vibaya kwenu kama mkifupisha sala, iwapo mnahofia wasije wale walio kufuru wakakuleteeni maudhi. Hakika makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi”. Surat An-Nisaa: 101.
Katika safari na jihadi, Allah ameruhusu kufupisha sala, kwa lengo la waumini kujilinda na maudhi ya makafiri. Na hii ni rehema ya Uislamu inayo dhihiri katika kuwepesisha ibada katika kipindi kigumu.
Tunajifunza kuwa:
Kuwepesishwa sala wakati wa dhiki ni huruma ya Uislamu.
Katika harakati zako za amani na safari, kumbuka kuwa Uislamu ni dini ya huruma na wepesi. Umeruhusu kufupisha sala ikiwa unahofia maudhi ya maadui. Na adui yenu yupo wazi wazi kwa vitimbi vyake, lakini rehema za Allah juu yenu ni pana sana.
Tunajifunza kuwa:
Kufupisha sala katika vipindi vya dhiki ni katika wepesi wa dini ya Uislam.
“Na wanaposikia upuuzi hujitenga nao na husema: Sisi tuna vitendo vyetu na nyinyi mna vitendo vyenu, Amani iwe juu yenu! Sisi hatutaki kujibizana na wajinga”. Surat Al-Qaswas: 55.
Unapokutana na upuuzi na maneno mabaya, basi kumbuka muongozo kuwa Muumini wa kweli huwa anajitenga na hayo na kuchagua salama. Bali inatakiwa kuwa mzuri wa majibu kwa kusema:
“Matendo yetu ni yetu, na yenu ni yenu, na sisi Waislamu hatutaki kujibizana na wajinga”.
Tunajifunza kuwa:
Katika tabia njema ni kujiepusha na batili.
Kujiepusha na upuuzi ni miongoni mwa tabia njema za waja wa Allah.
Hivyo, tunawajibika kuwajibu wajinga, wanapo tusemeza ubaya: “Sisi tuna vitendo vyetu na nyinyi mna vitendo vyenu, hatutaki mijadala na wajinga”.
Tunajifunza kuwa:
Amani ndio njia yetu, na adabu bora ya kujitenga na upuuzi ni amani.