Sura: ASH-SHARHI 

Aya : 1

أَلَمۡ نَشۡرَحۡ لَكَ صَدۡرَكَ

Je, hatukukunjulia kifua chako?



Sura: ASH-SHARHI 

Aya : 2

وَوَضَعۡنَا عَنكَ وِزۡرَكَ

Na tukakuondolea mzigo wako?



Sura: ASH-SHARHI 

Aya : 3

ٱلَّذِيٓ أَنقَضَ ظَهۡرَكَ

Ulio vunja mgongo wako?



Sura: ASH-SHARHI 

Aya : 4

وَرَفَعۡنَا لَكَ ذِكۡرَكَ

Na tukakunyanyulia utajo wako?



Sura: ASH-SHARHI 

Aya : 5

فَإِنَّ مَعَ ٱلۡعُسۡرِ يُسۡرًا

Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi,



Sura: ASH-SHARHI 

Aya : 6

إِنَّ مَعَ ٱلۡعُسۡرِ يُسۡرٗا

Hakika pamoja na uzito upo wepesi



Sura: ASH-SHARHI 

Aya : 7

فَإِذَا فَرَغۡتَ فَٱنصَبۡ

Na ukipata faragha, fanya juhudi



Sura: ASH-SHARHI 

Aya : 8

وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَٱرۡغَب

Na kwa (ajili ya) Mola wako Mlezi ushughulike