وَٱلضُّحَىٰ
Naapa kwa mchana!
Kushiriki :
وَٱلَّيۡلِ إِذَا سَجَىٰ
Na kwa usiku unapo tanda!
مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ
Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe
وَلَلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ لَّكَ مِنَ ٱلۡأُولَىٰ
Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia
وَلَسَوۡفَ يُعۡطِيكَ رَبُّكَ فَتَرۡضَىٰٓ
Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike
أَلَمۡ يَجِدۡكَ يَتِيمٗا فَـَٔاوَىٰ
Kwani hakukukuta yatima akakupa makazi?
وَوَجَدَكَ ضَآلّٗا فَهَدَىٰ
Na akakukuta umepotea akakuongoa?
وَوَجَدَكَ عَآئِلٗا فَأَغۡنَىٰ
Akakukuta mhitaji akakutosheleza?
فَأَمَّا ٱلۡيَتِيمَ فَلَا تَقۡهَرۡ
Basi yatima usimwonee!
وَأَمَّا ٱلسَّآئِلَ فَلَا تَنۡهَرۡ
Na anaye omba au kuuliza usimkaripie!
وَأَمَّا بِنِعۡمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثۡ
Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie