سَبِّحِ ٱسۡمَ رَبِّكَ ٱلۡأَعۡلَى
Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa,
Kushiriki :
ٱلَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ
Aliye umba, na akaweka sawa,
وَٱلَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ
Na ambaye amekadiria na akaongoa,
وَٱلَّذِيٓ أَخۡرَجَ ٱلۡمَرۡعَىٰ
Na aliye otesha malisho,
فَجَعَلَهُۥ غُثَآءً أَحۡوَىٰ
Kisha akayafanya makavu, meusi
سَنُقۡرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰٓ
Tutakusomesha wala hutasahau,
إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۚ إِنَّهُۥ يَعۡلَمُ ٱلۡجَهۡرَ وَمَا يَخۡفَىٰ
Ila akipenda Allah. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana
وَنُيَسِّرُكَ لِلۡيُسۡرَىٰ
Na tutakusahilishia yawe mepesi
فَذَكِّرۡ إِن نَّفَعَتِ ٱلذِّكۡرَىٰ
Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa
سَيَذَّكَّرُ مَن يَخۡشَىٰ
Atakumbuka mwenye kuogopa
وَيَتَجَنَّبُهَا ٱلۡأَشۡقَى
Na atajitenga mbali nayo mpotovu,
ٱلَّذِي يَصۡلَى ٱلنَّارَ ٱلۡكُبۡرَىٰ
Ambaye atauingia Moto mkubwa
ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحۡيَىٰ
Tena humo hatakufa wala hawi hai
قَدۡ أَفۡلَحَ مَن تَزَكَّىٰ
Hakika amekwisha fanikiwa aliyejitakasa
وَذَكَرَ ٱسۡمَ رَبِّهِۦ فَصَلَّىٰ
Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali
بَلۡ تُؤۡثِرُونَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا
Lakini nyinyi mnakhiari (mnapenda sana) maisha ya dunia!
وَٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ وَأَبۡقَىٰٓ
Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi
إِنَّ هَٰذَا لَفِي ٱلصُّحُفِ ٱلۡأُولَىٰ
Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo,
صُحُفِ إِبۡرَٰهِيمَ وَمُوسَىٰ
Vitabu vya Ibrahimu na Mussa