إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوۡمِهِۦٓ أَنۡ أَنذِرۡ قَوۡمَكَ مِن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ
Hakika, Sisi Tulimtuma Nuhu kwa watu wake (tukamwambia) kwamba: Waonye watu wako kabla haijawafikia adhabu iumizayo sana
قَالَ يَٰقَوۡمِ إِنِّي لَكُمۡ نَذِيرٞ مُّبِينٌ
(Nuhu) Akasema: Enyi watu wangu, hakika mimi kwenu ni muonyaji wa dhahiri (wa wazi) kwenu
أَنِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ وَٱتَّقُوهُ وَأَطِيعُونِ
(Nakuonyeni) Kwamba muabuduni Allah na mcheni (muogopeni) na mnitii
يَغۡفِرۡ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمۡ وَيُؤَخِّرۡكُمۡ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمًّىۚ إِنَّ أَجَلَ ٱللَّهِ إِذَا جَآءَ لَا يُؤَخَّرُۚ لَوۡ كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ
Atakusameheni madhambi yenu, na atakuahirisheni mpaka muda uliowekwa. Hakika muda wa Allah ukifika haucheleweshwi, lau kama mngekuwa mnajua
قَالَ رَبِّ إِنِّي دَعَوۡتُ قَوۡمِي لَيۡلٗا وَنَهَارٗا
(Nuhu) Akasema: Mola wangu! Hakika mimi nimewalingania watu wangu usiku na mchana
فَلَمۡ يَزِدۡهُمۡ دُعَآءِيٓ إِلَّا فِرَارٗا
Lakini haikuwazidishia wito wangu isipokuwa kukimbia
وَإِنِّي كُلَّمَا دَعَوۡتُهُمۡ لِتَغۡفِرَ لَهُمۡ جَعَلُوٓاْ أَصَٰبِعَهُمۡ فِيٓ ءَاذَانِهِمۡ وَٱسۡتَغۡشَوۡاْ ثِيَابَهُمۡ وَأَصَرُّواْ وَٱسۡتَكۡبَرُواْ ٱسۡتِكۡبَارٗا
Na hakika Mimi kila nilipowaita ili Uwasamehe; huweka vidole vyao masikioni mwao na wakajifunika nguo zao na wakashikilia (kukanusha) wakafanya kiburi kikubwa
ثُمَّ إِنِّي دَعَوۡتُهُمۡ جِهَارٗا
Kisha hakika mimi niliwalingania kwa waziwazi
ثُمَّ إِنِّيٓ أَعۡلَنتُ لَهُمۡ وَأَسۡرَرۡتُ لَهُمۡ إِسۡرَارٗا
Kisha nikawatangazia kwa sauti, halafu tena nikasema nao kwa siri
فَقُلۡتُ ٱسۡتَغۡفِرُواْ رَبَّكُمۡ إِنَّهُۥ كَانَ غَفَّارٗا
Nikasema: Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe
يُرۡسِلِ ٱلسَّمَآءَ عَلَيۡكُم مِّدۡرَارٗا
Atakuleteeni mvua inyeshe mfululizo (Yenye kuendelea)
وَيُمۡدِدۡكُم بِأَمۡوَٰلٖ وَبَنِينَ وَيَجۡعَل لَّكُمۡ جَنَّـٰتٖ وَيَجۡعَل لَّكُمۡ أَنۡهَٰرٗا
Na Atakuongezeeni mali na wana, na Atakupeni mabustani na Atakufanyieni mito
مَّا لَكُمۡ لَا تَرۡجُونَ لِلَّهِ وَقَارٗا
Mna nini hamweki heshima ya Allah?
وَقَدۡ خَلَقَكُمۡ أَطۡوَارًا
Na hali Amekuumbeni hatua baada ya hatua?
أَلَمۡ تَرَوۡاْ كَيۡفَ خَلَقَ ٱللَّهُ سَبۡعَ سَمَٰوَٰتٖ طِبَاقٗا
Kwani hamwoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyo ziumba mbingu saba kwa matabaka?
وَجَعَلَ ٱلۡقَمَرَ فِيهِنَّ نُورٗا وَجَعَلَ ٱلشَّمۡسَ سِرَاجٗا
Na Akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru, na Akalifanya jua ni taa yenye mwanga mkali?
وَٱللَّهُ أَنۢبَتَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ نَبَاتٗا
Na Allah amekuotesheni (Amekuanzisheni vizuri katika udongo) wa ardhi kama mimea
ثُمَّ يُعِيدُكُمۡ فِيهَا وَيُخۡرِجُكُمۡ إِخۡرَاجٗا
Kisha Atakurudisheni humo na Atakutoeni tena mtoke (kuwa hai)
وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَرۡضَ بِسَاطٗا
Na Allah Amekufanyieni ardhi kuwa (kama) busati
لِّتَسۡلُكُواْ مِنۡهَا سُبُلٗا فِجَاجٗا
Ili mtembee humo katika njia zilizo pana
قَالَ نُوحٞ رَّبِّ إِنَّهُمۡ عَصَوۡنِي وَٱتَّبَعُواْ مَن لَّمۡ يَزِدۡهُ مَالُهُۥ وَوَلَدُهُۥٓ إِلَّا خَسَارٗا
Nuhu akasema: Mola wangu! Hakika hao wameniasi, na wamemfuata yule ambaye mali yake na wanawe hawakumzidishia ila khasara tu
وَمَكَرُواْ مَكۡرٗا كُبَّارٗا
Na wakapanga vitimbi vikubwa
وَقَالُواْ لَا تَذَرُنَّ ءَالِهَتَكُمۡ وَلَا تَذَرُنَّ وَدّٗا وَلَا سُوَاعٗا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسۡرٗا
Na wakasema: Msiwaache miungu yenu, wala msimwache Wadda wala Suwaa’ wala Yaghutha, wala Yau’qa, wala Nasra.[1]
1- - Wadda, Su’waa’a, Yaghuwtha, Ya’uwqa, Nasraa: ni majina ya masanamu waliyokuwa wakiyaabudu watu wa Nabii Nuhu, haya masanamu yalikuwa makubwa na matukufu zaidi kwao, na kwaajili hiyo yalihusishwa kwa kutajwa hapa, na asili yake ni kama vile alivyosema U’rwah bin Zubeyri-
وَقَدۡ أَضَلُّواْ كَثِيرٗاۖ وَلَا تَزِدِ ٱلظَّـٰلِمِينَ إِلَّا ضَلَٰلٗا
Na hao walikwisha wapoteza wengi, wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea
مِّمَّا خَطِيٓـَٰٔتِهِمۡ أُغۡرِقُواْ فَأُدۡخِلُواْ نَارٗا فَلَمۡ يَجِدُواْ لَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ أَنصَارٗا
Basi kwa ajili ya makosa yao waligharikishwa wakaingizwa Motoni, wala hawakuwapata wa kuwanusuru badala ya Allah
وَقَالَ نُوحٞ رَّبِّ لَا تَذَرۡ عَلَى ٱلۡأَرۡضِ مِنَ ٱلۡكَٰفِرِينَ دَيَّارًا
Na Nuh’u akasema: Mola wangu Mlezi! Usimwache juu ya ardhi mkaazi wake yeyote katika makafiri!
إِنَّكَ إِن تَذَرۡهُمۡ يُضِلُّواْ عِبَادَكَ وَلَا يَلِدُوٓاْ إِلَّا فَاجِرٗا كَفَّارٗا
Hakika Wewe Ukiwaacha, watawapoteza waja Wako, na wala hawatozaa isipokuwa mtendaji dhambi, kafiri mkanushaji mno
رَّبِّ ٱغۡفِرۡ لِي وَلِوَٰلِدَيَّ وَلِمَن دَخَلَ بَيۡتِيَ مُؤۡمِنٗا وَلِلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِۖ وَلَا تَزِدِ ٱلظَّـٰلِمِينَ إِلَّا تَبَارَۢا
Eee Mola wangu! Nisamehe Mimi na wazazi wangu, na kila aliye ingia nyumbani mwangu kuwa ni mwenye kuamini, na Waumini wote wanaume, na Waumini wote wanawake. Na wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea, (na kuteketea kabisa)