Sura: AL-QALAM 

Aya : 1

نٓۚ وَٱلۡقَلَمِ وَمَا يَسۡطُرُونَ

Nuun. Nina apa kwa kalamu na yale wayoyaandika



Sura: AL-QALAM 

Aya : 2

مَآ أَنتَ بِنِعۡمَةِ رَبِّكَ بِمَجۡنُونٖ

(Kwamba) Wewe (Muhammad) kwa neema ya Mola wako Mlezi (aliyokupa) sio mwendawazimu



Sura: AL-QALAM 

Aya : 3

وَإِنَّ لَكَ لَأَجۡرًا غَيۡرَ مَمۡنُونٖ

Na kwa hakika wewe una malipo (makubwa) yasiyo katika



Sura: AL-QALAM 

Aya : 4

وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٖ

Na hakika wewe uko juu ya tabia njema sana



Sura: AL-QALAM 

Aya : 5

فَسَتُبۡصِرُ وَيُبۡصِرُونَ

Basi hivi karibuni utaona, na wao wataona



Sura: AL-QALAM 

Aya : 6

بِأَييِّكُمُ ٱلۡمَفۡتُونُ

(Kwamba) Ni nani mwenye kichaa miongoni mwenu



Sura: AL-QALAM 

Aya : 7

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ

Hakika, Mola wako Mlezi ndiye amjuae zaidi aliyepotea njia yake, ndiye awajuae zaidi walioongoka



Sura: AL-QALAM 

Aya : 8

فَلَا تُطِعِ ٱلۡمُكَذِّبِينَ

Basi usiwatii wanao kadhibisha



Sura: AL-QALAM 

Aya : 9

وَدُّواْ لَوۡ تُدۡهِنُ فَيُدۡهِنُونَ

Wangependa uwe laini (ulegeze msimamo wako), nao wawe laini (walegeze msimamo wao na wakufuate)



Sura: AL-QALAM 

Aya : 10

وَلَا تُطِعۡ كُلَّ حَلَّافٖ مَّهِينٍ

Wala usimtii kila mwapaji sana, aliye dhalili,



Sura: AL-QALAM 

Aya : 11

هَمَّازٖ مَّشَّآءِۭ بِنَمِيمٖ

Mwingi wa kusengenya, mpitaji huku na kule kwa kufitinisha



Sura: AL-QALAM 

Aya : 12

مَّنَّاعٖ لِّلۡخَيۡرِ مُعۡتَدٍ أَثِيمٍ

Mwingi wa kuzuia ya kheri, aliyependukia katika kuwadhulumu (Watu) mwingi wa kutenda dhambi



Sura: AL-QALAM 

Aya : 13

عُتُلِّۭ بَعۡدَ ذَٰلِكَ زَنِيمٍ

Mkavu, na juu ya hayo ni mwana haramu (kujipachika tu kabila)



Sura: AL-QALAM 

Aya : 14

أَن كَانَ ذَا مَالٖ وَبَنِينَ

Kwakuwa tu ni mwenye kumiliki mali na watoto?



Sura: AL-QALAM 

Aya : 15

إِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِ ءَايَٰتُنَا قَالَ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ

Anapo somewa Aya zetu, husema: Hizi ni simulizi za uwongo za watu wa zamani!



Sura: AL-QALAM 

Aya : 16

سَنَسِمُهُۥ عَلَى ٱلۡخُرۡطُومِ

Karibuni tutamtia kovu juu ya pua



Sura: AL-QALAM 

Aya : 17

إِنَّا بَلَوۡنَٰهُمۡ كَمَا بَلَوۡنَآ أَصۡحَٰبَ ٱلۡجَنَّةِ إِذۡ أَقۡسَمُواْ لَيَصۡرِمُنَّهَا مُصۡبِحِينَ

Hakika sisi Tumewajaribu (Maquraysh) kama Tulivyowajaribu watu wa shamba pale walipo apa kuwa bila shaka watayavuna (matunda yake) watakapo pambaukiwa asubuhi



Sura: AL-QALAM 

Aya : 18

وَلَا يَسۡتَثۡنُونَ

Na wala hawakusema In-Shaa Allaah (Allah akipenda)!



Sura: AL-QALAM 

Aya : 19

فَطَافَ عَلَيۡهَا طَآئِفٞ مِّن رَّبِّكَ وَهُمۡ نَآئِمُونَ

Basi (shamba lao) likazungukwa na (moto) kutoka kwa mola wako ilihali wao wamelala



Sura: AL-QALAM 

Aya : 20

فَأَصۡبَحَتۡ كَٱلصَّرِيمِ

Likawa kama lilovunwa (ilion-g’olewa mimea yake)



Sura: AL-QALAM 

Aya : 21

فَتَنَادَوۡاْ مُصۡبِحِينَ

Wakaitana, pale walipopam-baukiwa asubuhi



Sura: AL-QALAM 

Aya : 22

أَنِ ٱغۡدُواْ عَلَىٰ حَرۡثِكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰرِمِينَ

Kwamba nendeni asubuhi mapema shambani mwenu, mkiwa mnataka kuvuna



Sura: AL-QALAM 

Aya : 23

فَٱنطَلَقُواْ وَهُمۡ يَتَخَٰفَتُونَ

Wakatoka na huku wanakwenda kimya kimya wakinong’onezana



Sura: AL-QALAM 

Aya : 24

أَن لَّا يَدۡخُلَنَّهَا ٱلۡيَوۡمَ عَلَيۡكُم مِّسۡكِينٞ

Wakisema kwamba:: leo Maskini asiingie humo mwenu kinyume cha utashi wenu



Sura: AL-QALAM 

Aya : 25

وَغَدَوۡاْ عَلَىٰ حَرۡدٖ قَٰدِرِينَ

Wakatoka asubuhi mapema kwa kusudio la nguvu, wakidhani wana uwezo (wa kuwazuia maskini)



Sura: AL-QALAM 

Aya : 26

فَلَمَّا رَأَوۡهَا قَالُوٓاْ إِنَّا لَضَآلُّونَ

Basi walipoliona (shamba lao) wakasema: Hakika sisi bila shaka Tumepotea



Sura: AL-QALAM 

Aya : 27

بَلۡ نَحۡنُ مَحۡرُومُونَ

(Walivyo tanabahi!): wakasema Bali sisi tumenyimwa (mavuno yake)!



Sura: AL-QALAM 

Aya : 28

قَالَ أَوۡسَطُهُمۡ أَلَمۡ أَقُل لَّكُمۡ لَوۡلَا تُسَبِّحُونَ

Mbora wao akasema: Sikukwambieni, kwa nini hamumtakasi Allah (kuiacha nia yenu mbaya)?



Sura: AL-QALAM 

Aya : 29

قَالُواْ سُبۡحَٰنَ رَبِّنَآ إِنَّا كُنَّا ظَٰلِمِينَ

Wakasema: utukufu ni wa mola wetu, hakika tulikuwa wenye kudhulumu



Sura: AL-QALAM 

Aya : 30

فَأَقۡبَلَ بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ يَتَلَٰوَمُونَ

Basi Wakakabiliana wenyewe kwa wenyewe wakilaumiana