Sura: ATTAHRIIM 

Aya : 1

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَآ أَحَلَّ ٱللَّهُ لَكَۖ تَبۡتَغِي مَرۡضَاتَ أَزۡوَٰجِكَۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Ewe Nabii, kwa nini unaharamisha kile Allah alichokuhalalishia ukitafuta kuwaridhisha wake zako? Na Allah ni Mwingi wa kusamehe, Rahimu sana



Sura: ATTAHRIIM 

Aya : 2

قَدۡ فَرَضَ ٱللَّهُ لَكُمۡ تَحِلَّةَ أَيۡمَٰنِكُمۡۚ وَٱللَّهُ مَوۡلَىٰكُمۡۖ وَهُوَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡحَكِيمُ

Allah amekwisha kufaradhishieni (amekupeni sharia) ya kufungua (kutengua) viapo vyenu, na Allah ni Mola wenu, Naye ndiye Mjuzi wa yote, Mwenye hekima sana



Sura: ATTAHRIIM 

Aya : 3

وَإِذۡ أَسَرَّ ٱلنَّبِيُّ إِلَىٰ بَعۡضِ أَزۡوَٰجِهِۦ حَدِيثٗا فَلَمَّا نَبَّأَتۡ بِهِۦ وَأَظۡهَرَهُ ٱللَّهُ عَلَيۡهِ عَرَّفَ بَعۡضَهُۥ وَأَعۡرَضَ عَنۢ بَعۡضٖۖ فَلَمَّا نَبَّأَهَا بِهِۦ قَالَتۡ مَنۡ أَنۢبَأَكَ هَٰذَاۖ قَالَ نَبَّأَنِيَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡخَبِيرُ

Na (kumbuka) wakati Nabii alipomwambia mmoja wa wake zake jambo la siri. Basi alipolitangaza yule mke, na Allah akamdhihirishia Mtume, alimjuza sehemu na akaacha sehemu nyingine. Basi (Mtume) alipomwambia hayo, (mke) akasema: Nani aliyekuambia haya? (Mtume) Akasema: Ameniambia (Allah) Mjuzi sana, Mwenye habari zote



Sura: ATTAHRIIM 

Aya : 4

إِن تَتُوبَآ إِلَى ٱللَّهِ فَقَدۡ صَغَتۡ قُلُوبُكُمَاۖ وَإِن تَظَٰهَرَا عَلَيۡهِ فَإِنَّ ٱللَّهَ هُوَ مَوۡلَىٰهُ وَجِبۡرِيلُ وَصَٰلِحُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۖ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ بَعۡدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ

Ikiwa nyinyi wawili mtatubia kwa Allah (ni kheri kwenu) kwani kwa hakika nyoyo zenu zimeelemea (yanayomchukiza Mtume). Na mkisaidiana dhidi yake, basi hakika Allah Ndiye Mlinzi Msaidizi wake kipenzi chake, na Jibrili na Waumini wema, na zaidi ya hayo, Malaika pia watasaidia



Sura: ATTAHRIIM 

Aya : 5

عَسَىٰ رَبُّهُۥٓ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبۡدِلَهُۥٓ أَزۡوَٰجًا خَيۡرٗا مِّنكُنَّ مُسۡلِمَٰتٖ مُّؤۡمِنَٰتٖ قَٰنِتَٰتٖ تَـٰٓئِبَٰتٍ عَٰبِدَٰتٖ سَـٰٓئِحَٰتٖ ثَيِّبَٰتٖ وَأَبۡكَارٗا

Akikutalikini, asaa Mola Wake Akambadilishia wake bora kuliko nyinyi; Waislamu (wanyenyekevu), Waumini, watiifu na wanyenyekevu, wanaotubia, wenye kufanya ‘Ibaadah, wanaofunga, wajane, na walio bikra.(wanawari)



Sura: ATTAHRIIM 

Aya : 6

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ قُوٓاْ أَنفُسَكُمۡ وَأَهۡلِيكُمۡ نَارٗا وَقُودُهَا ٱلنَّاسُ وَٱلۡحِجَارَةُ عَلَيۡهَا مَلَـٰٓئِكَةٌ غِلَاظٞ شِدَادٞ لَّا يَعۡصُونَ ٱللَّهَ مَآ أَمَرَهُمۡ وَيَفۡعَلُونَ مَا يُؤۡمَرُونَ

Enyi walioamini! Jikingeni nafsi zenu na ahli zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe; Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Allah kwa yale Anayowaamrisha na wanafanya yale wanayoamrishwa



Sura: ATTAHRIIM 

Aya : 7

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَا تَعۡتَذِرُواْ ٱلۡيَوۡمَۖ إِنَّمَا تُجۡزَوۡنَ مَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

(Siku hiyo ya kiyama wataambiwa) Enyi mlio kufuru! Msilete udhuru leo. Hakika mnalipwa mliyo kuwa mkiyatenda



Sura: ATTAHRIIM 

Aya : 8

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ تُوبُوٓاْ إِلَى ٱللَّهِ تَوۡبَةٗ نَّصُوحًا عَسَىٰ رَبُّكُمۡ أَن يُكَفِّرَ عَنكُمۡ سَيِّـَٔاتِكُمۡ وَيُدۡخِلَكُمۡ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ يَوۡمَ لَا يُخۡزِي ٱللَّهُ ٱلنَّبِيَّ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥۖ نُورُهُمۡ يَسۡعَىٰ بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَبِأَيۡمَٰنِهِمۡ يَقُولُونَ رَبَّنَآ أَتۡمِمۡ لَنَا نُورَنَا وَٱغۡفِرۡ لَنَآۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Enyi walioamini! Tubieni kwa Allah tawbah ya kwelikweli; Asaa Mola wenu Akakufutieni maovu yenu, na Akakuingizeni katika Pepo zipitazo mito kati yake. Siku ambayo Allah Hatomfedhehesha Nabii na wale walioamini pamoja naye. Nuru yao itatembea mbele yao na kuliani mwao, watasema: Ee Mola wetu! Tutimizie Nuru yetu, na Tusamehe, hakika Wewe juu ya kila kitu ni Muweza



Sura: ATTAHRIIM 

Aya : 9

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ جَٰهِدِ ٱلۡكُفَّارَ وَٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱغۡلُظۡ عَلَيۡهِمۡۚ وَمَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ

Ee Nabii! Pambana na makafiri na wanafiki na kuwa mshupavu kwao, na makazi yao ni Motoni. Na ni mahali pabaya palioje pa kufikia



Sura: ATTAHRIIM 

Aya : 10

ضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلٗا لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱمۡرَأَتَ نُوحٖ وَٱمۡرَأَتَ لُوطٖۖ كَانَتَا تَحۡتَ عَبۡدَيۡنِ مِنۡ عِبَادِنَا صَٰلِحَيۡنِ فَخَانَتَاهُمَا فَلَمۡ يُغۡنِيَا عَنۡهُمَا مِنَ ٱللَّهِ شَيۡـٔٗا وَقِيلَ ٱدۡخُلَا ٱلنَّارَ مَعَ ٱلدَّـٰخِلِينَ

Allah Amewapigia mfano wale waliokufuru; kwa mke wa Nuhu na mke wa Luutwi. Wote wawili walikuwa chini ya waja wawili miongoni mwa waja Wetu Wema; wakawafanyia khiana, basi (Manabii hao) hawakuwafaa chochote mbele ya Allah, na ikasemwa: Ingieni Motoni pamoja na wenye kuingia



Sura: ATTAHRIIM 

Aya : 11

وَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلٗا لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱمۡرَأَتَ فِرۡعَوۡنَ إِذۡ قَالَتۡ رَبِّ ٱبۡنِ لِي عِندَكَ بَيۡتٗا فِي ٱلۡجَنَّةِ وَنَجِّنِي مِن فِرۡعَوۡنَ وَعَمَلِهِۦ وَنَجِّنِي مِنَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Na Allah Amewapigia mfano wale walioamini; kwa mke wa Firauni, aliposema: Ee Mola wangu! Nijengee nyumba Kwako kwenye Pepo na niokoe na Firauni na vitendo vyake na niokoe na watu madhalimu



Sura: ATTAHRIIM 

Aya : 12

وَمَرۡيَمَ ٱبۡنَتَ عِمۡرَٰنَ ٱلَّتِيٓ أَحۡصَنَتۡ فَرۡجَهَا فَنَفَخۡنَا فِيهِ مِن رُّوحِنَا وَصَدَّقَتۡ بِكَلِمَٰتِ رَبِّهَا وَكُتُبِهِۦ وَكَانَتۡ مِنَ ٱلۡقَٰنِتِينَ

Na Mariamu binti wa ‘Imrani ambaye amehifadhi tupu yake (aliye linda ubikira wake), Tukampulizia humo (katika nguo yake) kupitia kwa Roho Wetu (Jibrili), na akasadikisha Maneno ya Mola wake, na Vitabu Vyake, na akawa miongoni mwa watiifu na wanyenyekevu