Sura: AL-MUMTAHINA 

Aya : 1

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُواْ عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمۡ أَوۡلِيَآءَ تُلۡقُونَ إِلَيۡهِم بِٱلۡمَوَدَّةِ وَقَدۡ كَفَرُواْ بِمَا جَآءَكُم مِّنَ ٱلۡحَقِّ يُخۡرِجُونَ ٱلرَّسُولَ وَإِيَّاكُمۡ أَن تُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ رَبِّكُمۡ إِن كُنتُمۡ خَرَجۡتُمۡ جِهَٰدٗا فِي سَبِيلِي وَٱبۡتِغَآءَ مَرۡضَاتِيۚ تُسِرُّونَ إِلَيۡهِم بِٱلۡمَوَدَّةِ وَأَنَا۠ أَعۡلَمُ بِمَآ أَخۡفَيۡتُمۡ وَمَآ أَعۡلَنتُمۡۚ وَمَن يَفۡعَلۡهُ مِنكُمۡ فَقَدۡ ضَلَّ سَوَآءَ ٱلسَّبِيلِ

Enyi mlioamini, msiwafanye adui zangu na adui zenu wandani mnao wamwagia upendo na ilhali wao kwa hakika wameikufuru haki iliyokujieni. Wanamtoa Mtume na (pia wanakutoeni) nyinyi msimuamini Allah, Mola wenu Mlezi. Ikiwa nyinyi (kweli) mmetoka kwa ajili ya Jihadi katika Njia yangu na kutafuta radhi zangu (basi msifanye hivyo). (Hivi) Mnafanya nao urafiki kwa siri, na ilhali Mimi ninayajua sana mnayoyaficha na mnayoyadhihirisha? Na yeyote mwenye kufanya hayo kati yenu, basi kwa hakika kabisa amepotea njia ya sawa



Sura: AL-MUMTAHINA 

Aya : 2

إِن يَثۡقَفُوكُمۡ يَكُونُواْ لَكُمۡ أَعۡدَآءٗ وَيَبۡسُطُوٓاْ إِلَيۡكُمۡ أَيۡدِيَهُمۡ وَأَلۡسِنَتَهُم بِٱلسُّوٓءِ وَوَدُّواْ لَوۡ تَكۡفُرُونَ

(Makafiri) Wakikutana nanyi (na wakapata nafasi na mamlaka ya kuwa juu yenu na kukushindeni) wanakuwa maadui wenu na wanakunyosheeni mikono yao na ndimi zao kwa uovu na wanatamani lau mkufuru (kama wao walivyokufuru ili nyinyi na wao muwe sawa)



Sura: AL-MUMTAHINA 

Aya : 3

لَن تَنفَعَكُمۡ أَرۡحَامُكُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُكُمۡۚ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يَفۡصِلُ بَيۡنَكُمۡۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ

Hautakufaeni udugu wenu wala watoto wenu. Siku ya Kiyama Allah atapambanua (atatenganisha) baina yenu, na Allah anayaona vyema mnayoyatenda



Sura: AL-MUMTAHINA 

Aya : 4

قَدۡ كَانَتۡ لَكُمۡ أُسۡوَةٌ حَسَنَةٞ فِيٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥٓ إِذۡ قَالُواْ لِقَوۡمِهِمۡ إِنَّا بُرَءَـٰٓؤُاْ مِنكُمۡ وَمِمَّا تَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ كَفَرۡنَا بِكُمۡ وَبَدَا بَيۡنَنَا وَبَيۡنَكُمُ ٱلۡعَدَٰوَةُ وَٱلۡبَغۡضَآءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ وَحۡدَهُۥٓ إِلَّا قَوۡلَ إِبۡرَٰهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسۡتَغۡفِرَنَّ لَكَ وَمَآ أَمۡلِكُ لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٖۖ رَّبَّنَا عَلَيۡكَ تَوَكَّلۡنَا وَإِلَيۡكَ أَنَبۡنَا وَإِلَيۡكَ ٱلۡمَصِيرُ

Hakika, nyinyi mna mfano mzuri wa kuiga kwa (Mtume) Ibrahim na wale waliokuwa pamoja naye wakati walipowaambia watu wao kwamba: Hakika, sisi ni wenye kujitenga nanyi na (pia ni wenye kujitenga na) hao (Miungu masanamu) mnaowaabudu badala ya Allah. Tumekukataeni na umekwishadhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapomuamini Allah pekee. Isipokuwa kauli ya Ibrahim ya kumwambia baba yake kwamba: Hakika, nitakuombea msamaha na si miliki chochote kwa Allah kwa ajili yako. Ewe Mola wetu, tumekutegemea wewe tu, na tumetubu kwako tu, na kwako tu ndio marejeo (ya wote)



Sura: AL-MUMTAHINA 

Aya : 5

رَبَّنَا لَا تَجۡعَلۡنَا فِتۡنَةٗ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ وَٱغۡفِرۡ لَنَا رَبَّنَآۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Ee Mola wetu! Usitujaalie kuwa mtihani kwa wale waliokufuru, na Utusamehe Ee Mola wetu; Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima



Sura: AL-MUMTAHINA 

Aya : 6

لَقَدۡ كَانَ لَكُمۡ فِيهِمۡ أُسۡوَةٌ حَسَنَةٞ لِّمَن كَانَ يَرۡجُواْ ٱللَّهَ وَٱلۡيَوۡمَ ٱلۡأٓخِرَۚ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡغَنِيُّ ٱلۡحَمِيدُ

Kwa yakini imekuwa kwenu kigezo kizuri katika mwenendo wao kwa mwenye kumtaraji Allah na Siku ya Mwisho. Na mwenye kugeuka basi hakika Allah ni Mwenye kujitosha, Msifiwa



Sura: AL-MUMTAHINA 

Aya : 7

۞عَسَى ٱللَّهُ أَن يَجۡعَلَ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَ ٱلَّذِينَ عَادَيۡتُم مِّنۡهُم مَّوَدَّةٗۚ وَٱللَّهُ قَدِيرٞۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Asaa Mwenyezi Mungu akatia mapenzi baina yenu na hao maadui zenu, na Allah ni Mweza, na Allah ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu



Sura: AL-MUMTAHINA 

Aya : 8

لَّا يَنۡهَىٰكُمُ ٱللَّهُ عَنِ ٱلَّذِينَ لَمۡ يُقَٰتِلُوكُمۡ فِي ٱلدِّينِ وَلَمۡ يُخۡرِجُوكُم مِّن دِيَٰرِكُمۡ أَن تَبَرُّوهُمۡ وَتُقۡسِطُوٓاْ إِلَيۡهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُقۡسِطِينَ

Allah Hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale wasiokupigeni vita katika Dini, na wala hawaku-kutoeni kutoka majumbani mwenu. Hakika Allah Anawapenda wafanyao uadilifu



Sura: AL-MUMTAHINA 

Aya : 9

إِنَّمَا يَنۡهَىٰكُمُ ٱللَّهُ عَنِ ٱلَّذِينَ قَٰتَلُوكُمۡ فِي ٱلدِّينِ وَأَخۡرَجُوكُم مِّن دِيَٰرِكُمۡ وَظَٰهَرُواْ عَلَىٰٓ إِخۡرَاجِكُمۡ أَن تَوَلَّوۡهُمۡۚ وَمَن يَتَوَلَّهُمۡ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ

Hakika Allah anaku-katazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wa-fanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu



Sura: AL-MUMTAHINA 

Aya : 10

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا جَآءَكُمُ ٱلۡمُؤۡمِنَٰتُ مُهَٰجِرَٰتٖ فَٱمۡتَحِنُوهُنَّۖ ٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِإِيمَٰنِهِنَّۖ فَإِنۡ عَلِمۡتُمُوهُنَّ مُؤۡمِنَٰتٖ فَلَا تَرۡجِعُوهُنَّ إِلَى ٱلۡكُفَّارِۖ لَا هُنَّ حِلّٞ لَّهُمۡ وَلَا هُمۡ يَحِلُّونَ لَهُنَّۖ وَءَاتُوهُم مَّآ أَنفَقُواْۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ أَن تَنكِحُوهُنَّ إِذَآ ءَاتَيۡتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّۚ وَلَا تُمۡسِكُواْ بِعِصَمِ ٱلۡكَوَافِرِ وَسۡـَٔلُواْ مَآ أَنفَقۡتُمۡ وَلۡيَسۡـَٔلُواْ مَآ أَنفَقُواْۚ ذَٰلِكُمۡ حُكۡمُ ٱللَّهِ يَحۡكُمُ بَيۡنَكُمۡۖ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ

Enyi walioamini! Wanapokujieni Waumini wa kike waliohajiri (waliohama) basi wajaribuni. Allah ndiye Mwenye kujua zaidi Imani yao. Kisha mkiwatambua kuwa ni Waumini basi msiwarejeshe kwa makafiri. Wao si wake halaal kwao, wala hao makafiri hawahalalikii wanawake Waumini. Na wapeni (makafiri mahari) waliyotoa. Na wala si dhambi kufunga nao ndoa mkiwapa mahari yao. Na wala msiwaweke wanawake makafiri katika fungamano la ndoa; na takeni mlichotoa (katika mahari), nao watake walichotoa. Hiyo ndio hukumu ya Allah, Ana hukumu baina yenu, na Allah ni Mwenye kujua, Mwenye hekima



Sura: AL-MUMTAHINA 

Aya : 11

وَإِن فَاتَكُمۡ شَيۡءٞ مِّنۡ أَزۡوَٰجِكُمۡ إِلَى ٱلۡكُفَّارِ فَعَاقَبۡتُمۡ فَـَٔاتُواْ ٱلَّذِينَ ذَهَبَتۡ أَزۡوَٰجُهُم مِّثۡلَ مَآ أَنفَقُواْۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ ٱلَّذِيٓ أَنتُم بِهِۦ مُؤۡمِنُونَ

Na kama akikutorokeni yeyote kati ya wake zenu kurejea kwa makafiri kisha ikatokea kuwa mmelipiza mkashinda na kupata ngawira, basi wapeni wale walio ondokewa na wake zao mfano wa walichotoa (mahari); na mcheni Allah Ambaye nyinyi Kwake mnamuamini



Sura: AL-MUMTAHINA 

Aya : 12

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ إِذَا جَآءَكَ ٱلۡمُؤۡمِنَٰتُ يُبَايِعۡنَكَ عَلَىٰٓ أَن لَّا يُشۡرِكۡنَ بِٱللَّهِ شَيۡـٔٗا وَلَا يَسۡرِقۡنَ وَلَا يَزۡنِينَ وَلَا يَقۡتُلۡنَ أَوۡلَٰدَهُنَّ وَلَا يَأۡتِينَ بِبُهۡتَٰنٖ يَفۡتَرِينَهُۥ بَيۡنَ أَيۡدِيهِنَّ وَأَرۡجُلِهِنَّ وَلَا يَعۡصِينَكَ فِي مَعۡرُوفٖ فَبَايِعۡهُنَّ وَٱسۡتَغۡفِرۡ لَهُنَّ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Ewe Nabii! Wakikujia Waumini wa kike wanafungamana nawe ahadi ya utiifu kwamba hawata mshirikisha Allah na chochote, na wala hawatoiba, na wala hawatozini, na wala hawataua watoto wao, na wala hawatoleta usingiziaji wa kashfa walioizua baina ya mikono yao na miguu yao na wala hawatakuasi katika mema; basi pokea ahadi yao ya utiifu, na waombee maghfirah kwa Allaah. Hakika Allah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu



Sura: AL-MUMTAHINA 

Aya : 13

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَوَلَّوۡاْ قَوۡمًا غَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡ قَدۡ يَئِسُواْ مِنَ ٱلۡأٓخِرَةِ كَمَا يَئِسَ ٱلۡكُفَّارُ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡقُبُورِ

Enyi mlio amini! Msiwafanye rafiki zenu watu ambao Allah amewakasirikia. Hao wamekwisha kata tamaa ya Akhera, kama makafiri walivyo wakatia tamaa watu wa makaburini