وَٱلصَّـٰٓفَّـٰتِ صَفّٗا
Nina apa kwa wanao jipanga kwa safu
Kushiriki :
فَٱلزَّـٰجِرَٰتِ زَجۡرٗا
Na wenye kukemea mabaya
فَٱلتَّـٰلِيَٰتِ ذِكۡرًا
Na wenye kusoma ukumbusho
إِنَّ إِلَٰهَكُمۡ لَوَٰحِدٞ
(Kwamba) Hakika kabisa, Mungu wenu ni Mmoja tu
رَّبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا وَرَبُّ ٱلۡمَشَٰرِقِ
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yao, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote
إِنَّا زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنۡيَا بِزِينَةٍ ٱلۡكَوَاكِبِ
Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota
وَحِفۡظٗا مِّن كُلِّ شَيۡطَٰنٖ مَّارِدٖ
Na kwa ajili ya ulinzi dhidi ya kila shetani muasi
لَّا يَسَّمَّعُونَ إِلَى ٱلۡمَلَإِ ٱلۡأَعۡلَىٰ وَيُقۡذَفُونَ مِن كُلِّ جَانِبٖ
Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande
دُحُورٗاۖ وَلَهُمۡ عَذَابٞ وَاصِبٌ
Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu
إِلَّا مَنۡ خَطِفَ ٱلۡخَطۡفَةَ فَأَتۡبَعَهُۥ شِهَابٞ ثَاقِبٞ
Isipo kuwa anayenyakua kitu kidogo, na mara humfuatia kimondo kinacho ng’ara
فَٱسۡتَفۡتِهِمۡ أَهُمۡ أَشَدُّ خَلۡقًا أَم مَّنۡ خَلَقۡنَآۚ إِنَّا خَلَقۡنَٰهُم مِّن طِينٖ لَّازِبِۭ
Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tulio waumba? Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unao nata
بَلۡ عَجِبۡتَ وَيَسۡخَرُونَ
Bali unastaajabu, na wao wanafanya maskhara
وَإِذَا ذُكِّرُواْ لَا يَذۡكُرُونَ
Na wanapo kumbushwa hawakumbuki
وَإِذَا رَأَوۡاْ ءَايَةٗ يَسۡتَسۡخِرُونَ
Na wanapo ona Ishara, wanafanya maskhara
وَقَالُوٓاْ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ مُّبِينٌ
Na husema: Haya si chochote ila ni uchawi tu ulio dhaahiri
أَءِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ
Ati tukisha kufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa?
أَوَءَابَآؤُنَا ٱلۡأَوَّلُونَ
Hata baba zetu wa zamani?
قُلۡ نَعَمۡ وَأَنتُمۡ دَٰخِرُونَ
Sema: Naam! (Mtafufuliwa) Hali nanyi ni madhalili
فَإِنَّمَا هِيَ زَجۡرَةٞ وَٰحِدَةٞ فَإِذَا هُمۡ يَنظُرُونَ
Huko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndio wataona!
وَقَالُواْ يَٰوَيۡلَنَا هَٰذَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ
Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo
هَٰذَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِ ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ
Hii ndiyo Siku ya Hukumu mliyokuwa mnaikadhibisha
۞ٱحۡشُرُواْ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ وَأَزۡوَٰجَهُمۡ وَمَا كَانُواْ يَعۡبُدُونَ
Wakusanyeni walio dhulumu, na wake zao, na hao walio kuwa wakiwaabudu
مِن دُونِ ٱللَّهِ فَٱهۡدُوهُمۡ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلۡجَحِيمِ
Badala ya Allah. Waongozeni njia ya Jahannamu!
وَقِفُوهُمۡۖ إِنَّهُم مَّسۡـُٔولُونَ
Na wasimamisheni. Hakika hao wataulizwa:
مَا لَكُمۡ لَا تَنَاصَرُونَ
Mna nini? Mbona hamsaidiani?
بَلۡ هُمُ ٱلۡيَوۡمَ مُسۡتَسۡلِمُونَ
Bali hii leo, watasalimu amri
وَأَقۡبَلَ بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ يَتَسَآءَلُونَ
Watakabiliana wao kwa wao kuulizana
قَالُوٓاْ إِنَّكُمۡ كُنتُمۡ تَأۡتُونَنَا عَنِ ٱلۡيَمِينِ
Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia
قَالُواْ بَل لَّمۡ تَكُونُواْ مُؤۡمِنِينَ
Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini
وَمَا كَانَ لَنَا عَلَيۡكُم مِّن سُلۡطَٰنِۭۖ بَلۡ كُنتُمۡ قَوۡمٗا طَٰغِينَ
Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu