Sura: AL-HIJRI 

Aya : 1

الٓرۚ تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِ وَقُرۡءَانٖ مُّبِينٖ

Alif Lam Raa. Hizi ni Aya za Kitabu na Qur’ani inayobainisha



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 2

رُّبَمَا يَوَدُّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَوۡ كَانُواْ مُسۡلِمِينَ

Watatamani makafiri (Siku ya Kiyama) laiti na wao wangekuwa Waislamu



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 3

ذَرۡهُمۡ يَأۡكُلُواْ وَيَتَمَتَّعُواْ وَيُلۡهِهِمُ ٱلۡأَمَلُۖ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ

(Ewe Mtume) Waache (hao makafiri) wale na wastarehe, na liwapumbaze tumaini la uongo. (mwishowe) Watakuja kujua



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 4

وَمَآ أَهۡلَكۡنَا مِن قَرۡيَةٍ إِلَّا وَلَهَا كِتَابٞ مَّعۡلُومٞ

Na hatukuuangamiza mji wowote ule ila ulikuwa na muda wake maalumu (uliowekwa kimaangamizi)



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 5

مَّا تَسۡبِقُ مِنۡ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسۡتَـٔۡخِرُونَ

Hautangulii muda wa (kuangamizwa kwa) kaumu yoyote (ile), wala hawacheleweshwi



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 6

وَقَالُواْ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِي نُزِّلَ عَلَيۡهِ ٱلذِّكۡرُ إِنَّكَ لَمَجۡنُونٞ

Na (Washirikina) walisema (kwa lugha ya kebehi): Ewe uliyeteremshiwa Ukumbusho! Hakika wewe ni mwehu (kwa unayoyalingania)



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 7

لَّوۡمَا تَأۡتِينَا بِٱلۡمَلَـٰٓئِكَةِ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ

(Kama ni mkweli) Si utuletee Malaika (waje watuthibitishie Utume wako) ikiwa wewe ni miongoni mwa wanaosema kweli?



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 8

مَا نُنَزِّلُ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةَ إِلَّا بِٱلۡحَقِّ وَمَا كَانُوٓاْ إِذٗا مُّنظَرِينَ

(Allah akawajibu washirikina) Sisi hatuwateremshi Malaika ila kwa haki, na hapo (watakapoteremshwa Malaika) hawatapewa muhula



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 9

إِنَّا نَحۡنُ نَزَّلۡنَا ٱلذِّكۡرَ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَٰفِظُونَ

Hakika Sisi ndio tuliouteremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutakaoulinda



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 10

وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ فِي شِيَعِ ٱلۡأَوَّلِينَ

Na kwa hakika kabisa, tuliwatumia Mitume kwenye mataifa ya mwanzo



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 11

وَمَا يَأۡتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ

Na hakuwafikia Mtume yoyote isipokuwa hao (watu wake) walimdhihaki



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 12

كَذَٰلِكَ نَسۡلُكُهُۥ فِي قُلُوبِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ

Na kama tulivyoingiza (tabia ya ukafiri na shere kwa watu wa mwanzo dhidi ya Mitume wao) vivyo hivyo tunaingiza katika nyoyo za waovu (katika umati wako)



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 13

لَا يُؤۡمِنُونَ بِهِۦ وَقَدۡ خَلَتۡ سُنَّةُ ٱلۡأَوَّلِينَ

(Washirikina) Hawaiamini (hii) Qur’an (wala hawamuamini Mtume), na hali umeshawapitia mfano wa watu wa kale



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 14

وَلَوۡ فَتَحۡنَا عَلَيۡهِم بَابٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ فَظَلُّواْ فِيهِ يَعۡرُجُونَ

Na lau tungewafungulia (hawa washirikina) mlango wowote wa mbingu, wakawa wanapanda humo (na kushuhudia yaliyoko huko pia wasingeamini)



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 15

لَقَالُوٓاْ إِنَّمَا سُكِّرَتۡ أَبۡصَٰرُنَا بَلۡ نَحۡنُ قَوۡمٞ مَّسۡحُورُونَ

Basi (hawa washirikina) wangesema (kwa inadi): Macho yetu yamelevywa, bali sisi ni watu tuliorogwa



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 16

وَلَقَدۡ جَعَلۡنَا فِي ٱلسَّمَآءِ بُرُوجٗا وَزَيَّنَّـٰهَا لِلنَّـٰظِرِينَ

Na kwa hakika kabisa, tumeweka katika anga vituo vya sayari, na tumeipamba mbingu (hii ya dunia) kwa ajili ya watazamao (ili wapate mazingatio)



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 17

وَحَفِظۡنَٰهَا مِن كُلِّ شَيۡطَٰنٖ رَّجِيمٍ

Na (hilo anga) tunalilinda na kila Shetani aliyelaaniwa (ili asiweze kusikia Wahyi n.k)



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 18

إِلَّا مَنِ ٱسۡتَرَقَ ٱلسَّمۡعَ فَأَتۡبَعَهُۥ شِهَابٞ مُّبِينٞ

Isipokuwa kwa (Shetani) anayesikiliza kwa kuibia, naye hufuatwa na kimondo kinachoonekana (na kuteketezwa)



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 19

وَٱلۡأَرۡضَ مَدَدۡنَٰهَا وَأَلۡقَيۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ وَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا مِن كُلِّ شَيۡءٖ مَّوۡزُونٖ

Na ardhi tumeitandaza (ili maisha ya viumbe yawezekane) na humo tumeweka milima, na tumeotesha kila kitu kwa kipimo



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 20

وَجَعَلۡنَا لَكُمۡ فِيهَا مَعَٰيِشَ وَمَن لَّسۡتُمۡ لَهُۥ بِرَٰزِقِينَ

Na tukawawekeeni humo vitu (mnavyovihitajia) katika maisha yenu[1], na (pia tukajaalia maisha) ya hao ambao nyinyi sio wenye kuwaruzuku (isipokuwa Allah tu)


1- - Allah ndiye anayetoa vyakula, vinywaji, mavazi, makazi n.k. Na ndiye atoaye pia riziki za watoto wakila mtu, watumishi, wanyama n.k


Sura: AL-HIJRI 

Aya : 21

وَإِن مِّن شَيۡءٍ إِلَّا عِندَنَا خَزَآئِنُهُۥ وَمَا نُنَزِّلُهُۥٓ إِلَّا بِقَدَرٖ مَّعۡلُومٖ

Na hakuna chochote (chenye manufaa) isipokuwa hazina yake inatokana na Sisi; wala hatukiteremshi ila kwa kipimo maalumu (kulingana na mahitaji)



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 22

وَأَرۡسَلۡنَا ٱلرِّيَٰحَ لَوَٰقِحَ فَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَسۡقَيۡنَٰكُمُوهُ وَمَآ أَنتُمۡ لَهُۥ بِخَٰزِنِينَ

Na tunazipeleka pepo za kupandishia, na tunateremsha kutoka mawinguni maji, kisha tuka-kunywesheni maji hayo[1]. Wala si nyinyi mnayoyahifadhi


1- - Maji hayo ya mvua mnakunywa nyinyi, mifugo yenu, mnayatumia kwa kilimo, yanasafisha mazingira ardhi, anga, n.k


Sura: AL-HIJRI 

Aya : 23

وَإِنَّا لَنَحۡنُ نُحۡيِۦ وَنُمِيتُ وَنَحۡنُ ٱلۡوَٰرِثُونَ

Na kwa hakika Sisi ndio tunaohuisha na tunaofisha. Na Sisi ndio Warithi (wa viumbe na huu ulimwengu)



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 24

وَلَقَدۡ عَلِمۡنَا ٱلۡمُسۡتَقۡدِمِينَ مِنكُمۡ وَلَقَدۡ عَلِمۡنَا ٱلۡمُسۡتَـٔۡخِرِينَ

Na kwa hakika kabisa tunawajua waliotangulia (katika kuzaliwa na kufa) katika nyinyi, na tunawajua waliochelewa (vizazi vijavyo)



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 25

وَإِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَحۡشُرُهُمۡۚ إِنَّهُۥ حَكِيمٌ عَلِيمٞ

Na hakika Mola wako Mlezi ndiye atakayewakusanya (viumbe Siku ya Kiyama). Hakika Yeye ni Mwenye hekima Mjuzi sana



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 26

وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ مِن صَلۡصَٰلٖ مِّنۡ حَمَإٖ مَّسۡنُونٖ

Na tulimuumba mtu (wa kwanza) kwa udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope meusi yaliyovunda



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 27

وَٱلۡجَآنَّ خَلَقۡنَٰهُ مِن قَبۡلُ مِن نَّارِ ٱلسَّمُومِ

Na Majini tuliwaumba kabla (ya kumuumba Adamu) kwa miale ya moto



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 28

وَإِذۡ قَالَ رَبُّكَ لِلۡمَلَـٰٓئِكَةِ إِنِّي خَٰلِقُۢ بَشَرٗا مِّن صَلۡصَٰلٖ مِّنۡ حَمَإٖ مَّسۡنُونٖ

Na (kumbuka) Mola wako Mlezi alipowaambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope yaliyovunda



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 29

فَإِذَا سَوَّيۡتُهُۥ وَنَفَخۡتُ فِيهِ مِن رُّوحِي فَقَعُواْ لَهُۥ سَٰجِدِينَ

Basi nitakapomkamilisha na kumpulizia roho yangu, basi mumuangukie kwa kumsujudia



Sura: AL-HIJRI 

Aya : 30

فَسَجَدَ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ كُلُّهُمۡ أَجۡمَعُونَ

Basi Malaika wote kwa pamoja walimsujudia