Sura: AL-MAAUUN 

Aya : 1

أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي يُكَذِّبُ بِٱلدِّينِ

Je, umemuona anayekadhibisha (anayekataa) dini?



Sura: AL-MAAUUN 

Aya : 2

فَذَٰلِكَ ٱلَّذِي يَدُعُّ ٱلۡيَتِيمَ

Basi huyo ni anayemsukuma (na kumtelekeza) yatima



Sura: AL-MAAUUN 

Aya : 3

وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ

Wala hahimizi kumlisha (kumpa chakula) maskini



Sura: AL-MAAUUN 

Aya : 4

فَوَيۡلٞ لِّلۡمُصَلِّينَ

Basi, ole wao wanaoswali



Sura: AL-MAAUUN 

Aya : 5

ٱلَّذِينَ هُمۡ عَن صَلَاتِهِمۡ سَاهُونَ

Ambao wanapuuza Swala zao



Sura: AL-MAAUUN 

Aya : 6

ٱلَّذِينَ هُمۡ يُرَآءُونَ

Ambao wanaonyesha (matendo yao kwa watu ili wasifiwe)



Sura: AL-MAAUUN 

Aya : 7

وَيَمۡنَعُونَ ٱلۡمَاعُونَ

Na wanazuia msaada