۞أَوۡفُواْ ٱلۡكَيۡلَ وَلَا تَكُونُواْ مِنَ ٱلۡمُخۡسِرِينَ
Timizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe katika wanao punja
Kushiriki :
وَزِنُواْ بِٱلۡقِسۡطَاسِ ٱلۡمُسۡتَقِيمِ
Na pimeni kwa haki iliyo nyooka;
وَلَا تَبۡخَسُواْ ٱلنَّاسَ أَشۡيَآءَهُمۡ وَلَا تَعۡثَوۡاْ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُفۡسِدِينَ
Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri kwa ufisadi
وَٱتَّقُواْ ٱلَّذِي خَلَقَكُمۡ وَٱلۡجِبِلَّةَ ٱلۡأَوَّلِينَ
Na mcheni aliye kuumbeni nyinyi na vizazi vilivyo tangulia
قَالُوٓاْ إِنَّمَآ أَنتَ مِنَ ٱلۡمُسَحَّرِينَ
Wakasema: Hakika wewe ni katika walio rogwa
وَمَآ أَنتَ إِلَّا بَشَرٞ مِّثۡلُنَا وَإِن نَّظُنُّكَ لَمِنَ ٱلۡكَٰذِبِينَ
Na wewe si chochote ila ni mtu tu kama sisi, na kwa yakini tunakuona wewe ni katika waongo
فَأَسۡقِطۡ عَلَيۡنَا كِسَفٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ
Hebu tuangushie vipande kutoka mbinguni ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli
قَالَ رَبِّيٓ أَعۡلَمُ بِمَا تَعۡمَلُونَ
Akasema: Mola wangu Mlezi anajua zaidi mnayo yatenda
فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمۡ عَذَابُ يَوۡمِ ٱلظُّلَّةِۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٍ
Basi walimkanusha, na ikawashika adhabu ya siku ya kivuli. Hakika hiyo ilikuwa adhabu ya siku kubwa
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ
Hakika katika hayo ipo Ishara, lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu
وَإِنَّهُۥ لَتَنزِيلُ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na bila ya shaka huu ni Uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu wote
نَزَلَ بِهِ ٱلرُّوحُ ٱلۡأَمِينُ
Ameuteremsha Roho mua-minifu,(jibril)
عَلَىٰ قَلۡبِكَ لِتَكُونَ مِنَ ٱلۡمُنذِرِينَ
Juu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji,
بِلِسَانٍ عَرَبِيّٖ مُّبِينٖ
Kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi
وَإِنَّهُۥ لَفِي زُبُرِ ٱلۡأَوَّلِينَ
Na hakika bila ya shaka haya yamo katika Vitabu vya kale
أَوَلَمۡ يَكُن لَّهُمۡ ءَايَةً أَن يَعۡلَمَهُۥ عُلَمَـٰٓؤُاْ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ
Je! Haikuwa kwao ni Ishara kwamba wanayajua haya wanazuoni wa Wana wa Israili?
وَلَوۡ نَزَّلۡنَٰهُ عَلَىٰ بَعۡضِ ٱلۡأَعۡجَمِينَ
Na lau kuwa tungeli iteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu,
فَقَرَأَهُۥ عَلَيۡهِم مَّا كَانُواْ بِهِۦ مُؤۡمِنِينَ
Na akawasomea, wasingeli kuwa wenye kuamini
كَذَٰلِكَ سَلَكۡنَٰهُ فِي قُلُوبِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ
Namna hivi tunaingiza katika nyoyo za wakosefu
لَا يُؤۡمِنُونَ بِهِۦ حَتَّىٰ يَرَوُاْ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَلِيمَ
Hawataiamini mpaka waione adhabu chungu
فَيَأۡتِيَهُم بَغۡتَةٗ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ
Basi itawafikia kwa ghafla, na hali hawana khabari
فَيَقُولُواْ هَلۡ نَحۡنُ مُنظَرُونَ
Na watasema: Je, tutapewa muhula?
أَفَبِعَذَابِنَا يَسۡتَعۡجِلُونَ
Basi, je, wanaihimiza adhabu yetu?
أَفَرَءَيۡتَ إِن مَّتَّعۡنَٰهُمۡ سِنِينَ
Waonaje kama tukiwastarehesha kwa miaka
ثُمَّ جَآءَهُم مَّا كَانُواْ يُوعَدُونَ
Kisha yakawafikia waliyo kuwa wakiahidiwa,
مَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يُمَتَّعُونَ
Yatawafaa nini yale waliyo stareheshewa?
وَمَآ أَهۡلَكۡنَا مِن قَرۡيَةٍ إِلَّا لَهَا مُنذِرُونَ
Wala hatukuangamiza mji wowote ila ulikuwa na waonyaji
ذِكۡرَىٰ وَمَا كُنَّا ظَٰلِمِينَ
Kuwa ni ukumbusho. Wala Sisi hatukuwa wenye kudhulumu
وَمَا تَنَزَّلَتۡ بِهِ ٱلشَّيَٰطِينُ
Wala Mashet’ani hawakuteremka nayo,