Sura: ATTAUBA 

Aya : 121

وَلَا يُنفِقُونَ نَفَقَةٗ صَغِيرَةٗ وَلَا كَبِيرَةٗ وَلَا يَقۡطَعُونَ وَادِيًا إِلَّا كُتِبَ لَهُمۡ لِيَجۡزِيَهُمُ ٱللَّهُ أَحۡسَنَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Na hawatoi cha kutoa; kidogo wala kikubwa, wala hawavuki bonde (wawapo njiani), ila huandikiwa (mema) ili Allah awalipe mazuri zaidi ya waliyokuwa wakiyatenda



Sura: ATTAUBA 

Aya : 122

۞وَمَا كَانَ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ لِيَنفِرُواْ كَآفَّةٗۚ فَلَوۡلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرۡقَةٖ مِّنۡهُمۡ طَآئِفَةٞ لِّيَتَفَقَّهُواْ فِي ٱلدِّينِ وَلِيُنذِرُواْ قَوۡمَهُمۡ إِذَا رَجَعُوٓاْ إِلَيۡهِمۡ لَعَلَّهُمۡ يَحۡذَرُونَ

Na hawakutakiwa Waumini watoke wote (kwenda vitani). Basi kwa nini hawatoki baadhi katika kila kundi miongoni mwao, wakajifunze vyema Dini, na kisha waje kuwaonya wenzao watakaporejea kwao, ili nao wapate kujihadhari?



Sura: ATTAUBA 

Aya : 123

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ قَٰتِلُواْ ٱلَّذِينَ يَلُونَكُم مِّنَ ٱلۡكُفَّارِ وَلۡيَجِدُواْ فِيكُمۡ غِلۡظَةٗۚ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلۡمُتَّقِينَ

Enyi mlioamini, piganeni na wale makafiri walio mbele yenu na wakute kwenu ukali (ujasiri na ushupavu). Na jueni ya kwamba Allah yupo pamoja na wachaMungu



Sura: ATTAUBA 

Aya : 124

وَإِذَا مَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٞ فَمِنۡهُم مَّن يَقُولُ أَيُّكُمۡ زَادَتۡهُ هَٰذِهِۦٓ إِيمَٰنٗاۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فَزَادَتۡهُمۡ إِيمَٰنٗا وَهُمۡ يَسۡتَبۡشِرُونَ

Na inapoteremshwa Sura wapo miongoni mwao wanaosema (kwa kebehi): Ni nani miongoni mwenu Sura hii imemzidishia Imani? Basi ama wale walioamini imewazidishia Imani, nao wanafurahia



Sura: ATTAUBA 

Aya : 125

وَأَمَّا ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ فَزَادَتۡهُمۡ رِجۡسًا إِلَىٰ رِجۡسِهِمۡ وَمَاتُواْ وَهُمۡ كَٰفِرُونَ

Na ama wale ambao nyoyoni mwao mna maradhi (ya unafiki), basi (Sura) imewazidishia uchafu (uovu) juu ya uchafu (uovu) wao; na wanakufa hali ya kuwa ni makafiri



Sura: ATTAUBA 

Aya : 126

أَوَلَا يَرَوۡنَ أَنَّهُمۡ يُفۡتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٖ مَّرَّةً أَوۡ مَرَّتَيۡنِ ثُمَّ لَا يَتُوبُونَ وَلَا هُمۡ يَذَّكَّرُونَ

Je, hawaoni (wanafiki) ya kwamba wanatiwa mtihanini kila mwaka mara moja au mara mbili kisha hawatubu na hawakumbuki?



Sura: ATTAUBA 

Aya : 127

وَإِذَا مَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٞ نَّظَرَ بَعۡضُهُمۡ إِلَىٰ بَعۡضٍ هَلۡ يَرَىٰكُم مِّنۡ أَحَدٖ ثُمَّ ٱنصَرَفُواْۚ صَرَفَ ٱللَّهُ قُلُوبَهُم بِأَنَّهُمۡ قَوۡمٞ لَّا يَفۡقَهُونَ

Na ikiteremshwa Sura wanata-zamana (wanakonyezana) wao kwa wao, (kana kwamba wanasema): Je, kuna mtu yeyote anayekuoneni (mkiamua kuondoka kwa Mtume)? Kisha huondoka (kwa Mtume kwa kuogopa aibu). Allah amezigeuza nyoyo zao kwa kuwa hao ni watu wasiofahamu



Sura: ATTAUBA 

Aya : 128

لَقَدۡ جَآءَكُمۡ رَسُولٞ مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ عَزِيزٌ عَلَيۡهِ مَا عَنِتُّمۡ حَرِيصٌ عَلَيۡكُم بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ رَءُوفٞ رَّحِيمٞ

Kwa hakika kabisa, amekujieni Mtume anayetokana na nyinyi, kunamuumiza kutaabika kwenu, mwenye kukujalini sana (mwenye kuona mnafanikiwa) na kwa Waumini ni mpole sana, mwenye huruma sana



Sura: ATTAUBA 

Aya : 129

فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَقُلۡ حَسۡبِيَ ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُۖ وَهُوَ رَبُّ ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡعَظِيمِ

Basi (wanafiki na washirikishaji) wakikengeuka (wakipinga), wewe sema: Allah ananitosheleza. Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Yeye tu. Nimetegemea yeye tu, na Yeye tu ndiye Mola wa Arshi Tukufu