Sura: AL-IMRAN 

Aya : 121

وَإِذۡ غَدَوۡتَ مِنۡ أَهۡلِكَ تُبَوِّئُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ مَقَٰعِدَ لِلۡقِتَالِۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

Na kumbuka ulipotoka asubuhi mapema (ulipodamka) ukiiacha familia yako (ukaenda vitani ukawa) unawapangia Waumini maeneo ya mapambano (ya vita), na Allah ni Mwenye kusikia mno, Mjuzi sana



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 122

إِذۡ هَمَّت طَّآئِفَتَانِ مِنكُمۡ أَن تَفۡشَلَا وَٱللَّهُ وَلِيُّهُمَاۗ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ

Wakati Makundi mawili kati yenu yalipoingiwa na hofu ya kushindwa, na ilhali Allah ndiye Mlinzi wao. Na Waumini (wanatakiwa) wamtegemee Allah tu



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 123

وَلَقَدۡ نَصَرَكُمُ ٱللَّهُ بِبَدۡرٖ وَأَنتُمۡ أَذِلَّةٞۖ فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ

Na hakika, Allah alikunusuruni katika vita vya Badri na ilhali nyinyi ni wanyonge. Basi mcheni Allah ili mshukuru (ili mpate daraja ya kuwa wenye kushukuru)



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 124

إِذۡ تَقُولُ لِلۡمُؤۡمِنِينَ أَلَن يَكۡفِيَكُمۡ أَن يُمِدَّكُمۡ رَبُّكُم بِثَلَٰثَةِ ءَالَٰفٖ مِّنَ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةِ مُنزَلِينَ

Na (kumbuka) ulipowaambia Waumini: Hivi haitakutosheni Mola wenu kukuleteeni Malaika elfu tatu walioteremshwa?



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 125

بَلَىٰٓۚ إِن تَصۡبِرُواْ وَتَتَّقُواْ وَيَأۡتُوكُم مِّن فَوۡرِهِمۡ هَٰذَا يُمۡدِدۡكُمۡ رَبُّكُم بِخَمۡسَةِ ءَالَٰفٖ مِّنَ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةِ مُسَوِّمِينَ

Ni kweli kabisa; ikiwa mtakuwa na subira na mkamcha Allah na maadui wakakujieni kwa ghafla, basi hapo Mola wenu Mlezi atakuleteeni msaada wa Malaika elfu tano wenye kujiweka alama maalum



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 126

وَمَا جَعَلَهُ ٱللَّهُ إِلَّا بُشۡرَىٰ لَكُمۡ وَلِتَطۡمَئِنَّ قُلُوبُكُم بِهِۦۗ وَمَا ٱلنَّصۡرُ إِلَّا مِنۡ عِندِ ٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَكِيمِ

Na Allah hakufanya haya isipokuwa tu iwe bishara kwenu, na ili nyoyo zenu zipate utulivu kwayo, na hakuna nusura isipokuwa kutoka kwa Allah tu, Mwenye nguvu kubwa, Mwingi wa hekima



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 127

لِيَقۡطَعَ طَرَفٗا مِّنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَوۡ يَكۡبِتَهُمۡ فَيَنقَلِبُواْ خَآئِبِينَ

(Allah amefanya haya) Ili akate (aangamize) sehemu ya wale waliokufuru (kwa kuuawa vitani) au awafedheheshe wapate kurejea nyuma wakiwa hawakuambulia kitu



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 128

لَيۡسَ لَكَ مِنَ ٱلۡأَمۡرِ شَيۡءٌ أَوۡ يَتُوبَ عَلَيۡهِمۡ أَوۡ يُعَذِّبَهُمۡ فَإِنَّهُمۡ ظَٰلِمُونَ

Huna lako katika jambo (hili); ama (Allah) awakubalie toba (na kuwaongoa) au awaadhibu, kwa sababu wao ni madhalimu



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 129

وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ يَغۡفِرُ لِمَن يَشَآءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na ni vya Allah tu vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Ana msamehe amtakaye na anamuadhibu amtakaye. Na Allah ni Msamehevu sana, Mwenye rehema nyingi



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 130

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَأۡكُلُواْ ٱلرِّبَوٰٓاْ أَضۡعَٰفٗا مُّضَٰعَفَةٗۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ

Enyi mlioamini, msile Riba; ziada iliyozidishwa. Na mcheni Allah ili mpate kufaulu



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 131

وَٱتَّقُواْ ٱلنَّارَ ٱلَّتِيٓ أُعِدَّتۡ لِلۡكَٰفِرِينَ

Na ogopeni Moto ambao umeandaliwa kwa ajili ya Makafiri



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 132

وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ

Na mtiini Allah na Mtume ili mpate kupewa rehema



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 133

۞وَسَارِعُوٓاْ إِلَىٰ مَغۡفِرَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ وَجَنَّةٍ عَرۡضُهَا ٱلسَّمَٰوَٰتُ وَٱلۡأَرۡضُ أُعِدَّتۡ لِلۡمُتَّقِينَ

Na ukimbilieni msamaha wa Mola wenu Mlezi na Pepo (ambayo) upana wake ni mbingu na ardhi, iliyoandaliwa kwa ajili ya wacha Mungu



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 134

ٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ فِي ٱلسَّرَّآءِ وَٱلضَّرَّآءِ وَٱلۡكَٰظِمِينَ ٱلۡغَيۡظَ وَٱلۡعَافِينَ عَنِ ٱلنَّاسِۗ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

(Wacha Mungu) Ambao wanatoa (katika vile walivyopewa na Allah) katika hali ya wasaa na katika hali ya dhiki, na wenye kuzuia hasira (zao) na kusamehe watu (wanaowakosea). Na Allah anawapenda wafanyao mazuri



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 135

وَٱلَّذِينَ إِذَا فَعَلُواْ فَٰحِشَةً أَوۡ ظَلَمُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ ذَكَرُواْ ٱللَّهَ فَٱسۡتَغۡفَرُواْ لِذُنُوبِهِمۡ وَمَن يَغۡفِرُ ٱلذُّنُوبَ إِلَّا ٱللَّهُ وَلَمۡ يُصِرُّواْ عَلَىٰ مَا فَعَلُواْ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ

Na ambao wafanyapo uovu (wamadhambi makubwa) au wakazidhulumu nafsi zao (kwa kufanya madhambi madogo) wanamkumbuka Allah na kuomba msamaha kwa dhambi zao (hizo) na hakuna anayesamehe dhambi isipokuwa Allah tu, na hawaendelei kufanya (madhambi) waliyoyafanya na ilhali wanajua



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 136

أُوْلَـٰٓئِكَ جَزَآؤُهُم مَّغۡفِرَةٞ مِّن رَّبِّهِمۡ وَجَنَّـٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ وَنِعۡمَ أَجۡرُ ٱلۡعَٰمِلِينَ

Hao malipo yao ni msamaha wa Mola wao Mlezi na bustani zipitazo mito chini yake, watadumu humo milele, naujira bora kwawanaotenda (mema) ni huo



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 137

قَدۡ خَلَتۡ مِن قَبۡلِكُمۡ سُنَنٞ فَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَٱنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُكَذِّبِينَ

Yamepita kabla yenu mataifa (mengi)[1], basi tembeeni ardhini na muone ulikuwaje mwisho wa wanaokanusha (muongozo wa Allah)


1- - Makusudio hapa ni kuwakumbusha Waislamu kuwa, yamepita mataifa mengi yaliyokuwa na tabia na
nyendo za kupinga muongozo wa Allah na hatimae kuadhibiwa kwa adhabu za aina tafauti tafauti.
Waislamu hapa wanatakiwa kuyatembelea maeneo ya mataifa yaliyopita na ambayo yaliadhibiwa kwa
kutafakari na pia kwa kuona kwa macho lengo likiwa kupata maonyo na mafunzo na sio kutalii na
kuburudika.


Sura: AL-IMRAN 

Aya : 138

هَٰذَا بَيَانٞ لِّلنَّاسِ وَهُدٗى وَمَوۡعِظَةٞ لِّلۡمُتَّقِينَ

Huu ni ubainifu kwa watu, na ni uongofu na ni mawaidha kwa wacha Mungu



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 139

وَلَا تَهِنُواْ وَلَا تَحۡزَنُواْ وَأَنتُمُ ٱلۡأَعۡلَوۡنَ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Na msinyongee na msihuzunike na ilhali nyinyi ndio mlioko juu sana mkiwa ni Waumini (wa kweli)



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 140

إِن يَمۡسَسۡكُمۡ قَرۡحٞ فَقَدۡ مَسَّ ٱلۡقَوۡمَ قَرۡحٞ مِّثۡلُهُۥۚ وَتِلۡكَ ٱلۡأَيَّامُ نُدَاوِلُهَا بَيۡنَ ٱلنَّاسِ وَلِيَعۡلَمَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَيَتَّخِذَ مِنكُمۡ شُهَدَآءَۗ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Ikiwa yamekupateni majeraha, basi kwa hakika watu walipata majeraha kama hayo. Na hizo ni siku tunazizungusha kwa zamu kwa watu ili Allah awabainishe wale walioamini na afanye Mashahidi miongoni mwenu, na Allah hawapendi madhalimu



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 141

وَلِيُمَحِّصَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَيَمۡحَقَ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na ili Allah awasafishe ambao wameamini na awafute (awaangamize) makafiri



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 142

أَمۡ حَسِبۡتُمۡ أَن تَدۡخُلُواْ ٱلۡجَنَّةَ وَلَمَّا يَعۡلَمِ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ جَٰهَدُواْ مِنكُمۡ وَيَعۡلَمَ ٱلصَّـٰبِرِينَ

Hivi mlidhani kwamba, mtaingia Peponi na ilhali Allah hajawajua (hajawaweka hadharani) waliopigana Jihadi miongoni mwenu, na hajawajua wenye subira?



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 143

وَلَقَدۡ كُنتُمۡ تَمَنَّوۡنَ ٱلۡمَوۡتَ مِن قَبۡلِ أَن تَلۡقَوۡهُ فَقَدۡ رَأَيۡتُمُوهُ وَأَنتُمۡ تَنظُرُونَ

Na kwa hakika kabisa, nyinyi mlitamani mauti kabla hamjakutana nayo. Basi sasa mmeyaona na huku mnatazama



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 144

وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٞ قَدۡ خَلَتۡ مِن قَبۡلِهِ ٱلرُّسُلُۚ أَفَإِيْن مَّاتَ أَوۡ قُتِلَ ٱنقَلَبۡتُمۡ عَلَىٰٓ أَعۡقَٰبِكُمۡۚ وَمَن يَنقَلِبۡ عَلَىٰ عَقِبَيۡهِ فَلَن يَضُرَّ ٱللَّهَ شَيۡـٔٗاۚ وَسَيَجۡزِي ٱللَّهُ ٱلشَّـٰكِرِينَ

Na hakuwa Muhammadi isipokuwa ni Mtume tu. Hakika, wamepita Mitume (wengi) kabla yake. Hivi, akifa au akiuwawa ndiyo mtageuka mrudi nyuma? Na yeyote atakayegeuka (na) kurudi nyuma, basi hatamdhuru Allah chochote. Na Allah atawalipa wenye kushukuru



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 145

وَمَا كَانَ لِنَفۡسٍ أَن تَمُوتَ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِ كِتَٰبٗا مُّؤَجَّلٗاۗ وَمَن يُرِدۡ ثَوَابَ ٱلدُّنۡيَا نُؤۡتِهِۦ مِنۡهَا وَمَن يُرِدۡ ثَوَابَ ٱلۡأٓخِرَةِ نُؤۡتِهِۦ مِنۡهَاۚ وَسَنَجۡزِي ٱلشَّـٰكِرِينَ

Na nafsi yoyote haifi isipokuwa kwa idhini ya Allah tu ikiwa ni jambo lililoandikwa (na lenye) muda maalum. Na yeyote anayetaka malipo ya duniani tunampa humo, na mwenye kutaka malipo ya Akhera tutampa huko. Na tutawalipa wenye kushukuru



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 146

وَكَأَيِّن مِّن نَّبِيّٖ قَٰتَلَ مَعَهُۥ رِبِّيُّونَ كَثِيرٞ فَمَا وَهَنُواْ لِمَآ أَصَابَهُمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَمَا ضَعُفُواْ وَمَا ٱسۡتَكَانُواْۗ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلصَّـٰبِرِينَ

Na Manabii wengi wamepigana vita wakiwa pamoja na Waumini wao wengi watiifu. Hawakuwa wanyonge kutokana na yaliyowasibu katika njia ya Allah na hawakuwa dhaifu na hawakukubali kudhalilika, Na Allah anawapenda wenye kusubiri



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 147

وَمَا كَانَ قَوۡلَهُمۡ إِلَّآ أَن قَالُواْ رَبَّنَا ٱغۡفِرۡ لَنَا ذُنُوبَنَا وَإِسۡرَافَنَا فِيٓ أَمۡرِنَا وَثَبِّتۡ أَقۡدَامَنَا وَٱنصُرۡنَا عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na haikuwa kauli yao ila ni kusema tu: Ewe Mola wetu Mlezi, tusamehe madhambi yetu na kupita kwetu kiasi katika mambo yetu, na ithabitishe miguu yetu (tuimarishe) na tusaidie tuwashinde watu makafiri



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 148

فَـَٔاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ ثَوَابَ ٱلدُّنۡيَا وَحُسۡنَ ثَوَابِ ٱلۡأٓخِرَةِۗ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Basi (Allah) akawapa malipo ya duniani na thawabu nzuri za Akhera, na Allah anawapenda wafanyao mazuri



Sura: AL-IMRAN 

Aya : 149

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِن تُطِيعُواْ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يَرُدُّوكُمۡ عَلَىٰٓ أَعۡقَٰبِكُمۡ فَتَنقَلِبُواْ خَٰسِرِينَ

Enyi mlioamini, ikiwa mtawatii wale waliokufuru[1] watakurudisheni nyuma, na mtageuka kuwa wenye hasara


1- - Utii unaokatazwa hapa ni ule unaohusu masuala ya kuabudu na kupinga sheria za Allah na sio masuala ya maendeleo ya mazingira ya dunia.


Sura: AL-IMRAN 

Aya : 150

بَلِ ٱللَّهُ مَوۡلَىٰكُمۡۖ وَهُوَ خَيۡرُ ٱلنَّـٰصِرِينَ

Bali Allah ndiye Msimamizi wenu, na Yeye ni Msaidizi Bora zaidi kuliko wasaidizi wote)