Sura: AL-WAAQIA’H 

Aya : 91

فَسَلَٰمٞ لَّكَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ

Basi itaambiwa amani iwe juu yako uliye katika watu kuliani



Sura: AL-WAAQIA’H 

Aya : 92

وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُكَذِّبِينَ ٱلضَّآلِّينَ

Ama ikiwa mwenye roho hiyo ni miongoni mwa wakadhibisha waliyopotea



Sura: AL-WAAQIA’H 

Aya : 93

فَنُزُلٞ مِّنۡ حَمِيمٖ

Basi mapokezi na mafikio yake ni maji ya moto yachemkayo



Sura: AL-WAAQIA’H 

Aya : 94

وَتَصۡلِيَةُ جَحِيمٍ

Na kuingizwa kwenye Moto wa jahimu, (uwakao vikali mno)



Sura: AL-WAAQIA’H 

Aya : 95

إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ حَقُّ ٱلۡيَقِينِ

Hakika hii bila shaka ni haki yenye yakini.[1]


1- - Hakika haya yaliotajwa katika Sura hii tukufu bila shaka ni kiini cha yakini ilio thabiti, isiyo ingiliwa na shaka hata kidogo.


Sura: AL-WAAQIA’H 

Aya : 96

فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ

Basi litakase jina la Mola wako aliye Mtukufu