Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 91

وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ ءَامِنُواْ بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ قَالُواْ نُؤۡمِنُ بِمَآ أُنزِلَ عَلَيۡنَا وَيَكۡفُرُونَ بِمَا وَرَآءَهُۥ وَهُوَ ٱلۡحَقُّ مُصَدِّقٗا لِّمَا مَعَهُمۡۗ قُلۡ فَلِمَ تَقۡتُلُونَ أَنۢبِيَآءَ ٱللَّهِ مِن قَبۡلُ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Na wanapoambiwa: Yaaminini yale aliyoyateremsha Allah, husema: Tunaamini yale tulioteremshiwa na huyapinga yasiyokuwa hayo, nayo ndio haki yenye kuafiki waliyo nayo. Sema: Ni kwanini (mlikuwa) mnawaua Manabii wa Allah hapo zamani kama ninyi ni waumini?



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 92

۞وَلَقَدۡ جَآءَكُم مُّوسَىٰ بِٱلۡبَيِّنَٰتِ ثُمَّ ٱتَّخَذۡتُمُ ٱلۡعِجۡلَ مِنۢ بَعۡدِهِۦ وَأَنتُمۡ ظَٰلِمُونَ

Na kwa hakika kabisa, alikujieni Musa akiwa na miujiza ya wazi, kisha baada yake[1] mkamfanya Ndama (Mungu) na ilhali nyinyi ni wenye kudhulumu (nafsi zenu)


1- - Baada ya Musa kwenda kwenye kiaga cha kukutana na Mola wake


Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 93

وَإِذۡ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَكُمۡ وَرَفَعۡنَا فَوۡقَكُمُ ٱلطُّورَ خُذُواْ مَآ ءَاتَيۡنَٰكُم بِقُوَّةٖ وَٱسۡمَعُواْۖ قَالُواْ سَمِعۡنَا وَعَصَيۡنَا وَأُشۡرِبُواْ فِي قُلُوبِهِمُ ٱلۡعِجۡلَ بِكُفۡرِهِمۡۚ قُلۡ بِئۡسَمَا يَأۡمُرُكُم بِهِۦٓ إِيمَٰنُكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Na (kumbukeni) tulipochukua ahadi yenu na tukauinua (mlima) Turi juu yenu (tukakuambieni): Yashikeni kwa nguvu tuliyokupeni na sikilizeni. Wakasema: Tumesikia na tumeasi, na wakanyweshwa mioyoni mwao (kupenda) kuabudu ndama kwa sababu ya kufuru zao. Waambie: Ni jambo baya sana inavyokuamrisheni imani yenu, kama ninyi ni waumini



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 94

قُلۡ إِن كَانَتۡ لَكُمُ ٱلدَّارُ ٱلۡأٓخِرَةُ عِندَ ٱللَّهِ خَالِصَةٗ مِّن دُونِ ٱلنَّاسِ فَتَمَنَّوُاْ ٱلۡمَوۡتَ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Sema: Ikiwa makazi ya Akhera (yaliyopo) kwa Allah ni yenu tu kuliko watu wengine, basi tamanini kufa ikiwa nyinyi ni wakweli



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 95

وَلَن يَتَمَنَّوۡهُ أَبَدَۢا بِمَا قَدَّمَتۡ أَيۡدِيهِمۡۚ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِٱلظَّـٰلِمِينَ

Asilani, hawatalitamani hilo kwa sababu yale yaliyotangulizwa na mikono yao, na Allah anawajua sana wenye kudhulumu



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 96

وَلَتَجِدَنَّهُمۡ أَحۡرَصَ ٱلنَّاسِ عَلَىٰ حَيَوٰةٖ وَمِنَ ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْۚ يَوَدُّ أَحَدُهُمۡ لَوۡ يُعَمَّرُ أَلۡفَ سَنَةٖ وَمَا هُوَ بِمُزَحۡزِحِهِۦ مِنَ ٱلۡعَذَابِ أَن يُعَمَّرَۗ وَٱللَّهُ بَصِيرُۢ بِمَا يَعۡمَلُونَ

Na kwa hakika kabisa, utawakuta wao (Wayahudi) ndio wanaojali mno uhai[1] kuliko watu wote, na miongoni mwa washirikishaji (pia utakuta nao wako hivyo); anatamani mmoja wao angalau apewe umri wa miaka elfu moja. Na kupewa kwake umri mrefu hakutamuepushia adhabu, na Allah ni Mwenye kuyaona wanayoyatenda


1- - Katika maisha ya duniani


Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 97

قُلۡ مَن كَانَ عَدُوّٗا لِّـجِبۡرِيلَ فَإِنَّهُۥ نَزَّلَهُۥ عَلَىٰ قَلۡبِكَ بِإِذۡنِ ٱللَّهِ مُصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَهُدٗى وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُؤۡمِنِينَ

Sema: Mwenye kuwa adui wa Jibrili, basi (ajue kuwa) yeye ndiye aliyeuteremsha Wahyi (Qur’an) moyoni mwako kwa idhini ya Allah, unaosadikisha yale yaliyokuwa kabla yake na ni muongozo na bishara kwa waumini



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 98

مَن كَانَ عَدُوّٗا لِّلَّهِ وَمَلَـٰٓئِكَتِهِۦ وَرُسُلِهِۦ وَجِبۡرِيلَ وَمِيكَىٰلَ فَإِنَّ ٱللَّهَ عَدُوّٞ لِّلۡكَٰفِرِينَ

Mwenye kuwa adui wa Allah na Malaika wake na Mitume wake na Jibrilina Mikaili, basi hakika, Allah ni adui wa makafiri wote



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 99

وَلَقَدۡ أَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ ءَايَٰتِۭ بَيِّنَٰتٖۖ وَمَا يَكۡفُرُ بِهَآ إِلَّا ٱلۡفَٰسِقُونَ

Na kwa yakini kabisa, tume-kuteremshia hoja za wazi na hawazikanushi isipokuwa waovu tu



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 100

أَوَكُلَّمَا عَٰهَدُواْ عَهۡدٗا نَّبَذَهُۥ فَرِيقٞ مِّنۡهُمۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ

Hivi ni kwanini kila watoapo ahadi, kuna kundi miongoni mwao linaivunja ahadi hiyo! Lakini (ukweli ni kwamba) wengi wao hawaamini



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 101

وَلَمَّا جَآءَهُمۡ رَسُولٞ مِّنۡ عِندِ ٱللَّهِ مُصَدِّقٞ لِّمَا مَعَهُمۡ نَبَذَ فَرِيقٞ مِّنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ كِتَٰبَ ٱللَّهِ وَرَآءَ ظُهُورِهِمۡ كَأَنَّهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ

Na alipowafikia Mtume kutoka kwa Allah mwenye kusadikisha yale waliyo nayo, kundi miongoni mwa wale waliopewa Kitabu walikitupa Kitabu cha Allah nyuma ya migongo yao kama kwamba hawajui



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 102

وَٱتَّبَعُواْ مَا تَتۡلُواْ ٱلشَّيَٰطِينُ عَلَىٰ مُلۡكِ سُلَيۡمَٰنَۖ وَمَا كَفَرَ سُلَيۡمَٰنُ وَلَٰكِنَّ ٱلشَّيَٰطِينَ كَفَرُواْ يُعَلِّمُونَ ٱلنَّاسَ ٱلسِّحۡرَ وَمَآ أُنزِلَ عَلَى ٱلۡمَلَكَيۡنِ بِبَابِلَ هَٰرُوتَ وَمَٰرُوتَۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنۡ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَآ إِنَّمَا نَحۡنُ فِتۡنَةٞ فَلَا تَكۡفُرۡۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنۡهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِۦ بَيۡنَ ٱلۡمَرۡءِ وَزَوۡجِهِۦۚ وَمَا هُم بِضَآرِّينَ بِهِۦ مِنۡ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمۡ وَلَا يَنفَعُهُمۡۚ وَلَقَدۡ عَلِمُواْ لَمَنِ ٱشۡتَرَىٰهُ مَا لَهُۥ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ مِنۡ خَلَٰقٖۚ وَلَبِئۡسَ مَا شَرَوۡاْ بِهِۦٓ أَنفُسَهُمۡۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ

Na wamefuata yale yanayoso-mwa na Mashetani katika (wakati wa) ufalme wa Suleimani. Na Suleimani hakukufuru, lakini Mashetani ndio waliokufuru; (kwa sababu) wanawafundisha watu uchawi na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili Haruta na Maruta katika mji wa Babil. Na wala hawamfundishi yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru. Basi wakajifunza kwao yale yawezayo kumfarakanisha mtu na mkewe. Na wala wao hawana uwezo wa kumdhuru yeyote kwa hayo ila kwa idhini ya Allah tu. Na wanajifunza yale yanayowadhuru na wala hayawanufaishi. Na kwa yakini wamejua kwamba aliyechagua haya hatakuwa na fungu lolote Akhera. Na nikibaya mnokilewalichozichagulianafsizao laiti wangekuwa wanajua



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 103

وَلَوۡ أَنَّهُمۡ ءَامَنُواْ وَٱتَّقَوۡاْ لَمَثُوبَةٞ مِّنۡ عِندِ ٱللَّهِ خَيۡرٞۚ لَّوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ

Na lau wangeamini na kumcha Allah, bila ya shaka malipo yatokayo kwa Allah yangekuwa bora laiti wangelijua



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 104

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَقُولُواْ رَٰعِنَا وَقُولُواْ ٱنظُرۡنَا وَٱسۡمَعُواْۗ وَلِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Enyi mlioamini! Msiseme: “Raainaa” na semeni “Undhurnaa”. Na sikieni. Na makafiri watapata adhabu iumizayo



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 105

مَّا يَوَدُّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ وَلَا ٱلۡمُشۡرِكِينَ أَن يُنَزَّلَ عَلَيۡكُم مِّنۡ خَيۡرٖ مِّن رَّبِّكُمۡۚ وَٱللَّهُ يَخۡتَصُّ بِرَحۡمَتِهِۦ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ ذُو ٱلۡفَضۡلِ ٱلۡعَظِيمِ

Watu wa Kitabu waliokufuru na washirikishaji hawapendi mteremshiwe heri yoyote kutoka kwa Mola wenu. Na Allah humkusudia (kumpa) rehema zake amtakaye, na Allah ni Mwenye fadhila kubwa



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 106

۞مَا نَنسَخۡ مِنۡ ءَايَةٍ أَوۡ نُنسِهَا نَأۡتِ بِخَيۡرٖ مِّنۡهَآ أَوۡ مِثۡلِهَآۗ أَلَمۡ تَعۡلَمۡ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Hakuna Aya yoyote tunayoifuta au kuisahaulisha isipokuwa kwamba tunaleta iliyo bora zaidi kuliko ile au iliyo mfano wake. Je, hujui kwamba Allah ni Muweza wa kila jambo?



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 107

أَلَمۡ تَعۡلَمۡ أَنَّ ٱللَّهَ لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٍ

Je, hujui kwamba Allah ndiye Mwenye ufalme wa mbinguni na ardhini? Na nyinyi hamna mlinzi wala msaidizi mwingine badala ya Allah



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 108

أَمۡ تُرِيدُونَ أَن تَسۡـَٔلُواْ رَسُولَكُمۡ كَمَا سُئِلَ مُوسَىٰ مِن قَبۡلُۗ وَمَن يَتَبَدَّلِ ٱلۡكُفۡرَ بِٱلۡإِيمَٰنِ فَقَدۡ ضَلَّ سَوَآءَ ٱلسَّبِيلِ

Au mnataka kumuuliza Mtume wenu kama (Mtume) Musa alivyoulizwa hapo zamani? Na anayebadilisha imani kwa ukafiri, bila shaka ameipotea njia yasawa



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 109

وَدَّ كَثِيرٞ مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ لَوۡ يَرُدُّونَكُم مِّنۢ بَعۡدِ إِيمَٰنِكُمۡ كُفَّارًا حَسَدٗا مِّنۡ عِندِ أَنفُسِهِم مِّنۢ بَعۡدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ ٱلۡحَقُّۖ فَٱعۡفُواْ وَٱصۡفَحُواْ حَتَّىٰ يَأۡتِيَ ٱللَّهُ بِأَمۡرِهِۦٓۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Watu wa Kitabu wengi wanapenda laiti wakurudisheni muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa sababu ya husuda iliyomo nyoyoni mwao baada ya kuwa haki imewapambanukia. Basi sameheni na puuzeni mpaka Allah alete amri yake. Hakika, Allah ni Muweza sana wa kila jambo



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 110

وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَۚ وَمَا تُقَدِّمُواْ لِأَنفُسِكُم مِّنۡ خَيۡرٖ تَجِدُوهُ عِندَ ٱللَّهِۗ إِنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ

Na simamisheni Swala na toeni Zaka, na heri yoyote muitanguliziayo kwa ajili yenu mtaikuta mbele ya Allah. Hakika, Allah anayaona mno mnayoyatenda



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 111

وَقَالُواْ لَن يَدۡخُلَ ٱلۡجَنَّةَ إِلَّا مَن كَانَ هُودًا أَوۡ نَصَٰرَىٰۗ تِلۡكَ أَمَانِيُّهُمۡۗ قُلۡ هَاتُواْ بُرۡهَٰنَكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Na wamesema: Katu, hataingia Peponi isipokuwa tu Myahudi au Mnaswara! Hayo ndio matamanio yao. Sema: Leteni ushahidi wenu kama ninyi ni wa kweli



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 112

بَلَىٰۚ مَنۡ أَسۡلَمَ وَجۡهَهُۥ لِلَّهِ وَهُوَ مُحۡسِنٞ فَلَهُۥٓ أَجۡرُهُۥ عِندَ رَبِّهِۦ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Naam, wenye kujisalimisha kwa Allah na ilhali wanatenda yaliyo mazuri, basi watapata malipo yao kwa Mola wao, na hawatakuwa na hofu na hawatahuzunika



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 113

وَقَالَتِ ٱلۡيَهُودُ لَيۡسَتِ ٱلنَّصَٰرَىٰ عَلَىٰ شَيۡءٖ وَقَالَتِ ٱلنَّصَٰرَىٰ لَيۡسَتِ ٱلۡيَهُودُ عَلَىٰ شَيۡءٖ وَهُمۡ يَتۡلُونَ ٱلۡكِتَٰبَۗ كَذَٰلِكَ قَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَعۡلَمُونَ مِثۡلَ قَوۡلِهِمۡۚ فَٱللَّهُ يَحۡكُمُ بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فِيمَا كَانُواْ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ

Na Wayahudi wamesema: Manaswara hawa na kitu (chochote cha maana). Na Manaswara wame-sema: Wayahudi hawana kitu (chochote cha maana), na wao (wote) wanasoma Kitabu (kitakatifu kitokacho kwa Mola wao). Kama hivyo, wale ambao hawajui kitu wamesema mfano wa maneno yao. Basi Allah atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakitafautiana



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 114

وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَٰجِدَ ٱللَّهِ أَن يُذۡكَرَ فِيهَا ٱسۡمُهُۥ وَسَعَىٰ فِي خَرَابِهَآۚ أُوْلَـٰٓئِكَ مَا كَانَ لَهُمۡ أَن يَدۡخُلُوهَآ إِلَّا خَآئِفِينَۚ لَهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا خِزۡيٞ وَلَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٞ

Na ninani dhalimu zaidi kuliko yule azuiaye Misikitiya Allah kutajwa humo jina lake na kujitahidi kuiharibu? Hao haitawawia kuingia humo ila kwa kuogopa. Watapata fedheha katika dunia, na akhera watapata adhabu kubwa



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 115

وَلِلَّهِ ٱلۡمَشۡرِقُ وَٱلۡمَغۡرِبُۚ فَأَيۡنَمَا تُوَلُّواْ فَثَمَّ وَجۡهُ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ وَٰسِعٌ عَلِيمٞ

Mashariki na magharibi ni ya Allah. Hakika Allah ni Mwenye ukwasi, Mwenye kujua



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 116

وَقَالُواْ ٱتَّخَذَ ٱللَّهُ وَلَدٗاۗ سُبۡحَٰنَهُۥۖ بَل لَّهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ كُلّٞ لَّهُۥ قَٰنِتُونَ

Na (Makafiri wote) wamesema: Allah amefanya mtoto. Utakasifu ni wake. Bali ni miliki yake yeye tu vilivyomo mbinguni na ardhini. Vyote vina myenyekea yeye tu



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 117

بَدِيعُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ وَإِذَا قَضَىٰٓ أَمۡرٗا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ

Muanzilishi wa mbingu na ardhi. Na anapopitisha jambo liwe, basi huliambia tu “kuwa” na linakuwa



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 118

وَقَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَعۡلَمُونَ لَوۡلَا يُكَلِّمُنَا ٱللَّهُ أَوۡ تَأۡتِينَآ ءَايَةٞۗ كَذَٰلِكَ قَالَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِم مِّثۡلَ قَوۡلِهِمۡۘ تَشَٰبَهَتۡ قُلُوبُهُمۡۗ قَدۡ بَيَّنَّا ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يُوقِنُونَ

Na walisema wasiojua (kitu kwamba): Kwanini Allah asituambie wenyewe, au usitujie muujiza!? Kama hivyo walisema waliokuwa kabla yao mfano wa kauli yao hiyo. Zimefanana nyoyo zao. Hakika tumebainisha miujiza mbalimbali kwa watu wanaoamini



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 119

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ بَشِيرٗا وَنَذِيرٗاۖ وَلَا تُسۡـَٔلُ عَنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡجَحِيمِ

Hakika sisi tumekutuma kwa haki ukiwa mwenye kutoa habari njema na kutahadharisha. Na wala hutaulizwa kuhusu watu wa motoni



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 120

وَلَن تَرۡضَىٰ عَنكَ ٱلۡيَهُودُ وَلَا ٱلنَّصَٰرَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمۡۗ قُلۡ إِنَّ هُدَى ٱللَّهِ هُوَ ٱلۡهُدَىٰۗ وَلَئِنِ ٱتَّبَعۡتَ أَهۡوَآءَهُم بَعۡدَ ٱلَّذِي جَآءَكَ مِنَ ٱلۡعِلۡمِ مَا لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٍ

Na kamwe hawatakuridhia Wayahudi na Wanaswara hadi utakapoifuata dini yao. Sema: Muongozo wa Allah ndio muongozo. Na ikiwa utafuata matamanio yao baada ya elimu iliyo kujia, basi hutampata yeyote wa kukutetea wala wa kukunusuru zaidi ya Allah