Sura: HUUD 

Aya : 91

قَالُواْ يَٰشُعَيۡبُ مَا نَفۡقَهُ كَثِيرٗا مِّمَّا تَقُولُ وَإِنَّا لَنَرَىٰكَ فِينَا ضَعِيفٗاۖ وَلَوۡلَا رَهۡطُكَ لَرَجَمۡنَٰكَۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيۡنَا بِعَزِيزٖ

Wakasema: Ewe Shuaibu! Hatufahamu saana hayo uyasemayo. Na wewe kwetu tunakuona mtu dhaifu tu. Lau kama sio kuwepo jamaa zako, tunge (kuuwa kwa) kukupiga mawe, na wewe kwetu si mtu mwenye heshima yoyote



Sura: HUUD 

Aya : 92

قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَهۡطِيٓ أَعَزُّ عَلَيۡكُم مِّنَ ٱللَّهِ وَٱتَّخَذۡتُمُوهُ وَرَآءَكُمۡ ظِهۡرِيًّاۖ إِنَّ رَبِّي بِمَا تَعۡمَلُونَ مُحِيطٞ

Akasema: Enyi watu wangu! Hivi kundi langu ndio lina nguvu zaidi kwenu kuliko Allah? Na mmemuweka (Allah) nyuma ya migongo yenu! Hakika Mola wangu mlezi ni mwenye kuyazunguka yote mnayo yatenda



Sura: HUUD 

Aya : 93

وَيَٰقَوۡمِ ٱعۡمَلُواْ عَلَىٰ مَكَانَتِكُمۡ إِنِّي عَٰمِلٞۖ سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ مَن يَأۡتِيهِ عَذَابٞ يُخۡزِيهِ وَمَنۡ هُوَ كَٰذِبٞۖ وَٱرۡتَقِبُوٓاْ إِنِّي مَعَكُمۡ رَقِيبٞ

Na enyi watu wangu! Fanyeni muwezayo, na mimi pia ninafanya. Karibuni mtajua ni nani itakaye mfika adhabu ya kumfedhehesha, na nani aliye mwongo. Na ngojeni, mimi pia ninangoja pamoja nanyi



Sura: HUUD 

Aya : 94

وَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا نَجَّيۡنَا شُعَيۡبٗا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ بِرَحۡمَةٖ مِّنَّا وَأَخَذَتِ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ ٱلصَّيۡحَةُ فَأَصۡبَحُواْ فِي دِيَٰرِهِمۡ جَٰثِمِينَ

Na ilipo fika amri yetu, tulimuokoa Shuaibu na wale walioamini pamoja naye kwa rehema kutoka kwetu. Na uliwachukuwa wale waliyodhulumu ukelele, basi wakapambazukiwa wakiwa wamekufa kifudifudi! Majumbani mwao



Sura: HUUD 

Aya : 95

كَأَن لَّمۡ يَغۡنَوۡاْ فِيهَآۗ أَلَا بُعۡدٗا لِّمَدۡيَنَ كَمَا بَعِدَتۡ ثَمُودُ

Kana kwamba hawakuishi humo. Elewa mangamizi yawe kwa watu wa Madyana, kama walivyo angamia watu wa Thamud!



Sura: HUUD 

Aya : 96

وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا مُوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَا وَسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٍ

Na kwa hakika tulimtuma Mussa akiwa na ishara zetu na uthibitisho ulio wazi



Sura: HUUD 

Aya : 97

إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ فَٱتَّبَعُوٓاْ أَمۡرَ فِرۡعَوۡنَۖ وَمَآ أَمۡرُ فِرۡعَوۡنَ بِرَشِيدٖ

Kwenda kwa firauni na waheshimiwa wake. Lakini wao walifuata amri ya Firauni, na amri ya Firauni haikuwa na busara



Sura: HUUD 

Aya : 98

يَقۡدُمُ قَوۡمَهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فَأَوۡرَدَهُمُ ٱلنَّارَۖ وَبِئۡسَ ٱلۡوِرۡدُ ٱلۡمَوۡرُودُ

Siku ya Kiyama (Firauni) atawatangulia watu wake na atawaingiza Motoni (kama alivyokuwa akiwatangulia duniani). Na ubaya ulioje huo wataoingia!



Sura: HUUD 

Aya : 99

وَأُتۡبِعُواْ فِي هَٰذِهِۦ لَعۡنَةٗ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ بِئۡسَ ٱلرِّفۡدُ ٱلۡمَرۡفُودُ

Na wamefuatishiwa laana hapa duniani na Siku ya Kiyama. Ni mabaya yalioje watakayo pewa!



Sura: HUUD 

Aya : 100

ذَٰلِكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلۡقُرَىٰ نَقُصُّهُۥ عَلَيۡكَۖ مِنۡهَا قَآئِمٞ وَحَصِيدٞ

Hizi ni katika habari za miji, tunakusimulia. Mingine ipo bado na mingine haipo tena



Sura: HUUD 

Aya : 101

وَمَا ظَلَمۡنَٰهُمۡ وَلَٰكِن ظَلَمُوٓاْ أَنفُسَهُمۡۖ فَمَآ أَغۡنَتۡ عَنۡهُمۡ ءَالِهَتُهُمُ ٱلَّتِي يَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٖ لَّمَّا جَآءَ أَمۡرُ رَبِّكَۖ وَمَا زَادُوهُمۡ غَيۡرَ تَتۡبِيبٖ

Na sisi hatukuwadhulumu, lakini wao wenyewe wamezidhulumu nafsi zao. Na haikuwafaa chochote Miungu yao waliyokuwa wakiiomba badala ya Allah ilipokuja amri ya Mola wako mlezi. Na hiyo Miungu haikuwazidishia kitu isipokuwa maangamizi tu



Sura: HUUD 

Aya : 102

وَكَذَٰلِكَ أَخۡذُ رَبِّكَ إِذَآ أَخَذَ ٱلۡقُرَىٰ وَهِيَ ظَٰلِمَةٌۚ إِنَّ أَخۡذَهُۥٓ أَلِيمٞ شَدِيدٌ

Na hivyo ndivyo Mola wako mlezi anawachukulia hatua anapowachukulia hatua watu wa miji wanapodhulumu. Hakika (akikamata) mkamato wake ni mchungu na mkali mno



Sura: HUUD 

Aya : 103

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّمَنۡ خَافَ عَذَابَ ٱلۡأٓخِرَةِۚ ذَٰلِكَ يَوۡمٞ مَّجۡمُوعٞ لَّهُ ٱلنَّاسُ وَذَٰلِكَ يَوۡمٞ مَّشۡهُودٞ

Hakika katika hilo kuna ishara kwa kila anayeogopa adhabu ya Akhera. Hiyo ni Siku itakayokusanyiwa watukwake, na hiyo ni Siku itakayoshuhudiwa



Sura: HUUD 

Aya : 104

وَمَا نُؤَخِّرُهُۥٓ إِلَّا لِأَجَلٖ مَّعۡدُودٖ

Na sisi hatuicheleweshi ispokuwa kwa muda tu unao hesabiwa



Sura: HUUD 

Aya : 105

يَوۡمَ يَأۡتِ لَا تَكَلَّمُ نَفۡسٌ إِلَّا بِإِذۡنِهِۦۚ فَمِنۡهُمۡ شَقِيّٞ وَسَعِيدٞ

Siku hiyo itakapo fika, hatosema hata mtu mmoja (chochote) isipokuwa kwa idhini yake (Allah). Basi kati yao wapo waovu na walio wema



Sura: HUUD 

Aya : 106

فَأَمَّا ٱلَّذِينَ شَقُواْ فَفِي ٱلنَّارِ لَهُمۡ فِيهَا زَفِيرٞ وَشَهِيقٌ

Ama wale waovu basi hao Motoni ndio makazi yao humo watasikia sauti za Moto ukivuta pumzi ndani na kutoa nje



Sura: HUUD 

Aya : 107

خَٰلِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ ٱلسَّمَٰوَٰتُ وَٱلۡأَرۡضُ إِلَّا مَا شَآءَ رَبُّكَۚ إِنَّ رَبَّكَ فَعَّالٞ لِّمَا يُرِيدُ

Watadumu humo muda wa kuwepo mbingu na ardhi, isipokuwa vile apendavyo Mola wako mlezi. Hakika Mola wako mlezi anatenda apendavyo



Sura: HUUD 

Aya : 108

۞وَأَمَّا ٱلَّذِينَ سُعِدُواْ فَفِي ٱلۡجَنَّةِ خَٰلِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ ٱلسَّمَٰوَٰتُ وَٱلۡأَرۡضُ إِلَّا مَا شَآءَ رَبُّكَۖ عَطَآءً غَيۡرَ مَجۡذُوذٖ

Na ama wale walio bahatika (kupata maisha mazuri), wao watakuwa Peponi watadumu humo muda wa kuwepo mbingu na ardhi, isipokuwa apendavyo Mola wako mlezi. Hicho ni zawadi (kipawa) kisio na ukomo



Sura: HUUD 

Aya : 109

فَلَا تَكُ فِي مِرۡيَةٖ مِّمَّا يَعۡبُدُ هَـٰٓؤُلَآءِۚ مَا يَعۡبُدُونَ إِلَّا كَمَا يَعۡبُدُ ءَابَآؤُهُم مِّن قَبۡلُۚ وَإِنَّا لَمُوَفُّوهُمۡ نَصِيبَهُمۡ غَيۡرَ مَنقُوصٖ

Basi usiwe na shaka juu ya wanayo yaabudu hawa. Hawaabudu isipokuwa kama walivyo abudu baba zao zamani. Na hakika sisi tutawatimilizia fungu lao bila ya kupunguzwa



Sura: HUUD 

Aya : 110

وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ فَٱخۡتُلِفَ فِيهِۚ وَلَوۡلَا كَلِمَةٞ سَبَقَتۡ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيۡنَهُمۡۚ وَإِنَّهُمۡ لَفِي شَكّٖ مِّنۡهُ مُرِيبٖ

Na kwa yakini tulimpa Mussa kitabu (Taurati) wakatofautiana kuna walioiamini na wapo waliyoikataa). Na lau kama si kutangulia neno kutoka kwa Mola wako mlezi, (kwamba hatawaharakishia adhabu) bila ya shaka ingehukumiwa baina yao kwakuwaangamiza. Na hakika wao wamo katika shaka juu yake inayo wahangaisha



Sura: HUUD 

Aya : 111

وَإِنَّ كُلّٗا لَّمَّا لَيُوَفِّيَنَّهُمۡ رَبُّكَ أَعۡمَٰلَهُمۡۚ إِنَّهُۥ بِمَا يَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ

Na hakika kila kaumu (zilizotajwa) watalipwa malipo yao kamili. Hakika Yeye kwa yote myatendayo anayo habari



Sura: HUUD 

Aya : 112

فَٱسۡتَقِمۡ كَمَآ أُمِرۡتَ وَمَن تَابَ مَعَكَ وَلَا تَطۡغَوۡاْۚ إِنَّهُۥ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ

Basi, simama imara kama ulivyo amrishwa, na wale waliotubu pamoja na wewe, na msichupe mipaka. Hakika Yeye anayaona yote myatendayo



Sura: HUUD 

Aya : 113

وَلَا تَرۡكَنُوٓاْ إِلَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ فَتَمَسَّكُمُ ٱلنَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِنۡ أَوۡلِيَآءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ

Wala msiwategemee wale walio dhulumu, na ikasababisha ukakuguseni Moto. na nyinyi hamna walinzi (wengine) badala ya Allah, kisha hamtanusuriwa



Sura: HUUD 

Aya : 114

وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ طَرَفَيِ ٱلنَّهَارِ وَزُلَفٗا مِّنَ ٱلَّيۡلِۚ إِنَّ ٱلۡحَسَنَٰتِ يُذۡهِبۡنَ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ ذَٰلِكَ ذِكۡرَىٰ لِلذَّـٰكِرِينَ

Na simamisha swala katika ncha mbili za mchana na nyakati za usiku. Hakika mema huondoa maovu. Huo ni ukumbusho kwa wale wanaokumbuka



Sura: HUUD 

Aya : 115

وَٱصۡبِرۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Na subiri (kuwa mvumilivu), kwani Allah hapotezi ujira wa wafanyao wema



Sura: HUUD 

Aya : 116

فَلَوۡلَا كَانَ مِنَ ٱلۡقُرُونِ مِن قَبۡلِكُمۡ أُوْلُواْ بَقِيَّةٖ يَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡفَسَادِ فِي ٱلۡأَرۡضِ إِلَّا قَلِيلٗا مِّمَّنۡ أَنجَيۡنَا مِنۡهُمۡۗ وَٱتَّبَعَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مَآ أُتۡرِفُواْ فِيهِ وَكَانُواْ مُجۡرِمِينَ

Na lau ingekuwepo katika karine za kabla yenu masalia ya watu wa kheri wanakataza maovu ardhini, (lakini hawakuwepo miongoni mwa watu wa kheri) isipokuwa wachache tu. Miongoni mwa (walioamini) tuliowaokoa kutoka kwenye adhabu. Na wale waliodhulumu wakafuata starehe zao walizoneemeshwa, na wakawa waovu



Sura: HUUD 

Aya : 117

وَمَا كَانَ رَبُّكَ لِيُهۡلِكَ ٱلۡقُرَىٰ بِظُلۡمٖ وَأَهۡلُهَا مُصۡلِحُونَ

Na hakuwa Mola wako mlezi ni mwenye kuangamiza watu wa miji kwa dhulma tu na hali watu wake ni watenda mema



Sura: HUUD 

Aya : 118

وَلَوۡ شَآءَ رَبُّكَ لَجَعَلَ ٱلنَّاسَ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗۖ وَلَا يَزَالُونَ مُخۡتَلِفِينَ

Na lau angetaka Mola wako mlezi ange wafanya watu wote kuwa umma mmoja. Na hawaachi kukhitalifiana,



Sura: HUUD 

Aya : 119

إِلَّا مَن رَّحِمَ رَبُّكَۚ وَلِذَٰلِكَ خَلَقَهُمۡۗ وَتَمَّتۡ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمۡلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ أَجۡمَعِينَ

Isipokuwa tu wale Mola wako mlezi amewarehemu (wakaamini); na Allah amewaumba hivyo. Na neno la Mola wako mlezi litatimia: Kwe hakika nitaijaza Jahannam miongoni mwa majini na watu wote kwa pamoja



Sura: HUUD 

Aya : 120

وَكُلّٗا نَّقُصُّ عَلَيۡكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلرُّسُلِ مَا نُثَبِّتُ بِهِۦ فُؤَادَكَۚ وَجَآءَكَ فِي هَٰذِهِ ٱلۡحَقُّ وَمَوۡعِظَةٞ وَذِكۡرَىٰ لِلۡمُؤۡمِنِينَ

Na yote haya tunakusimulia miongoni mwa habari za Mitume yale yanayoupa nguvu moyo wako. Na katika haya imekujia haki na mawaidha na ukumbusho kwa waumini