Sura: AN-FAL 

Aya : 61

۞وَإِن جَنَحُواْ لِلسَّلۡمِ فَٱجۡنَحۡ لَهَا وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Na (makafiri) wakielekea kutaka amani (na suluhu), basi na wewe elekea kwenye amani (na suluhu) hiyo na mtegemee Allah. Hakika, yeye (Allah) ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua



Sura: AN-FAL 

Aya : 62

وَإِن يُرِيدُوٓاْ أَن يَخۡدَعُوكَ فَإِنَّ حَسۡبَكَ ٱللَّهُۚ هُوَ ٱلَّذِيٓ أَيَّدَكَ بِنَصۡرِهِۦ وَبِٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na (makafiri) wakitaka kukuhadaa (kwenye suluhu na amani) basi Allah anakutosha (dhidi ya hila na khiyana zao). Yeye (Allah) ndiye aliyekupa nguvu kwa nusra yake na kwa waumini



Sura: AN-FAL 

Aya : 63

وَأَلَّفَ بَيۡنَ قُلُوبِهِمۡۚ لَوۡ أَنفَقۡتَ مَا فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا مَّآ أَلَّفۡتَ بَيۡنَ قُلُوبِهِمۡ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ أَلَّفَ بَيۡنَهُمۡۚ إِنَّهُۥ عَزِيزٌ حَكِيمٞ

Na ameziunganisha nyoyo zao[1]. Lau kama ungetoa vyote vilivyomo duniani usingeweza kuziunganisha nyoyo zao, lakini Allah ndiye aliyewaunganisha[2]. Hakika, Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima


1- - Hapa inakumbushwa jamii yote ya Waarabu wa mji wa Madina na hasa wale wa kabila la Ausi na Khazraji ambao hawakuwa na masikilizano wala maelewano kwa kipindi kirefu. Uislamu ulipokuja uliwaunganisha wakawa ndugu na kusahau tofauti zao. Na huu ni ukumbusho pia kwa Waislamu wote juu ya neema ya Uislamu uliowaunganisha na kuwafanya ndugu.


2- - Hapa Aya inatoa angalizo kwamba, umoja, mshikamano, maelewano na maridhiano ya kweli sio jambo la ujanja ujanja au hila. Ni jambo linalofanywa na Allah mwenyewe pale nia na dhamira zinapokuwa safi kwa ajili yake na kwa ajili ya dini yake na sio vinginevyo.


Sura: AN-FAL 

Aya : 64

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ حَسۡبُكَ ٱللَّهُ وَمَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Ewe Nabii, Allah anakutosha wewe na waumini waliokufuata (katika kukukinga na kukupa nusra dhidi ya shari za makafiri, njama na fitina zao)



Sura: AN-FAL 

Aya : 65

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ حَرِّضِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ عَلَى ٱلۡقِتَالِۚ إِن يَكُن مِّنكُمۡ عِشۡرُونَ صَٰبِرُونَ يَغۡلِبُواْ مِاْئَتَيۡنِۚ وَإِن يَكُن مِّنكُم مِّاْئَةٞ يَغۡلِبُوٓاْ أَلۡفٗا مِّنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِأَنَّهُمۡ قَوۡمٞ لَّا يَفۡقَهُونَ

Ewe Nabii, wahimize Waumini kupigana (dhidi ya makafiri na maadui wa Uislamu). Kati yenu wakiwepo (wapiganaji) ishirini wenye uvumilivu watawashinda (makafiri) mia mbili. Na kati yenu wakiwepo (wapiganaji) mia (moja) watawashinda makafiri elfu moja, kwasababu wao (makafiri) ni watu wasiofahamu (mantiki ya vita na wanapigana bila ya weledi)



Sura: AN-FAL 

Aya : 66

ٱلۡـَٰٔنَ خَفَّفَ ٱللَّهُ عَنكُمۡ وَعَلِمَ أَنَّ فِيكُمۡ ضَعۡفٗاۚ فَإِن يَكُن مِّنكُم مِّاْئَةٞ صَابِرَةٞ يَغۡلِبُواْ مِاْئَتَيۡنِۚ وَإِن يَكُن مِّنكُمۡ أَلۡفٞ يَغۡلِبُوٓاْ أَلۡفَيۡنِ بِإِذۡنِ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ مَعَ ٱلصَّـٰبِرِينَ

Sasa Allah amekupunguzieni (idadi) na amejua kwamba mna udhaifu. Basi kati yenu wakiwepo (wapiganaji) mia moja wenye uvumilivu watawashinda (makafiri) mia mbili. Na kati yenu wakiwepo (wapiganaji) elfu moja watawashinda (makafiri) elfu mbili kwa idhini ya Allah. Na Allah yupo pamoja na wenye subira



Sura: AN-FAL 

Aya : 67

مَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَكُونَ لَهُۥٓ أَسۡرَىٰ حَتَّىٰ يُثۡخِنَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ تُرِيدُونَ عَرَضَ ٱلدُّنۡيَا وَٱللَّهُ يُرِيدُ ٱلۡأٓخِرَةَۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٞ

Haiwi kwa Nabii yeyote kuwa na mateka (katika kipindi cha vita halafu akakubali kupokea fidia) mpaka awe ameshinda (na kushika mamlaka) katika nchi (na amani ikawa imetawala). Mnataka vitu vya dunia vya kupita (ngawira, fidia na vikombozi), na Allah anataka Akhera. Na Allah ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima



Sura: AN-FAL 

Aya : 68

لَّوۡلَا كِتَٰبٞ مِّنَ ٱللَّهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمۡ فِيمَآ أَخَذۡتُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٞ

Lau kama sio kuwepo kwa maandiko kutoka kwa Allah yaliyokwishatangulia (kwamba aliyekosea kwenye jitihada ya rai ya kuchukua fidia hatoadhibiwa) ingekushikeni hasa (ingekupateni adhabu kubwa mno kwasababu ya vile mlivyochukua (fidia ya mateka)



Sura: AN-FAL 

Aya : 69

فَكُلُواْ مِمَّا غَنِمۡتُمۡ حَلَٰلٗا طَيِّبٗاۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Basi kuleni katika ngawira mlizoteka zikiwa halali na nzuri na mcheni Allah. Hakika, Allah ni Mwenye kusamehe, Mwingi wa rehema



Sura: AN-FAL 

Aya : 70

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ قُل لِّمَن فِيٓ أَيۡدِيكُم مِّنَ ٱلۡأَسۡرَىٰٓ إِن يَعۡلَمِ ٱللَّهُ فِي قُلُوبِكُمۡ خَيۡرٗا يُؤۡتِكُمۡ خَيۡرٗا مِّمَّآ أُخِذَ مِنكُمۡ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Ewe Nabii, waambie mateka waliomo mikononi mwenu (kwamba): Kama Allah akijua (akibaini) heri yoyote nyoyoni mwenu (utayari wa kuamini) atakupeni vilivyo bora zaidi kuliko vilivyochukuliwa kwenu, na atakusameheni. Na Allah ni Mwenye kusamehe, Mwingi wa rehema



Sura: AN-FAL 

Aya : 71

وَإِن يُرِيدُواْ خِيَانَتَكَ فَقَدۡ خَانُواْ ٱللَّهَ مِن قَبۡلُ فَأَمۡكَنَ مِنۡهُمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Na ikiwa (hao mateka) wanataka kukufanyia khiyana (baada ya kuwaachia), basi walikwishamfanyia khiyana Allah kabla (ya vita vya Badri), na Yeye (Allah) akawadhibiti (akawezesha kuwashinda). Na Allah ni Mwenye kujua, Mwenye hekima



Sura: AN-FAL 

Aya : 72

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَهَاجَرُواْ وَجَٰهَدُواْ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلَّذِينَ ءَاوَواْ وَّنَصَرُوٓاْ أُوْلَـٰٓئِكَ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلِيَآءُ بَعۡضٖۚ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَلَمۡ يُهَاجِرُواْ مَا لَكُم مِّن وَلَٰيَتِهِم مِّن شَيۡءٍ حَتَّىٰ يُهَاجِرُواْۚ وَإِنِ ٱسۡتَنصَرُوكُمۡ فِي ٱلدِّينِ فَعَلَيۡكُمُ ٱلنَّصۡرُ إِلَّا عَلَىٰ قَوۡمِۭ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَهُم مِّيثَٰقٞۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ

Hakika, wale walioamini na wakahama (katika miji yao kwa ajili ya Uislamu) na wakapigana Jihadi kwa mali zao na nafsi zao, na wale waliotoa hifadhi (mahala pa kuishi kwa wakimbizi wa Kiislamu) na wakanusuru (wakatoa misaada mbali mbali), hao ni walinzi wa wao kwa wao. Na wale walioamini lakini hawakuhama (kwenye miji ya kikafiri), nyinyi hamna wajibu wa ulinzi kwao hata kidogo mpaka wahame. Na wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni jukumu lenu kuwasaidia, isipokuwa kwa watu ambao yapo mapatano baina yenu na wao. Na Allah anayaona sana mnayoyatenda



Sura: AN-FAL 

Aya : 73

وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلِيَآءُ بَعۡضٍۚ إِلَّا تَفۡعَلُوهُ تَكُن فِتۡنَةٞ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَفَسَادٞ كَبِيرٞ

Na wale waliokufuru baadhi yao ni watetezi wa wengine (hawawezi kumuhami Mwislamu). Msipofanya hayo (niliyokuamrisheni) itatokea fitina katika ardhi (katika nchi) na uovu mkubwa sana



Sura: AN-FAL 

Aya : 74

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَهَاجَرُواْ وَجَٰهَدُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلَّذِينَ ءَاوَواْ وَّنَصَرُوٓاْ أُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ حَقّٗاۚ لَّهُم مَّغۡفِرَةٞ وَرِزۡقٞ كَرِيمٞ

Na walioamini na wakahama (kwa ajili ya usalama wa imani zao) na wakapigana Jihadi katika njia ya Allah, na waliotoa mahali pa kuishi (hifadhi) na wakatoa misaada (mbali mbali), hao ndio Waumini wa kweli. Watapata msamaha na riziki nzuri



Sura: AN-FAL 

Aya : 75

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنۢ بَعۡدُ وَهَاجَرُواْ وَجَٰهَدُواْ مَعَكُمۡ فَأُوْلَـٰٓئِكَ مِنكُمۡۚ وَأُوْلُواْ ٱلۡأَرۡحَامِ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلَىٰ بِبَعۡضٖ فِي كِتَٰبِ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمُۢ

Na walioamini baada ya hapo (baada ya suluhu ya Hudaibiya) na wakahama na wakapigana Jihadi pamoja nanyi, basi hao ni katika nyinyi (kiulinzi na nusra). Na ndugu wa nasaba wanastahikiana zaidi wenyewe kwa wenyewe (katika kurithiana) katika kitabu cha Allah (kuliko kurithiana kwasababu ya Hijira). Hakika, Allah ni Mwenye kukijua kila kitu