Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 61

لِمِثۡلِ هَٰذَا فَلۡيَعۡمَلِ ٱلۡعَٰمِلُونَ

Kwa mfano wa haya nawatende watendao



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 62

أَذَٰلِكَ خَيۡرٞ نُّزُلًا أَمۡ شَجَرَةُ ٱلزَّقُّومِ

Je! Kukaribishwa hivi si ndio bora, au mti wa Zaqqum?



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 63

إِنَّا جَعَلۡنَٰهَا فِتۡنَةٗ لِّلظَّـٰلِمِينَ

Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa walio dhulumu



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 64

إِنَّهَا شَجَرَةٞ تَخۡرُجُ فِيٓ أَصۡلِ ٱلۡجَحِيمِ

Hakika huo ni mti unao toka katikati ya Jahannamu



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 65

طَلۡعُهَا كَأَنَّهُۥ رُءُوسُ ٱلشَّيَٰطِينِ

Mashada ya matunda yake kana kwamba (ni) vichwa vya mashetani



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 66

فَإِنَّهُمۡ لَأٓكِلُونَ مِنۡهَا فَمَالِـُٔونَ مِنۡهَا ٱلۡبُطُونَ

Basi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 67

ثُمَّ إِنَّ لَهُمۡ عَلَيۡهَا لَشَوۡبٗا مِّنۡ حَمِيمٖ

Kisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji ya moto yaliyo chemka



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 68

ثُمَّ إِنَّ مَرۡجِعَهُمۡ لَإِلَى ٱلۡجَحِيمِ

Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 69

إِنَّهُمۡ أَلۡفَوۡاْ ءَابَآءَهُمۡ ضَآلِّينَ

Hakika waliwakuta baba zao wamepotea



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 70

فَهُمۡ عَلَىٰٓ ءَاثَٰرِهِمۡ يُهۡرَعُونَ

Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 71

وَلَقَدۡ ضَلَّ قَبۡلَهُمۡ أَكۡثَرُ ٱلۡأَوَّلِينَ

Na bila shaka walikwishapotea kabla yao watu wengi wa zamani



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 72

وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا فِيهِم مُّنذِرِينَ

Na Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 73

فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُنذَرِينَ

Basi hebu angalia ulikuwaje mwisho wa walio onywa?



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 74

إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ

Isipokuwa waja wa Allah walio chaguliwa



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 75

وَلَقَدۡ نَادَىٰنَا نُوحٞ فَلَنِعۡمَ ٱلۡمُجِيبُونَ

Na hakika Nuhu alituita, na Sisi ni bora wa waitikiaji



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 76

وَنَجَّيۡنَٰهُ وَأَهۡلَهُۥ مِنَ ٱلۡكَرۡبِ ٱلۡعَظِيمِ

Na tulimwokoa yeye na watu wake kutokana na msiba mkubwa



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 77

وَجَعَلۡنَا ذُرِّيَّتَهُۥ هُمُ ٱلۡبَاقِينَ

Na tuliwajaalia dhuriya zake (watoto wake) ndio wenye kubakia



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 78

وَتَرَكۡنَا عَلَيۡهِ فِي ٱلۡأٓخِرِينَ

Na tukamwachia (sifa njema) kwa walio kuja baadaye



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 79

سَلَٰمٌ عَلَىٰ نُوحٖ فِي ٱلۡعَٰلَمِينَ

Iwe salama kwa Nuhu ulimwenguni kote!



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 80

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Kwa hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 81

إِنَّهُۥ مِنۡ عِبَادِنَا ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 82

ثُمَّ أَغۡرَقۡنَا ٱلۡأٓخَرِينَ

Kisha tukawazamisha wale wengine



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 83

۞وَإِنَّ مِن شِيعَتِهِۦ لَإِبۡرَٰهِيمَ

Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake,



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 84

إِذۡ جَآءَ رَبَّهُۥ بِقَلۡبٖ سَلِيمٍ

Alipo mjia Mola wake Mlezi kwa moyo ulio salama



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 85

إِذۡ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوۡمِهِۦ مَاذَا تَعۡبُدُونَ

Alimwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini?



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 86

أَئِفۡكًا ءَالِهَةٗ دُونَ ٱللَّهِ تُرِيدُونَ

Kwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Allah?



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 87

فَمَا ظَنُّكُم بِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Mnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote?



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 88

فَنَظَرَ نَظۡرَةٗ فِي ٱلنُّجُومِ

Kisha akapiga jicho kutazama nyota



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 89

فَقَالَ إِنِّي سَقِيمٞ

Akasema: Hakika mimi ni mgonjwa!



Sura: ASSWAAFFAAT 

Aya : 90

فَتَوَلَّوۡاْ عَنۡهُ مُدۡبِرِينَ

Nao wakamwacha, wakampa kisogo