فَلَمَّا تَرَـٰٓءَا ٱلۡجَمۡعَانِ قَالَ أَصۡحَٰبُ مُوسَىٰٓ إِنَّا لَمُدۡرَكُونَ
Na yalipoonana majeshi mawili haya, watu wa Mussa wakasema: Hakika sisi bila ya shaka tumepatikana!
Kushiriki :
قَالَ كَلَّآۖ إِنَّ مَعِيَ رَبِّي سَيَهۡدِينِ
(Mussa) akasema: Hasha! Hakika yu pamoja nami Mola wangu Mlezi. Yeye ataniongoa!
فَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنِ ٱضۡرِب بِّعَصَاكَ ٱلۡبَحۡرَۖ فَٱنفَلَقَ فَكَانَ كُلُّ فِرۡقٖ كَٱلطَّوۡدِ ٱلۡعَظِيمِ
Tulimletea wahyi Mussa tuka-mwambia: Piga bahari kwa fimbo yako. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mlima mkubwa
وَأَزۡلَفۡنَا ثَمَّ ٱلۡأٓخَرِينَ
Na tukawajongeza hapo wale wengine
وَأَنجَيۡنَا مُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُۥٓ أَجۡمَعِينَ
Tukawaokoa Musa na walio kuwa pamoja naye wote
ثُمَّ أَغۡرَقۡنَا ٱلۡأٓخَرِينَ
Kisha tukawazamisha hao wengine
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ
Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara; lakini wengi wao si katika wenye kuamini
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Na kwa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu
وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ إِبۡرَٰهِيمَ
Na wasomee khabari za Ibrahim
إِذۡ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوۡمِهِۦ مَا تَعۡبُدُونَ
Alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Mnaabudu nini?
قَالُواْ نَعۡبُدُ أَصۡنَامٗا فَنَظَلُّ لَهَا عَٰكِفِينَ
Wakasema: Tunaabudu masa-namu, daima tunayanyenyekea
قَالَ هَلۡ يَسۡمَعُونَكُمۡ إِذۡ تَدۡعُونَ
Akasema: Je! Yanakusikieni mnapo yaita?
أَوۡ يَنفَعُونَكُمۡ أَوۡ يَضُرُّونَ
Au yanakufaeni, au yanaku-dhuruni?
قَالُواْ بَلۡ وَجَدۡنَآ ءَابَآءَنَا كَذَٰلِكَ يَفۡعَلُونَ
Wakasema: Bali tumewakuta baba zetu wakifanya hivyo hivyo
قَالَ أَفَرَءَيۡتُم مَّا كُنتُمۡ تَعۡبُدُونَ
Je! Mmewaona hawa mnao waabudu-
أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُمُ ٱلۡأَقۡدَمُونَ
Nyinyi na baba zenu wa zamani?
فَإِنَّهُمۡ عَدُوّٞ لِّيٓ إِلَّا رَبَّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Kwani hakika hao ni adui zangu, isipokuwa Mola Mlezi wa walimwengu wote
ٱلَّذِي خَلَقَنِي فَهُوَ يَهۡدِينِ
Ambaye ndiye aliyeniumba, na Yeye ndiye ananiongoa
وَٱلَّذِي هُوَ يُطۡعِمُنِي وَيَسۡقِينِ
Na ambaye ndiye ananilisha na kuninywesha
وَإِذَا مَرِضۡتُ فَهُوَ يَشۡفِينِ
Na ninapo ugua ni Yeye ndiye anaye niponesha
وَٱلَّذِي يُمِيتُنِي ثُمَّ يُحۡيِينِ
Na ambaye atanifisha, na kisha atanihuisha
وَٱلَّذِيٓ أَطۡمَعُ أَن يَغۡفِرَ لِي خَطِيٓـَٔتِي يَوۡمَ ٱلدِّينِ
Na ambaye ndiye ninaye mtumai kunisamehe makosa yangu Siku ya Malipo
رَبِّ هَبۡ لِي حُكۡمٗا وَأَلۡحِقۡنِي بِٱلصَّـٰلِحِينَ
Mola wangu Mlezi! Nitunukie hukumu na uniunganishe na watendao mema
وَٱجۡعَل لِّي لِسَانَ صِدۡقٖ فِي ٱلۡأٓخِرِينَ
Na unijaalie nitajwe kwa wema na watu watakao kuja baadaye
وَٱجۡعَلۡنِي مِن وَرَثَةِ جَنَّةِ ٱلنَّعِيمِ
Na unijaalie katika warithi wa Bustani za neema
وَٱغۡفِرۡ لِأَبِيٓ إِنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلضَّآلِّينَ
Na umsamehe baba yangu, kwani hakika alikuwa miongoni mwa wapotovu
وَلَا تُخۡزِنِي يَوۡمَ يُبۡعَثُونَ
Wala usinihizi (usinifedheheshe) Siku watapo fufuliwa
يَوۡمَ لَا يَنفَعُ مَالٞ وَلَا بَنُونَ
Siku ambayo kwamba mali hayatofaa kitu wala watoto
إِلَّا مَنۡ أَتَى ٱللَّهَ بِقَلۡبٖ سَلِيمٖ
Isipokuwa mwenye kumjia Allah na moyo safi
وَأُزۡلِفَتِ ٱلۡجَنَّةُ لِلۡمُتَّقِينَ
Na Pepo itasogezwa kwa wacha-mungu