فَلَمَّا جَآءَ ءَالَ لُوطٍ ٱلۡمُرۡسَلُونَ
Basi wale wajumbe (waliotumwa) walipofika kwa Lutwi
قَالَ إِنَّكُمۡ قَوۡمٞ مُّنكَرُونَ
(Lutwi) Alisema: Hakika nyinyi ni watu msiojulikana (hapa kwetu)
قَالُواْ بَلۡ جِئۡنَٰكَ بِمَا كَانُواْ فِيهِ يَمۡتَرُونَ
(Malaika) Walisema: Bali sisi tumekuletea (adhabu ya) yale waliyokuwa wakiyatilia shaka
وَأَتَيۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ وَإِنَّا لَصَٰدِقُونَ
Na tumefika kwako kwa Haki, na hakika sisi tunasema kweli
فَأَسۡرِ بِأَهۡلِكَ بِقِطۡعٖ مِّنَ ٱلَّيۡلِ وَٱتَّبِعۡ أَدۡبَٰرَهُمۡ وَلَا يَلۡتَفِتۡ مِنكُمۡ أَحَدٞ وَٱمۡضُواْ حَيۡثُ تُؤۡمَرُونَ
Basi ondoka na ahli zako kwenye sehemu ya usiku, nawe ufuate nyuma yao (huku ukiwahimiza ili waharakishe kuondoka), wala yeyote kati yenu asigeuke nyuma. Na mwende mlikoamrishwa
وَقَضَيۡنَآ إِلَيۡهِ ذَٰلِكَ ٱلۡأَمۡرَ أَنَّ دَابِرَ هَـٰٓؤُلَآءِ مَقۡطُوعٞ مُّصۡبِحِينَ
Na tukamfunulia Lutwi wahyi huo kwamba, mwisho wa watu hawa ikifika (mapambazuko ya) asubuhi watakuwa wameshakatiliwa mbali
وَجَآءَ أَهۡلُ ٱلۡمَدِينَةِ يَسۡتَبۡشِرُونَ
Na walikuja watu wa mji ule (baada ya kusikia kwa Lutu kuna wageni wazuri) huku wakifurahi
قَالَ إِنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ ضَيۡفِي فَلَا تَفۡضَحُونِ
(Lutwi) Alisema (kuwaambia): Hakika hawa wageni wangu (wanahitaji kuenziwa), tafadhalini msinifedheheshe
وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلَا تُخۡزُونِ
Na mcheni Allah, wala msinidhalilishe (mbele ya wageni)
قَالُوٓاْ أَوَلَمۡ نَنۡهَكَ عَنِ ٱلۡعَٰلَمِينَ
(Watu wa Lutwi) Walisema: Sisi situlikukataza usitie (neno tunapomtaka) yeyote katika walimwengu?
قَالَ هَـٰٓؤُلَآءِ بَنَاتِيٓ إِن كُنتُمۡ فَٰعِلِينَ
(Lutwi) Alisema (kuwaambia msinivunjie heshima): Hawa (hapa) binti zangu (waoeni), ikiwa nyinyi ni wafanyaji (mnaotaka kukata hamu zenu)
لَعَمۡرُكَ إِنَّهُمۡ لَفِي سَكۡرَتِهِمۡ يَعۡمَهُونَ
(Allah alisema) Naapia kwa umri wako! Hakika hao (watu wa Lutwi) wamepagawa katika ulevi wao, wanahangaika
فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّيۡحَةُ مُشۡرِقِينَ
Basi (ghafla) Ukelele mkali uliwachukua kipindi cha mapam-bazuko
فَجَعَلۡنَا عَٰلِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهِمۡ حِجَارَةٗ مِّن سِجِّيلٍ
Na tukaigeuza nchi (yao) juu chini chini juu, na tukawanyeshea (mvua ya) mawe ya udongo wa Motoni
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّلۡمُتَوَسِّمِينَ
Hakika katika hiyo (adhabu iliyowapata watu wa Lutwi) zipo ishara kwa wanaozingatia
وَإِنَّهَا لَبِسَبِيلٖ مُّقِيمٍ
Na (kitongoji cha watu wa Lutwi) kipo kwenye barabara ipitwayo (na watu wanaokwenda Sham)
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ
Hakika katika hiyo (adhabu) ipo ishara (na mazingatio) kwa Waumini
وَإِن كَانَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأَيۡكَةِ لَظَٰلِمِينَ
Japokuwa watu wa mji uliozingirwa na msitu (nao) walikuwa madhalimu[1]
1- - Hawa ni watu wa Nabii Shuaib, nao pia walikuwa wanamkufuru Allah.
فَٱنتَقَمۡنَا مِنۡهُمۡ وَإِنَّهُمَا لَبِإِمَامٖ مُّبِينٖ
Kwa hivyo tuliwaadhibu. Na miji miwili hiyo ipo kwenye barabara iliyo wazi
وَلَقَدۡ كَذَّبَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡحِجۡرِ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Na bila ya shaka wakazi wa Hijr[1] waliwapinga Mitume
1- - Hijri ni bonde linalopatikana kati ya mji wa Madina na ardhi ya Shamu
وَءَاتَيۡنَٰهُمۡ ءَايَٰتِنَا فَكَانُواْ عَنۡهَا مُعۡرِضِينَ
Na tuliwapa (watu wa Thamud) ishara zetu, nao walizipuuza
وَكَانُواْ يَنۡحِتُونَ مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتًا ءَامِنِينَ
Nao walikuwa wakichonga katika milima (na kuyafanya majumba) kwa amani
فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّيۡحَةُ مُصۡبِحِينَ
Basi ukelele ukawatwaa asubuhi
فَمَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ
Basi hayakuwafaa waliyokuwa wanayachuma
وَمَا خَلَقۡنَا ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَآ إِلَّا بِٱلۡحَقِّۗ وَإِنَّ ٱلسَّاعَةَ لَأٓتِيَةٞۖ فَٱصۡفَحِ ٱلصَّفۡحَ ٱلۡجَمِيلَ
Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ila kwa ajili ya Haki. Na hakika Kiyama kitafika tu (wala hilo halina shaka). Basi (Ewe Mtume) samehe (watu wako) msamaha mzuri
إِنَّ رَبَّكَ هُوَ ٱلۡخَلَّـٰقُ ٱلۡعَلِيمُ
Hakika Mola wako Mlezi ndiye Muumbaji (wa kila kitu tena) Mjuzi sana
وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَٰكَ سَبۡعٗا مِّنَ ٱلۡمَثَانِي وَٱلۡقُرۡءَانَ ٱلۡعَظِيمَ
Na tumekupa Aya saba (za Sura Al-fatiha) zisomwazo mara kwa mara, na Qur’ani Tukufu
لَا تَمُدَّنَّ عَيۡنَيۡكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعۡنَا بِهِۦٓ أَزۡوَٰجٗا مِّنۡهُمۡ وَلَا تَحۡزَنۡ عَلَيۡهِمۡ وَٱخۡفِضۡ جَنَاحَكَ لِلۡمُؤۡمِنِينَ
Usivikodolee macho yako vitu tulivyo waneemesha makundi fulani kati yao (hao makafiri), wala usiwahuzunikie (wasipoamaini). Na wainamishie bawa lako (la huruma) Waumini
وَقُلۡ إِنِّيٓ أَنَا ٱلنَّذِيرُ ٱلۡمُبِينُ
Na sema: Hakika mimi ni muonyaji mwenye kubainisha
كَمَآ أَنزَلۡنَا عَلَى ٱلۡمُقۡتَسِمِينَ
(Tumekuteremshia hii Qur’an) Kama tulivyowateremshia (Kitabu Mayahudi na Manaswara) walikigawanya (kwa kuamini baadhi na kukataa baadhi)