Sura: ANNABAI 

Aya : 31

إِنَّ لِلۡمُتَّقِينَ مَفَازًا

Hakika wacha Mungu wanastahiki kufuzu



Sura: ANNABAI 

Aya : 32

حَدَآئِقَ وَأَعۡنَٰبٗا

[watapata] Mabustani na mizabibu



Sura: ANNABAI 

Aya : 33

وَكَوَاعِبَ أَتۡرَابٗا

Na wake wenye vifua vya kujaa, na walio lingana nao



Sura: ANNABAI 

Aya : 34

وَكَأۡسٗا دِهَاقٗا

Na bilauri zilizo jaa,



Sura: ANNABAI 

Aya : 35

لَّا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوٗا وَلَا كِذَّـٰبٗا

Hawatasikia humo upuuzi wala uongo



Sura: ANNABAI 

Aya : 36

جَزَآءٗ مِّن رَّبِّكَ عَطَآءً حِسَابٗا

Hali yakuwa ni Malipo kutoka kwa Mola wako, ni kipawa cha kutosha



Sura: ANNABAI 

Aya : 37

رَّبِّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا ٱلرَّحۡمَٰنِۖ لَا يَمۡلِكُونَ مِنۡهُ خِطَابٗا

Mola wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake Mwingi wa rehema; hawatoweza kumsemesha



Sura: ANNABAI 

Aya : 38

يَوۡمَ يَقُومُ ٱلرُّوحُ وَٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ صَفّٗاۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنۡ أَذِنَ لَهُ ٱلرَّحۡمَٰنُ وَقَالَ صَوَابٗا

Siku atakayosimama Roho (Jibrili) na Malaika hali ya kujipanga safu; Hawatasema ila aliye mruhusu Mwingi wa rehema, na atasema yaliyo sawa tu



Sura: ANNABAI 

Aya : 39

ذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمُ ٱلۡحَقُّۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ مَـَٔابًا

Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anayetaka na ashike njia arejee kwa Mola wake



Sura: ANNABAI 

Aya : 40

إِنَّآ أَنذَرۡنَٰكُمۡ عَذَابٗا قَرِيبٗا يَوۡمَ يَنظُرُ ٱلۡمَرۡءُ مَا قَدَّمَتۡ يَدَاهُ وَيَقُولُ ٱلۡكَافِرُ يَٰلَيۡتَنِي كُنتُ تُرَٰبَۢا

Hakika Sisi Tumekuonyeni adhabu ya karibu, Siku mtu atakapotazama yale yaliyo tangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningelikuwa mchanga