فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ
Kwa sababu hakusadiki, wala hakusali, (hakumsadiki Mtume wala Qur’ani)
Kushiriki :
وَلَٰكِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ
Lakini alikadhibisha na akakengeuka
ثُمَّ ذَهَبَ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ يَتَمَطَّىٰٓ
Kisha akaenda kwa watu wake wa nyumbani kwa maringo
أَوۡلَىٰ لَكَ فَأَوۡلَىٰ
Ole wako! Ole wako! (Ewe unaye kadhibisha, utaangamia!)
ثُمَّ أَوۡلَىٰ لَكَ فَأَوۡلَىٰٓ
Kisha! Ole wako! Ole wako! (Ewe unaye kadhibisha, utaangamia!)
أَيَحۡسَبُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَن يُتۡرَكَ سُدًى
Je, mwanadamu anadhani kuwa ataachwa bure tu?
أَلَمۡ يَكُ نُطۡفَةٗ مِّن مَّنِيّٖ يُمۡنَىٰ
Kwani yeye hakuwa tone la manii lililotonwa?
ثُمَّ كَانَ عَلَقَةٗ فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ
Kisha akawa pande la damu, (Allaah) Akamuumba na Akamsawazisha?
فَجَعَلَ مِنۡهُ ٱلزَّوۡجَيۡنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰٓ
Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke
أَلَيۡسَ ذَٰلِكَ بِقَٰدِرٍ عَلَىٰٓ أَن يُحۡـِۧيَ ٱلۡمَوۡتَىٰ
Je! Huyo (aliyefanya hivyo) hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu?