Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 31

وَمَا جَعَلۡنَآ أَصۡحَٰبَ ٱلنَّارِ إِلَّا مَلَـٰٓئِكَةٗۖ وَمَا جَعَلۡنَا عِدَّتَهُمۡ إِلَّا فِتۡنَةٗ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ لِيَسۡتَيۡقِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ وَيَزۡدَادَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِيمَٰنٗا وَلَا يَرۡتَابَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ وَلِيَقُولَ ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ وَٱلۡكَٰفِرُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِهَٰذَا مَثَلٗاۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُۚ وَمَا يَعۡلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَۚ وَمَا هِيَ إِلَّا ذِكۡرَىٰ لِلۡبَشَرِ

Na Hatukuweka walinzi wa moto isipokuwa ni Malaika, na Hatukufanya idadi yao isipokuwa iwe ni mtihani kwa wale waliokufuru; ili wawe na yakini wale waliopewa Kitabu, na iwazidishie Imani wale walioamini; na wala wasitie shaka wale waliopewa Kitabu na Waumini; na ili wale waliokuwa na maradhi nyoyoni mwao (ya unafiki), na makafiri waseme: Allah Amekusudia nini kwa mfano huu? Hivyo ndivyo Allah Anavyompoteza Amtakaye na Anamuongoa Amtakaye. Na hakuna ajuaye majeshi ya Mola wako isipokuwa Yeye Peke yake, na haya hayakuwa isipokuwa ni ukumbusho tu kwa binadamu



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 32

كَلَّا وَٱلۡقَمَرِ

Sivyo hivyo! Naapa kwa mwezi



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 33

وَٱلَّيۡلِ إِذۡ أَدۡبَرَ

Na Naapa kwa usiku unapoondoka



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 34

وَٱلصُّبۡحِ إِذَآ أَسۡفَرَ

Na Naapa kwa asubuhi inapoangaza (inapo pambazuka)



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 35

إِنَّهَا لَإِحۡدَى ٱلۡكُبَرِ

Hakika huo (Moto) bila shaka ni mojawapo ya majanga makubwa kabisa



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 36

نَذِيرٗا لِّلۡبَشَرِ

Ni onyo kwa binadamu



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 37

لِمَن شَآءَ مِنكُمۡ أَن يَتَقَدَّمَ أَوۡ يَتَأَخَّرَ

Kwa atakaye miongoni mwenu atatangulia mbele au atachelewa nyuma



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 38

كُلُّ نَفۡسِۭ بِمَا كَسَبَتۡ رَهِينَةٌ

Kila nafsi iko katika rehani kwa yale iliyoyachuma.[1]


1- - Kila nafsi itashikwa kwa iliyo yatenda.


Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 39

إِلَّآ أَصۡحَٰبَ ٱلۡيَمِينِ

Isipokuwa watu wa kuliani



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 40

فِي جَنَّـٰتٖ يَتَسَآءَلُونَ

Hao watakuwa katika Mabustani ya Peponi, wanaulizana



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 41

عَنِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ

Kuhusu wakosefu



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 42

مَا سَلَكَكُمۡ فِي سَقَرَ

(Watawauliza): Nini kilicho kuingizeni katika Moto?



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 43

قَالُواْ لَمۡ نَكُ مِنَ ٱلۡمُصَلِّينَ

Watasema: Hatukuwa miongoni mwa wanaosali



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 44

وَلَمۡ نَكُ نُطۡعِمُ ٱلۡمِسۡكِينَ

Na wala hatukuwa tunalisha masikini



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 45

وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ ٱلۡخَآئِضِينَ

Na tulikuwa tukipiga porojo pamoja na wanaopiga porojo



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 46

وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ

Na tulikuwa tunaikadhibisha Siku ya malipo



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 47

حَتَّىٰٓ أَتَىٰنَا ٱلۡيَقِينُ

Mpaka ikatufikia yakini (mauti)



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 48

فَمَا تَنفَعُهُمۡ شَفَٰعَةُ ٱلشَّـٰفِعِينَ

Basi haitowafaa uombezi wowote wa waombezi



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 49

فَمَا لَهُمۡ عَنِ ٱلتَّذۡكِرَةِ مُعۡرِضِينَ

Basi wana nini hata wanapuuza ukumbusho huu!



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 50

كَأَنَّهُمۡ حُمُرٞ مُّسۡتَنفِرَةٞ

Kama kwamba ni punda milia wenye kutimuliwa, (wenye kushtuka)



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 51

فَرَّتۡ مِن قَسۡوَرَةِۭ

Wamekimbia mbio kutokana na kumkimbia simba



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 52

بَلۡ يُرِيدُ كُلُّ ٱمۡرِيٕٖ مِّنۡهُمۡ أَن يُؤۡتَىٰ صُحُفٗا مُّنَشَّرَةٗ

Bali anataka kila mtu miongoni mwao apewe nyaraka zilizofunuliwa



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 53

كَلَّاۖ بَل لَّا يَخَافُونَ ٱلۡأٓخِرَةَ

Si hivyo! hasha! Bali hawaiogopi Akhera



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 54

كَلَّآ إِنَّهُۥ تَذۡكِرَةٞ

Na sihivyo! Hakika hii (Qur’ani) ni mawaidha



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 55

فَمَن شَآءَ ذَكَرَهُۥ

Basi anayetaka atawaidhika



Sura: ALMUDDATH-THIR 

Aya : 56

وَمَا يَذۡكُرُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُۚ هُوَ أَهۡلُ ٱلتَّقۡوَىٰ وَأَهۡلُ ٱلۡمَغۡفِرَةِ

Na hawatowaidhika isipokuwa Akitaka Allah; Yeye Ndiye mwenye kustahiki kuogopwa, na mwenye kustahiki kusamehe (madhambi)