Sura: ALMA’RIJ 

Aya : 31

فَمَنِ ٱبۡتَغَىٰ وَرَآءَ ذَٰلِكَ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡعَادُونَ

Basi yeyote yule atakayetaka kinyume ya hayo, basi hao ndio warukao mipaka



Sura: ALMA’RIJ 

Aya : 32

وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِأَمَٰنَٰتِهِمۡ وَعَهۡدِهِمۡ رَٰعُونَ

Na ambao amana zao na ahadi zao ni wenye kuzichunga (na kuzitimiza)



Sura: ALMA’RIJ 

Aya : 33

وَٱلَّذِينَ هُم بِشَهَٰدَٰتِهِمۡ قَآئِمُونَ

Na ambao wanasimama imara katika kutoa ushahidi wao,



Sura: ALMA’RIJ 

Aya : 34

وَٱلَّذِينَ هُمۡ عَلَىٰ صَلَاتِهِمۡ يُحَافِظُونَ

Na ambao kwenye Sala zao ni wenye kuzilinda



Sura: ALMA’RIJ 

Aya : 35

أُوْلَـٰٓئِكَ فِي جَنَّـٰتٖ مُّكۡرَمُونَ

Hao ndio watakao heshimiwa Peponi



Sura: ALMA’RIJ 

Aya : 36

فَمَالِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ قِبَلَكَ مُهۡطِعِينَ

Wana nini wale walio kufuru (wanaharakiza mbele yako) na wanakutumbulia macho tu?



Sura: ALMA’RIJ 

Aya : 37

عَنِ ٱلۡيَمِينِ وَعَنِ ٱلشِّمَالِ عِزِينَ

(Kukukalia) makundi kwa makundi kuliani na kushotoni.[1]


1- - Kitu gani kinawapelekea hao walio kufuru kukujia mbio mbio kutoka kuliani na kushotoni kwa makundi?.


Sura: ALMA’RIJ 

Aya : 38

أَيَطۡمَعُ كُلُّ ٱمۡرِيٕٖ مِّنۡهُمۡ أَن يُدۡخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٖ

Je, kwani kila mmoja wao ana tamaa ya kuingia kwenye Pepo yenye neema?



Sura: ALMA’RIJ 

Aya : 39

كَلَّآۖ إِنَّا خَلَقۡنَٰهُم مِّمَّا يَعۡلَمُونَ

Sivyo hivyo! Hakika Sisi Tumewaumba kutokana na kile wanachokijua.[1]


1- - Basi nawaache hiyo tamaa yao ya kuingia Peponi. Hakika Sisi tumewaumba wao kutokana na maji ya kudharauliwa (dhalili).


Sura: ALMA’RIJ 

Aya : 40

فَلَآ أُقۡسِمُ بِرَبِّ ٱلۡمَشَٰرِقِ وَٱلۡمَغَٰرِبِ إِنَّا لَقَٰدِرُونَ

Basi Naapa kwa Mola wa Mashariki zote na Magharibi zote, hakika Sisi bila shaka ni Wenye kuweza



Sura: ALMA’RIJ 

Aya : 41

عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ خَيۡرٗا مِّنۡهُمۡ وَمَا نَحۡنُ بِمَسۡبُوقِينَ

(Tuna uwezo wa) Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi



Sura: ALMA’RIJ 

Aya : 42

فَذَرۡهُمۡ يَخُوضُواْ وَيَلۡعَبُواْ حَتَّىٰ يُلَٰقُواْ يَوۡمَهُمُ ٱلَّذِي يُوعَدُونَ

Basi waachilie mbali watumbukie katika porojo na upuuzi, na wacheze, mpaka wakutane na Siku yao ambayo wanayo ahidiwa



Sura: ALMA’RIJ 

Aya : 43

يَوۡمَ يَخۡرُجُونَ مِنَ ٱلۡأَجۡدَاثِ سِرَاعٗا كَأَنَّهُمۡ إِلَىٰ نُصُبٖ يُوفِضُونَ

Siku watapotoka makaburini haraka haraka kana kwamba wanakimbilia kushindana kuifikia kwenye Lengo



Sura: ALMA’RIJ 

Aya : 44

خَٰشِعَةً أَبۡصَٰرُهُمۡ تَرۡهَقُهُمۡ ذِلَّةٞۚ ذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمُ ٱلَّذِي كَانُواْ يُوعَدُونَ

Macho yao yatainama chini, udhalili utawafunika. Hiyo ndio ile siku waliyokuwa wakiahidiwa