Sura: ALHAAQQA 

Aya : 31

ثُمَّ ٱلۡجَحِيمَ صَلُّوهُ

Kisha kwenye moto uwakao vikali mtupeni humo!



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 32

ثُمَّ فِي سِلۡسِلَةٖ ذَرۡعُهَا سَبۡعُونَ ذِرَاعٗا فَٱسۡلُكُوهُ

Mkamateni Na Mtieni Minyororo Shingoni Mwake,



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 33

إِنَّهُۥ كَانَ لَا يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ ٱلۡعَظِيمِ

Kwani huyo hakika alikuwa hamuamini Allah Mtukufu



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 34

وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ

Wala Hakuhimiza Juu Ya Kulisha Maskini



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 35

فَلَيۡسَ لَهُ ٱلۡيَوۡمَ هَٰهُنَا حَمِيمٞ

Basi Leo Hapa Hana Rafiki Mpenzi ( wa kumwonea uchungu)



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 36

وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنۡ غِسۡلِينٖ

Na wala hana chakula isipokuwa maji ya usaha ya vidonda vilivyooshwa (vya watu wa motoni)



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 37

لَّا يَأۡكُلُهُۥٓ إِلَّا ٱلۡخَٰطِـُٔونَ

Hawakili chakula hicho isipokuwa wakosefu



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 38

فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَا تُبۡصِرُونَ

Basi Naapa kwa yale mnayoyaona



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 39

وَمَا لَا تُبۡصِرُونَ

Na Naapa kwa yale msiyoyaona



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 40

إِنَّهُۥ لَقَوۡلُ رَسُولٖ كَرِيمٖ

Kwa hakika hii (Qur’ani) ni kauli iliyo letwa na Mjumbe mwenye heshima



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 41

وَمَا هُوَ بِقَوۡلِ شَاعِرٖۚ قَلِيلٗا مَّا تُؤۡمِنُونَ

Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayoyaamini



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 42

وَلَا بِقَوۡلِ كَاهِنٖۚ قَلِيلٗا مَّا تَذَكَّرُونَ

Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo yakumbuka



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 43

تَنزِيلٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Ni Uteremsho Kutoka Kwa Mola Wa Viumbe Vyote



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 44

وَلَوۡ تَقَوَّلَ عَلَيۡنَا بَعۡضَ ٱلۡأَقَاوِيلِ

Na Kama (Mtume) Angelizua Juu Yetu Baadhi Ya Maneno tu,



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 45

لَأَخَذۡنَا مِنۡهُ بِٱلۡيَمِينِ

Bila ya shaka tungeli mshika kwa mkono wa kulia



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 46

ثُمَّ لَقَطَعۡنَا مِنۡهُ ٱلۡوَتِينَ

Kisha kwa hakika tungeli mkata mshipa mkubwa (wa moyo!)



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 47

فَمَا مِنكُم مِّنۡ أَحَدٍ عَنۡهُ حَٰجِزِينَ

Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeli weza kutuzuia



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 48

وَإِنَّهُۥ لَتَذۡكِرَةٞ لِّلۡمُتَّقِينَ

Kwa hakika hii (Qur’ani) ni ukumbusho kwa wachamungu



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 49

وَإِنَّا لَنَعۡلَمُ أَنَّ مِنكُم مُّكَذِّبِينَ

Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanao kadhibisha



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 50

وَإِنَّهُۥ لَحَسۡرَةٌ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na hakika hii (Qur’ani) bila shaka itakuwa ni majuto makubwa juu ya makafiri



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 51

وَإِنَّهُۥ لَحَقُّ ٱلۡيَقِينِ

Na hakika hii (Qur’an) ni haki ya yakini



Sura: ALHAAQQA 

Aya : 52

فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ

Basi litukuze jina la Mola Wako aliye Mkuu