Sura: ATTUR 

Aya : 31

قُلۡ تَرَبَّصُواْ فَإِنِّي مَعَكُم مِّنَ ٱلۡمُتَرَبِّصِينَ

Sema subirini basi hakika mimi pamoja nanyi ni miongoni mwa wenye kusubiri



Sura: ATTUR 

Aya : 32

أَمۡ تَأۡمُرُهُمۡ أَحۡلَٰمُهُم بِهَٰذَآۚ أَمۡ هُمۡ قَوۡمٞ طَاغُونَ

Au zinawaamuru wao ndoto zao kwa hili au wao ni watu waovu



Sura: ATTUR 

Aya : 33

أَمۡ يَقُولُونَ تَقَوَّلَهُۥۚ بَل لَّا يُؤۡمِنُونَ

Au wanasema ameizua hiyo qurani bali hawaamini



Sura: ATTUR 

Aya : 34

فَلۡيَأۡتُواْ بِحَدِيثٖ مِّثۡلِهِۦٓ إِن كَانُواْ صَٰدِقِينَ

Basi walete mazungumzo (Quran) mfano wake kama watakua wakweli



Sura: ATTUR 

Aya : 35

أَمۡ خُلِقُواْ مِنۡ غَيۡرِ شَيۡءٍ أَمۡ هُمُ ٱلۡخَٰلِقُونَ

Au wameumbwa pasipo na kitu chochote (bila ya muumba) au wao ndio waumbaji?



Sura: ATTUR 

Aya : 36

أَمۡ خَلَقُواْ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَۚ بَل لَّا يُوقِنُونَ

Au wameumba mbingu na ardhi? Bali hawana yakini



Sura: ATTUR 

Aya : 37

أَمۡ عِندَهُمۡ خَزَآئِنُ رَبِّكَ أَمۡ هُمُ ٱلۡمُصَۜيۡطِرُونَ

Au wanazo hazina za Mola wako mlezi, au wao ndio wenye madaraka? (wenye kudhibiti)?



Sura: ATTUR 

Aya : 38

أَمۡ لَهُمۡ سُلَّمٞ يَسۡتَمِعُونَ فِيهِۖ فَلۡيَأۡتِ مُسۡتَمِعُهُم بِسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٍ

Au wanazo ngazi wanasikilizia kwa makini humo? Basi msikilizaji wao alete dalili bayana



Sura: ATTUR 

Aya : 39

أَمۡ لَهُ ٱلۡبَنَٰتُ وَلَكُمُ ٱلۡبَنُونَ

Au (Allah) Ana watoto wa kike, nanyi mna watoto wa kiume?



Sura: ATTUR 

Aya : 40

أَمۡ تَسۡـَٔلُهُمۡ أَجۡرٗا فَهُم مِّن مَّغۡرَمٖ مُّثۡقَلُونَ

Au unawaomba ujira kwa hiyo wameelemewa na uzito wa gharama?



Sura: ATTUR 

Aya : 41

أَمۡ عِندَهُمُ ٱلۡغَيۡبُ فَهُمۡ يَكۡتُبُونَ

Au wanayo elimu ya ghayb kisha wao wanaandika?



Sura: ATTUR 

Aya : 42

أَمۡ يُرِيدُونَ كَيۡدٗاۖ فَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ هُمُ ٱلۡمَكِيدُونَ

Au wanakusudia hila (shari)? Basi wale waliokufuru wao ndio watakaopangiwa hila



Sura: ATTUR 

Aya : 43

أَمۡ لَهُمۡ إِلَٰهٌ غَيۡرُ ٱللَّهِۚ سُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Au wana wao mungu asiye Allah utakasifu ni wake allah na yote wanayomshirikisha nayo



Sura: ATTUR 

Aya : 44

وَإِن يَرَوۡاْ كِسۡفٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ سَاقِطٗا يَقُولُواْ سَحَابٞ مَّرۡكُومٞ

Na hata wangeliona pande la moto kutoka mbinguni linaanguka wangelisema: Mawingu tu yamerundikana



Sura: ATTUR 

Aya : 45

فَذَرۡهُمۡ حَتَّىٰ يُلَٰقُواْ يَوۡمَهُمُ ٱلَّذِي فِيهِ يُصۡعَقُونَ

Basi waachilie mbali mpaka wakutane na Siku yao ambayo humo wataangamizwa



Sura: ATTUR 

Aya : 46

يَوۡمَ لَا يُغۡنِي عَنۡهُمۡ كَيۡدُهُمۡ شَيۡـٔٗا وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ

Siku ambayo njama zao hazitowafaa kitu chochote, na wala wao hawatonusuriwa



Sura: ATTUR 

Aya : 47

وَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُواْ عَذَابٗا دُونَ ذَٰلِكَ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ

Na hakika wale waliodhulumu watapata adhabu nyingine isiyokuwa hiyo, lakini wengi wao hawajui



Sura: ATTUR 

Aya : 48

وَٱصۡبِرۡ لِحُكۡمِ رَبِّكَ فَإِنَّكَ بِأَعۡيُنِنَاۖ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ حِينَ تَقُومُ

Na subiri hukumu ya mola wako mlezi na hakika wewe uko machoni kwetu (uangalizi wetu) na msabihi Mola wako mlezi pamoja na kusifu wakati unapoamka



Sura: ATTUR 

Aya : 49

وَمِنَ ٱلَّيۡلِ فَسَبِّحۡهُ وَإِدۡبَٰرَ ٱلنُّجُومِ

Na katika usiku Msabbih na zinapokuchwa nyota