Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 31

وَعَلَّمَ ءَادَمَ ٱلۡأَسۡمَآءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمۡ عَلَى ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةِ فَقَالَ أَنۢبِـُٔونِي بِأَسۡمَآءِ هَـٰٓؤُلَآءِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Na akamfundisha Adamu majina yote, kisha akawaleta wenye majina hayo mbele ya malaika. Akawaambia: Nitajieni majina ya hawa kama ninyi ni wa kweli



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 32

قَالُواْ سُبۡحَٰنَكَ لَا عِلۡمَ لَنَآ إِلَّا مَا عَلَّمۡتَنَآۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡحَكِيمُ

Wakasema: Utakatifu ni wako. Hakuna tunachokijua ila tu ulichotujulisha. Hakika, wewe tu ndiye Mjuzi, Mwenye hekima



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 33

قَالَ يَـٰٓـَٔادَمُ أَنۢبِئۡهُم بِأَسۡمَآئِهِمۡۖ فَلَمَّآ أَنۢبَأَهُم بِأَسۡمَآئِهِمۡ قَالَ أَلَمۡ أَقُل لَّكُمۡ إِنِّيٓ أَعۡلَمُ غَيۡبَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَأَعۡلَمُ مَا تُبۡدُونَ وَمَا كُنتُمۡ تَكۡتُمُونَ

Akasema: Ewe Adamu, waambie majina yao. Basi alipowaambia majina yao, (Allah) akasema: Je, si nilikuambieni kuwa mimi ninajua visivyoonekana mbinguni na ardhini? Na ninayajua mno mnayo yadhihirisha na mnayoyaficha



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 34

وَإِذۡ قُلۡنَا لِلۡمَلَـٰٓئِكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأٓدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ أَبَىٰ وَٱسۡتَكۡبَرَ وَكَانَ مِنَ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na (kumbuka) tulipowaambia Malaika (kuwa): Msujudieni Adamu. Wakasujudu, isipokuwa Ibilisi alikataa na kuleta kiburi na akawa miongoni mwa makafiri



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 35

وَقُلۡنَا يَـٰٓـَٔادَمُ ٱسۡكُنۡ أَنتَ وَزَوۡجُكَ ٱلۡجَنَّةَ وَكُلَا مِنۡهَا رَغَدًا حَيۡثُ شِئۡتُمَا وَلَا تَقۡرَبَا هَٰذِهِ ٱلشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Na tulisema: Ewe Adamu, ishi wewe na mkeo Peponi na kuleni humo kwa uhuru popote mtakapo na msiusogelee mti huu ili msije mkawa miongoni mwa madhalimu



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 36

فَأَزَلَّهُمَا ٱلشَّيۡطَٰنُ عَنۡهَا فَأَخۡرَجَهُمَا مِمَّا كَانَا فِيهِۖ وَقُلۡنَا ٱهۡبِطُواْ بَعۡضُكُمۡ لِبَعۡضٍ عَدُوّٞۖ وَلَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُسۡتَقَرّٞ وَمَتَٰعٌ إِلَىٰ حِينٖ

Shetani akawatelezesha kwenye Pepo hiyo, hivyo akawatoa katika hali waliyokuwa nayo. Na tukasema: Teremkeni. Nyinyi kwa nyinyi mtakuwa maadui. Na mtakuwa na makazi na starehe ardhini mpaka muda maalumu



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 37

فَتَلَقَّىٰٓ ءَادَمُ مِن رَّبِّهِۦ كَلِمَٰتٖ فَتَابَ عَلَيۡهِۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ

Adamu akapokea maneno (ya toba) kutoka kwa Mola wake (akatubu) na (Allah) akamkubalia toba yake. Hakika yeye (Allah) ni Mwingi wa kupokea toba, Mwingi wa rehema



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 38

قُلۡنَا ٱهۡبِطُواْ مِنۡهَا جَمِيعٗاۖ فَإِمَّا يَأۡتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدٗى فَمَن تَبِعَ هُدَايَ فَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Tukasema: Teremkeni humo nyote. Basi utakapokujieni muongozo kutoka kwangu, watakaoufuata muongozo wangu hawatakuwa na hofu yoyote na wao hawatahuzunika



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 39

وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآ أُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Na ambao wamekufuru na wakazikadhibisha Aya zetu, hao ni watu wa motoni, wataishi humo milele



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 40

يَٰبَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتِيَ ٱلَّتِيٓ أَنۡعَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ وَأَوۡفُواْ بِعَهۡدِيٓ أُوفِ بِعَهۡدِكُمۡ وَإِيَّـٰيَ فَٱرۡهَبُونِ

Enyi Wana wa Israeli, kumbukeni neema zangu ambazo nimekuneemesheni, na tekelezeni ahadi zangu, nami nitekeleze ahadi zenu, naniogopeni mimi tu



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 41

وَءَامِنُواْ بِمَآ أَنزَلۡتُ مُصَدِّقٗا لِّمَا مَعَكُمۡ وَلَا تَكُونُوٓاْ أَوَّلَ كَافِرِۭ بِهِۦۖ وَلَا تَشۡتَرُواْ بِـَٔايَٰتِي ثَمَنٗا قَلِيلٗا وَإِيَّـٰيَ فَٱتَّقُونِ

Na yaaminini yale niliyo-yateremsha yakiwa yanasadikisha hayo mliyonayo, na msiwe wa kwanza kuyakufuru, na msizi-badilishe Aya zangu kwa thamani ndogo, na mniogope mimi tu



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 42

وَلَا تَلۡبِسُواْ ٱلۡحَقَّ بِٱلۡبَٰطِلِ وَتَكۡتُمُواْ ٱلۡحَقَّ وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Na msichanganye haki na batili na msifiche haki na ilhali mnajua



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 43

وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱرۡكَعُواْ مَعَ ٱلرَّـٰكِعِينَ

Na simamisheni Swala na toeni Zaka na rukuuni pamoja na wanaorukuu



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 44

۞أَتَأۡمُرُونَ ٱلنَّاسَ بِٱلۡبِرِّ وَتَنسَوۡنَ أَنفُسَكُمۡ وَأَنتُمۡ تَتۡلُونَ ٱلۡكِتَٰبَۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Je, mnaamrisha watu kutenda wema na mnajisahau, na ilhali nyinyi mnakisoma kitabu? Je, hamtumii akili?



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 45

وَٱسۡتَعِينُواْ بِٱلصَّبۡرِ وَٱلصَّلَوٰةِۚ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى ٱلۡخَٰشِعِينَ

Na ombeni msaada kwa kusubiri na kuswali. Na kwa hakika kabisa, hiyo Swala ni nzito mno isipokuwa kwa wanyenyekevu tu



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 46

ٱلَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَٰقُواْ رَبِّهِمۡ وَأَنَّهُمۡ إِلَيۡهِ رَٰجِعُونَ

Ambao wana yakini kwamba watakutana na Mola wao, na kwamba kwake tu watarejea



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 47

يَٰبَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتِيَ ٱلَّتِيٓ أَنۡعَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ وَأَنِّي فَضَّلۡتُكُمۡ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ

Enyi Wana wa Israeli, kumbukeni neema zangu nilizo kuneemesheni, na kwamba mimi nimekufanyeni bora kuliko walimwengu (wa zama zenu)



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 48

وَٱتَّقُواْ يَوۡمٗا لَّا تَجۡزِي نَفۡسٌ عَن نَّفۡسٖ شَيۡـٔٗا وَلَا يُقۡبَلُ مِنۡهَا شَفَٰعَةٞ وَلَا يُؤۡخَذُ مِنۡهَا عَدۡلٞ وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ

Na iogopeni siku ambayo nafsi haitaisaidia chochote nafsi nyingine, na wala hautakubaliwa uombezi wowote kwa nafsi hiyo (kumuombea mwengine), na wala haitachukuliwa fidia yoyote kwa nafsi hiyo, nao hawatanusuriwa



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 49

وَإِذۡ نَجَّيۡنَٰكُم مِّنۡ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ يَسُومُونَكُمۡ سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِ يُذَبِّحُونَ أَبۡنَآءَكُمۡ وَيَسۡتَحۡيُونَ نِسَآءَكُمۡۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَآءٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَظِيمٞ

Na (kumbukeni) tulipokuokoeni kutoka kwenye mateso ya Firauni na watu wake waliokupeni adhabu mbaya kabisa; wakiwauwa watoto wenu wanaume kwa kuwachinjachinja na wakiwaacha hai watoto wenu wanawake. Na katika hayo kuna mtihani mkubwa sana kwenu kutoka kwa Mola wenu



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 50

وَإِذۡ فَرَقۡنَا بِكُمُ ٱلۡبَحۡرَ فَأَنجَيۡنَٰكُمۡ وَأَغۡرَقۡنَآ ءَالَ فِرۡعَوۡنَ وَأَنتُمۡ تَنظُرُونَ

Na (kumbukeni) tulipokut-enganishieni bahari tukakuokoeni na tukawazamisha watu wa Firauni na nyinyi mkitazama



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 51

وَإِذۡ وَٰعَدۡنَا مُوسَىٰٓ أَرۡبَعِينَ لَيۡلَةٗ ثُمَّ ٱتَّخَذۡتُمُ ٱلۡعِجۡلَ مِنۢ بَعۡدِهِۦ وَأَنتُمۡ ظَٰلِمُونَ

Na (kumbukeni) tulipoahidiana na Musa siku arobaini, kisha nyinyi mkamfanya ndama (kuwa Mungu) baada ya hapo, na ilhali nyinyi ni wenye kudhulumu (nafsi zenu)”



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 52

ثُمَّ عَفَوۡنَا عَنكُم مِّنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ

Kisha tukakusameheni baada ya hapo ili mpate kushukuru



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 53

وَإِذۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡفُرۡقَانَ لَعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ

Na (kumbukeni) tulipompa Musa kitabu na upambanuzi ili mpate kuongoka



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 54

وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِۦ يَٰقَوۡمِ إِنَّكُمۡ ظَلَمۡتُمۡ أَنفُسَكُم بِٱتِّخَاذِكُمُ ٱلۡعِجۡلَ فَتُوبُوٓاْ إِلَىٰ بَارِئِكُمۡ فَٱقۡتُلُوٓاْ أَنفُسَكُمۡ ذَٰلِكُمۡ خَيۡرٞ لَّكُمۡ عِندَ بَارِئِكُمۡ فَتَابَ عَلَيۡكُمۡۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ

Na (kumbukeni) Musa alip-owaambia watu wake (kuwa): Enyi watu wangu, kwa hakika nyinyi mmezidhulumu nafsi zenu kwa kumfanya kwenu ndama Mungu. Basi tubieni kwa Mola wenu na uaneni. Hilo ni bora kwenu mbeleya Muumba wenu. Allah akakubali toba yenu. Kwa hakika, yeye ni Mwingi wa kukubali toba, Mwingi wa rehema



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 55

وَإِذۡ قُلۡتُمۡ يَٰمُوسَىٰ لَن نُّؤۡمِنَ لَكَ حَتَّىٰ نَرَى ٱللَّهَ جَهۡرَةٗ فَأَخَذَتۡكُمُ ٱلصَّـٰعِقَةُ وَأَنتُمۡ تَنظُرُونَ

Na (kumbukeni) mliposema (kumwambia Mtume Musa kuwa): Ewe Musa, hatutakuamini mpaka tumuone Allah waziwazi. Basi ukakuchukueni (ukakuteketezeni) moto wa radi na hali mnatazama



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 56

ثُمَّ بَعَثۡنَٰكُم مِّنۢ بَعۡدِ مَوۡتِكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ

Kisha tukakufufueni baada ya kufa kwenu ili mpate kushukuru



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 57

وَظَلَّلۡنَا عَلَيۡكُمُ ٱلۡغَمَامَ وَأَنزَلۡنَا عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَنَّ وَٱلسَّلۡوَىٰۖ كُلُواْ مِن طَيِّبَٰتِ مَا رَزَقۡنَٰكُمۡۚ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ

Na tukakufunikeni kivuli cha mawingu na tukakuteremshieni Mana na Salwa, (na kukuambieni): Kuleni katika vitu vizuri tulivyokuruzukuni, na hawakutudhulumu sisi, lakini walikuwa wanajidhulumu wenyewe



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 58

وَإِذۡ قُلۡنَا ٱدۡخُلُواْ هَٰذِهِ ٱلۡقَرۡيَةَ فَكُلُواْ مِنۡهَا حَيۡثُ شِئۡتُمۡ رَغَدٗا وَٱدۡخُلُواْ ٱلۡبَابَ سُجَّدٗا وَقُولُواْ حِطَّةٞ نَّغۡفِرۡ لَكُمۡ خَطَٰيَٰكُمۡۚ وَسَنَزِيدُ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Na (kumbuka) tuliposema (kuwaambia Wana wa Israili kuwa): Ingieni katika mji huu. Kuleni humo mtakavyo (na) kwa wasaa, naingieni katika lango mkiwa mmesujudu, na sememeni: “Ombi letu ni kusamehewa dhambi”, tutakusameheni makosa yenu. Na tutawazidishia watendao mazuri



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 59

فَبَدَّلَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ قَوۡلًا غَيۡرَ ٱلَّذِي قِيلَ لَهُمۡ فَأَنزَلۡنَا عَلَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ رِجۡزٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ بِمَا كَانُواْ يَفۡسُقُونَ

Basi waliodhulumu walibadilisha kauli (nyingine) sio ile waliyoambiwa. Kwa sababu hiyo, tuliwateremshia waliodhulumu adhabu kutoka mbinguni kwa sababu ya uovu waliokuwa wakiufanya



Sura: AL-BAQARAH 

Aya : 60

۞وَإِذِ ٱسۡتَسۡقَىٰ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِۦ فَقُلۡنَا ٱضۡرِب بِّعَصَاكَ ٱلۡحَجَرَۖ فَٱنفَجَرَتۡ مِنۡهُ ٱثۡنَتَا عَشۡرَةَ عَيۡنٗاۖ قَدۡ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٖ مَّشۡرَبَهُمۡۖ كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ مِن رِّزۡقِ ٱللَّهِ وَلَا تَعۡثَوۡاْ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُفۡسِدِينَ

Na kumbuka Musa alipo-waombea maji watu wake tukam-wambia: Lipige jiwe kwa fimbo yako. (Alipolipiga) Zikabubujika kutoka katika jiwe hilo chemchemi kumi na mbili. Kila watu walijua mahali pao pa (kuchota maji ya) kunywa. (Tuliwaambia:) Kuleni na kunyweni katika riziki za Allah, na msifanye uovu katika ardhi