Sura: YUNUS 

Aya : 31

قُلۡ مَن يَرۡزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ أَمَّن يَمۡلِكُ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡأَبۡصَٰرَ وَمَن يُخۡرِجُ ٱلۡحَيَّ مِنَ ٱلۡمَيِّتِ وَيُخۡرِجُ ٱلۡمَيِّتَ مِنَ ٱلۡحَيِّ وَمَن يُدَبِّرُ ٱلۡأَمۡرَۚ فَسَيَقُولُونَ ٱللَّهُۚ فَقُلۡ أَفَلَا تَتَّقُونَ

Sema: Ni nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini? Au ni nani anayemiliki masikio na macho? Na ni nani atoae kilicho hai kutoka katika kilichokufa na atoae kilichokufa kutoka katika kilicho hai? Na ni nani anaye endesha mambo yote? Bila shaka watasema: Ni Allah. Basi sema: Hivi ni kwa nini hamuwi wachaMungu?



Sura: YUNUS 

Aya : 32

فَذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمُ ٱلۡحَقُّۖ فَمَاذَا بَعۡدَ ٱلۡحَقِّ إِلَّا ٱلضَّلَٰلُۖ فَأَنَّىٰ تُصۡرَفُونَ

Basi huyo ndiye Allah Mola wenu Mlezi. Basi ni nini baada ya haki sio upotevu tu? Basi ni vipi mnageuzwa (mnapotoshwa)?



Sura: YUNUS 

Aya : 33

كَذَٰلِكَ حَقَّتۡ كَلِمَتُ رَبِّكَ عَلَى ٱلَّذِينَ فَسَقُوٓاْ أَنَّهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ

Kama hivyo (ilivyothibiti kwamba Mola wenu ni wa haki ndio hivyo hivyo), imethibiti kauli ya Mola wako Mlezi kwa wale waliofanya uovu kwamba, wao hawaamini



Sura: YUNUS 

Aya : 34

قُلۡ هَلۡ مِن شُرَكَآئِكُم مَّن يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥۚ قُلِ ٱللَّهُ يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥۖ فَأَنَّىٰ تُؤۡفَكُونَ

Sema: Hivi, katika washirika (Miungu) wenu mnaowashirikisha na (Allah) yupo yeyote anayeanzisha kuumba (viumbe) kisha akarudia kuumba? Sema: Allah pekee ndiye anayeanzisha kuumba kisha (Siku ya Kiyama) atavirudisha alivyoviumba (kama vilivyokuwa mwanzo). Kwanini mnapotoshwa kuhusu kumpwekesha Allah!?



Sura: YUNUS 

Aya : 35

قُلۡ هَلۡ مِن شُرَكَآئِكُم مَّن يَهۡدِيٓ إِلَى ٱلۡحَقِّۚ قُلِ ٱللَّهُ يَهۡدِي لِلۡحَقِّۗ أَفَمَن يَهۡدِيٓ إِلَى ٱلۡحَقِّ أَحَقُّ أَن يُتَّبَعَ أَمَّن لَّا يَهِدِّيٓ إِلَّآ أَن يُهۡدَىٰۖ فَمَا لَكُمۡ كَيۡفَ تَحۡكُمُونَ

Sema: Hivi katika washirika (Miungu) wenu (mnaowashirikisha na Allah), yupo anayeongoza kwenye haki? Sema: Allah pekee ndiye anayeongoza kwenye haki. Basi, hivi anayeongoza kwenye haki ana haki zaidi ya kufuatwa au (mwenye haki zaidi ya kufuatwa ni) yule asiyeweza kuongoza chochote isipokuwa aongozwe? Basi mnanini nyinyi? Mnahukumuje?



Sura: YUNUS 

Aya : 36

وَمَا يَتَّبِعُ أَكۡثَرُهُمۡ إِلَّا ظَنًّاۚ إِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغۡنِي مِنَ ٱلۡحَقِّ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمُۢ بِمَا يَفۡعَلُونَ

Na wengi wao hawafuati isipokuwa dhana tu. Hakika, dhana haifaidishi chochote kwenye haki. Hakika, Allah ni Mjuzi wa wanayoyatenda



Sura: YUNUS 

Aya : 37

وَمَا كَانَ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانُ أَن يُفۡتَرَىٰ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَٰكِن تَصۡدِيقَ ٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَتَفۡصِيلَ ٱلۡكِتَٰبِ لَا رَيۡبَ فِيهِ مِن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Na haiwezekani Qur’ani hii kutungwa na yeyote kinyume na Allah, lakini (Qur’ani) ni usadikisho wa yote yaliyotangulia (katika vitabu na sheria za Manabii waliotangulia), na ni ufafanuzi wa kitabu (sheria za umma wa Muhammad) kisichokuwa na shaka kutoka kwa Mola mlezi wa walimwengu wote



Sura: YUNUS 

Aya : 38

أَمۡ يَقُولُونَ ٱفۡتَرَىٰهُۖ قُلۡ فَأۡتُواْ بِسُورَةٖ مِّثۡلِهِۦ وَٱدۡعُواْ مَنِ ٱسۡتَطَعۡتُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Au wanasema (kuwa Muhammad) ameitunga (hiyo Qur’ani)? Sema: Basi leteni sura moja tu mfano wake na waiteni muwawezao kuwaleta kinyume na Allah (wakusaidieni), kama nyinyi ni wa kweli (katika madai yenu)



Sura: YUNUS 

Aya : 39

بَلۡ كَذَّبُواْ بِمَا لَمۡ يُحِيطُواْ بِعِلۡمِهِۦ وَلَمَّا يَأۡتِهِمۡ تَأۡوِيلُهُۥۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Bali wamekadhibisha mambo wasiyoyajua undani wake, na haijawafikia tafsiri yake. Kama hivyo walikadhibisha waliokuwepo kabla yao. Basi angalia, ilikuwaje hatima ya madhalimu?



Sura: YUNUS 

Aya : 40

وَمِنۡهُم مَّن يُؤۡمِنُ بِهِۦ وَمِنۡهُم مَّن لَّا يُؤۡمِنُ بِهِۦۚ وَرَبُّكَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُفۡسِدِينَ

Na miongoni mwao wapo wanaoiamini (Qur’ani) na miongoni mwao wapo wasioiamini. Na Mola wako Mlezi anawajua sana waharibifu



Sura: YUNUS 

Aya : 41

وَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل لِّي عَمَلِي وَلَكُمۡ عَمَلُكُمۡۖ أَنتُم بَرِيٓـُٔونَ مِمَّآ أَعۡمَلُ وَأَنَا۠ بَرِيٓءٞ مِّمَّا تَعۡمَلُونَ

Na kama wakikukadhibisha, basi sema: Mimi nina amali zangu na nyinyi mna amali zenu. Nyinyi si wenye kuhusika na ninayoyafanya na mimi si mwenye kuhusika na mnayoyafanya



Sura: YUNUS 

Aya : 42

وَمِنۡهُم مَّن يَسۡتَمِعُونَ إِلَيۡكَۚ أَفَأَنتَ تُسۡمِعُ ٱلصُّمَّ وَلَوۡ كَانُواْ لَا يَعۡقِلُونَ

Na miongoni mwao wapo wanaokusikiliza. Hivi wewe utawasikilizisha viziwi na hata kama hawafahamu?[1]


1- - Aya hii inabainisha kuwa wapo baadhi ya makafiri wanaosikiliza Qur’ani kwa makini inaposomwa lakini hawaongoki na hawaifuati. Hivyo kusikiliza kwao Qur’ani bila ya kuifuta ni sawa na viziwi ambao hawasikii kabisa.


Sura: YUNUS 

Aya : 43

وَمِنۡهُم مَّن يَنظُرُ إِلَيۡكَۚ أَفَأَنتَ تَهۡدِي ٱلۡعُمۡيَ وَلَوۡ كَانُواْ لَا يُبۡصِرُونَ

Na miongoni mwao wapo wanaokutazama (na kuona dalili za Utume wako na nuru ya imani). Hivi wewe utawaongoza vipofu na ingawa hawaoni?



Sura: YUNUS 

Aya : 44

إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَظۡلِمُ ٱلنَّاسَ شَيۡـٔٗا وَلَٰكِنَّ ٱلنَّاسَ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ

Hakika, Allah hawadhulumu watu chochote na lakini watu wanazidhulumu nafsi zao



Sura: YUNUS 

Aya : 45

وَيَوۡمَ يَحۡشُرُهُمۡ كَأَن لَّمۡ يَلۡبَثُوٓاْ إِلَّا سَاعَةٗ مِّنَ ٱلنَّهَارِ يَتَعَارَفُونَ بَيۡنَهُمۡۚ قَدۡ خَسِرَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِلِقَآءِ ٱللَّهِ وَمَا كَانُواْ مُهۡتَدِينَ

Na (kumbuka) siku (Allah) atakapowakusanya (wataona) kana kwamba hawakukaa (duniani) isipokuwa saa moja tu ya mchana (muda mdogo tu wa mchana), wakitambulishana wao kwa wao. Hakika, wamekwisha pata hasara wale walioukadhibisha (waliokanusha) kukutana na Allah, na hawakuwa wenye kuongoka



Sura: YUNUS 

Aya : 46

وَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعۡضَ ٱلَّذِي نَعِدُهُمۡ أَوۡ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيۡنَا مَرۡجِعُهُمۡ ثُمَّ ٱللَّهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا يَفۡعَلُونَ

Na ikiwa kwa hakika tutakuonesha baadhi ya yale tunayowaahidi au tutakufisha, basi kwetu tu ndio marejeo yao, kisha Allah ni shahidi wa yale wanayoyafanya



Sura: YUNUS 

Aya : 47

وَلِكُلِّ أُمَّةٖ رَّسُولٞۖ فَإِذَا جَآءَ رَسُولُهُمۡ قُضِيَ بَيۡنَهُم بِٱلۡقِسۡطِ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Na kila umma una Mtume (wake). Basi anapofika Mtume wao watahukumiwa baina yao kwa uadilifu nao hawatadhulumiwa



Sura: YUNUS 

Aya : 48

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا ٱلۡوَعۡدُ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Na (makafiri) wanasema: Ni lini (itatokea) hii ahadi kama nyinyi ni wakweli?



Sura: YUNUS 

Aya : 49

قُل لَّآ أَمۡلِكُ لِنَفۡسِي ضَرّٗا وَلَا نَفۡعًا إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۗ لِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌۚ إِذَا جَآءَ أَجَلُهُمۡ فَلَا يَسۡتَـٔۡخِرُونَ سَاعَةٗ وَلَا يَسۡتَقۡدِمُونَ

Sema: Siimilikii nafsi yangu madhara wala manufaa, isipokuwa tu yale ayatakayo Allah. Kila umma una muda (wake wa kuishi). Pindi ukifika muda wao, basi hawatachelewesha saa moja wala kutanguliza



Sura: YUNUS 

Aya : 50

قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ إِنۡ أَتَىٰكُمۡ عَذَابُهُۥ بَيَٰتًا أَوۡ نَهَارٗا مَّاذَا يَسۡتَعۡجِلُ مِنۡهُ ٱلۡمُجۡرِمُونَ

Sema: Mnaonaje kama itakufikieni adhabu yake usiku au mchana, hivi ni kitu gani wanachokiharakia waovu?



Sura: YUNUS 

Aya : 51

أَثُمَّ إِذَا مَا وَقَعَ ءَامَنتُم بِهِۦٓۚ ءَآلۡـَٰٔنَ وَقَدۡ كُنتُم بِهِۦ تَسۡتَعۡجِلُونَ

Hivi hapo ikishatokea ndio mnaiamini? Je, hivi sasa (ndio mnaamini) na ilhali mlikuwa mkiitaka kwa haraka?



Sura: YUNUS 

Aya : 52

ثُمَّ قِيلَ لِلَّذِينَ ظَلَمُواْ ذُوقُواْ عَذَابَ ٱلۡخُلۡدِ هَلۡ تُجۡزَوۡنَ إِلَّا بِمَا كُنتُمۡ تَكۡسِبُونَ

Kisha waliodhulumu wataambiwa: “Onjeni adhabu ya milele. Hamtalipwa isipokuwa tu yale mliyokuwa mkiyachuma



Sura: YUNUS 

Aya : 53

۞وَيَسۡتَنۢبِـُٔونَكَ أَحَقٌّ هُوَۖ قُلۡ إِي وَرَبِّيٓ إِنَّهُۥ لَحَقّٞۖ وَمَآ أَنتُم بِمُعۡجِزِينَ

Na wanataka uwaeleze: Je, ni kweli hayo (unayowaambia)? Sema: Ndio! Ninaapa kwa Mola wangu Mlezi kwamba, kwa hakika kabisa, hayo ni kweli, na ninyi si wenye kushinda!



Sura: YUNUS 

Aya : 54

وَلَوۡ أَنَّ لِكُلِّ نَفۡسٖ ظَلَمَتۡ مَا فِي ٱلۡأَرۡضِ لَٱفۡتَدَتۡ بِهِۦۗ وَأَسَرُّواْ ٱلنَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُاْ ٱلۡعَذَابَۖ وَقُضِيَ بَيۡنَهُم بِٱلۡقِسۡطِ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ

Na lau kama kila nafsi iliyodhu-lumu ingekuwa inamiliki vyote vilivyomo duniani, bila shaka yoyote ingevitoa fidia (ili kujikomboa isiadhibiwe). Na watakapoiona adhabu wataficha majuto na patahu-kumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatadhulumiwa



Sura: YUNUS 

Aya : 55

أَلَآ إِنَّ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ أَلَآ إِنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٞ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ

Zindukeni: Bila ya shaka, ni vya Allah tu vyote vilivyomo mbinguni na ardhini. Zindukeni: Hakika, ahadi ya Allah ni kweli, na lakini wengi wao sana hawajui



Sura: YUNUS 

Aya : 56

هُوَ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ

Yeye (Allah) anahuisha na anafisha, na kwake tu mtarejeshwa



Sura: YUNUS 

Aya : 57

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدۡ جَآءَتۡكُم مَّوۡعِظَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَشِفَآءٞ لِّمَا فِي ٱلصُّدُورِ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٞ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ

Enyi watu, hakika yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi na ponyo (dawa) ya (maradhi) yaliyomo vifuani (mwenu) na muongozo na rehema kwa Waumini



Sura: YUNUS 

Aya : 58

قُلۡ بِفَضۡلِ ٱللَّهِ وَبِرَحۡمَتِهِۦ فَبِذَٰلِكَ فَلۡيَفۡرَحُواْ هُوَ خَيۡرٞ مِّمَّا يَجۡمَعُونَ

Sema: Fadhila za Allah na rehema zake, basi wafurahie hayo. Hilo ni bora zaidi kwao kuliko wanavyovikusanya



Sura: YUNUS 

Aya : 59

قُلۡ أَرَءَيۡتُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ لَكُم مِّن رِّزۡقٖ فَجَعَلۡتُم مِّنۡهُ حَرَامٗا وَحَلَٰلٗا قُلۡ ءَآللَّهُ أَذِنَ لَكُمۡۖ أَمۡ عَلَى ٱللَّهِ تَفۡتَرُونَ

Sema: Hivi mwaonaje, zile riziki alizokuteremshieni Allah na mkafanya baadhi yake haramu na (nyingine) halali, sema (uwaulize): Hivi Allah, amekuruhusuni (hayo) au mnamzulia Allah tu uongo?



Sura: YUNUS 

Aya : 60

وَمَا ظَنُّ ٱلَّذِينَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَذُو فَضۡلٍ عَلَى ٱلنَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَشۡكُرُونَ

Na ni ipi dhana ya wanaomzushia Allah uongo Siku ya Kiyama? (Wanadhani hali yao itakuwaje siku hiyo?). Hakika kabisa, Allah ndiye mwenye fadhila kwa watu, na lakini wengi wao sana hawashukuru