Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 1

ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلَّذِي خَلَقَ

Soma kwa jina la Mola wako Mlezi ambaye ameumba



Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 2

خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِنۡ عَلَقٍ

Amemuumba binaadamu kwa tone la damu



Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 3

ٱقۡرَأۡ وَرَبُّكَ ٱلۡأَكۡرَمُ

Soma! Na Mola wako Mlezi ni Mkarimu kushinda wote!



Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 4

ٱلَّذِي عَلَّمَ بِٱلۡقَلَمِ

Ambaye amefundisha kwa kalamu



Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 5

عَلَّمَ ٱلۡإِنسَٰنَ مَا لَمۡ يَعۡلَمۡ

Kamfundisha mtu aliyokuwa hayajui



Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 6

كَلَّآ إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لَيَطۡغَىٰٓ

Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri



Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 7

أَن رَّءَاهُ ٱسۡتَغۡنَىٰٓ

Akijiona katajirika



Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 8

إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلرُّجۡعَىٰٓ

Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo



Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 9

أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي يَنۡهَىٰ

Umemwona yule anaye mkataza



Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 10

عَبۡدًا إِذَا صَلَّىٰٓ

Mja anapo sali?



Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 11

أَرَءَيۡتَ إِن كَانَ عَلَى ٱلۡهُدَىٰٓ

Waonaje kama yeye yuko juu ya uwongofu?



Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 12

أَوۡ أَمَرَ بِٱلتَّقۡوَىٰٓ

Au anaamrisha ucha Mungu?



Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 13

أَرَءَيۡتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰٓ

Waonaje kama yeye akikanusha na akarudi nyuma?



Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 14

أَلَمۡ يَعۡلَم بِأَنَّ ٱللَّهَ يَرَىٰ

Hajui ya kwamba Allah anaona?



Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 15

كَلَّا لَئِن لَّمۡ يَنتَهِ لَنَسۡفَعَۢا بِٱلنَّاصِيَةِ

Si hivyo! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele (nywele za mbele)!



Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 16

نَاصِيَةٖ كَٰذِبَةٍ خَاطِئَةٖ

Shungi la uwongo, lenye makosa!



Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 17

فَلۡيَدۡعُ نَادِيَهُۥ

Basi na awaite wenzake!



Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 18

سَنَدۡعُ ٱلزَّبَانِيَةَ

Nasi tutawaita Mazabania!



Sura: AL-A’LAQ 

Aya : 19

كَلَّا لَا تُطِعۡهُ وَٱسۡجُدۡۤ وَٱقۡتَرِب۩

Hasha! Usimtii! Nawe sujudu na ujongee!