Sura: ATTIIN 

Aya : 1

وَٱلتِّينِ وَٱلزَّيۡتُونِ

Naapa kwa tini na zaituni



Sura: ATTIIN 

Aya : 2

وَطُورِ سِينِينَ

Na Mlima wa Sinai



Sura: ATTIIN 

Aya : 3

وَهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ ٱلۡأَمِينِ

Na mji huu (wa Makka) wenye amani



Sura: ATTIIN 

Aya : 4

لَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ فِيٓ أَحۡسَنِ تَقۡوِيمٖ

Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa



Sura: ATTIIN 

Aya : 5

ثُمَّ رَدَدۡنَٰهُ أَسۡفَلَ سَٰفِلِينَ

Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini!



Sura: ATTIIN 

Aya : 6

إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ فَلَهُمۡ أَجۡرٌ غَيۡرُ مَمۡنُونٖ

Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha



Sura: ATTIIN 

Aya : 7

فَمَا يُكَذِّبُكَ بَعۡدُ بِٱلدِّينِ

Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo?



Sura: ATTIIN 

Aya : 8

أَلَيۡسَ ٱللَّهُ بِأَحۡكَمِ ٱلۡحَٰكِمِينَ

Kwani Allah si muadilifu kuliko mahakimu wote?