وَٱلشَّمۡسِ وَضُحَىٰهَا
Naapa kwa jua na mwangaza wake!
Tarayya :
وَٱلۡقَمَرِ إِذَا تَلَىٰهَا
Na kwa mwezi unapo lifuatia!
وَٱلنَّهَارِ إِذَا جَلَّىٰهَا
Na kwa mchana unapo lidhihirisha!
وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَغۡشَىٰهَا
Na kwa usiku unapo lifunika!
وَٱلسَّمَآءِ وَمَا بَنَىٰهَا
Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga!
وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا طَحَىٰهَا
Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza!
وَنَفۡسٖ وَمَا سَوَّىٰهَا
Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza!
فَأَلۡهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقۡوَىٰهَا
Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake,
قَدۡ أَفۡلَحَ مَن زَكَّىٰهَا
Hakika amefanikiwa aliye itakasa,
وَقَدۡ خَابَ مَن دَسَّىٰهَا
Na hakika amepata hasara aliye iviza (ichafua)
كَذَّبَتۡ ثَمُودُ بِطَغۡوَىٰهَآ
Kina Thamudi walikadhibisha kwasababu ya upotofu wao,
إِذِ ٱنۢبَعَثَ أَشۡقَىٰهَا
Alipo simama mwovu wao mkubwa
فَقَالَ لَهُمۡ رَسُولُ ٱللَّهِ نَاقَةَ ٱللَّهِ وَسُقۡيَٰهَا
Hapo Mtume wa Allah alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Allah, mwacheni anywe maji fungu lake
فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمۡدَمَ عَلَيۡهِمۡ رَبُّهُم بِذَنۢبِهِمۡ فَسَوَّىٰهَا
Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwahivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwasababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa
وَلَا يَخَافُ عُقۡبَٰهَا
Wala Yeye haogopi matokeo yake