Sura: ATTAARIQ 

Aya : 1

وَٱلسَّمَآءِ وَٱلطَّارِقِ

Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku!



Sura: ATTAARIQ 

Aya : 2

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلطَّارِقُ

Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinachokuja usiku?



Sura: ATTAARIQ 

Aya : 3

ٱلنَّجۡمُ ٱلثَّاقِبُ

Ni Nyota yenye mwanga mkali



Sura: ATTAARIQ 

Aya : 4

إِن كُلُّ نَفۡسٖ لَّمَّا عَلَيۡهَا حَافِظٞ

Hapana nafsi ila inayo mwangalizi



Sura: ATTAARIQ 

Aya : 5

فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَٰنُ مِمَّ خُلِقَ

Hebu na ajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani?



Sura: ATTAARIQ 

Aya : 6

خُلِقَ مِن مَّآءٖ دَافِقٖ

Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa,



Sura: ATTAARIQ 

Aya : 7

يَخۡرُجُ مِنۢ بَيۡنِ ٱلصُّلۡبِ وَٱلتَّرَآئِبِ

Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu



Sura: ATTAARIQ 

Aya : 8

إِنَّهُۥ عَلَىٰ رَجۡعِهِۦ لَقَادِرٞ

Hakika Yeye ana uwezo wa kumrudisha



Sura: ATTAARIQ 

Aya : 9

يَوۡمَ تُبۡلَى ٱلسَّرَآئِرُ

Siku zitakapo dhihirishwa siri



Sura: ATTAARIQ 

Aya : 10

فَمَا لَهُۥ مِن قُوَّةٖ وَلَا نَاصِرٖ

Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi



Sura: ATTAARIQ 

Aya : 11

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلرَّجۡعِ

Naapa kwa mbingu yenye marejeo!



Sura: ATTAARIQ 

Aya : 12

وَٱلۡأَرۡضِ ذَاتِ ٱلصَّدۡعِ

Na kwa ardhi inayo pasuka!



Sura: ATTAARIQ 

Aya : 13

إِنَّهُۥ لَقَوۡلٞ فَصۡلٞ

Hakika hii ni kauli ya kupambanua



Sura: ATTAARIQ 

Aya : 14

وَمَا هُوَ بِٱلۡهَزۡلِ

Wala si mzaha



Sura: ATTAARIQ 

Aya : 15

إِنَّهُمۡ يَكِيدُونَ كَيۡدٗا

Hakika wao wanapanga mpango



Sura: ATTAARIQ 

Aya : 16

وَأَكِيدُ كَيۡدٗا

Na Mimi napanga mpango



Sura: ATTAARIQ 

Aya : 17

فَمَهِّلِ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَمۡهِلۡهُمۡ رُوَيۡدَۢا

Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole