إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنشَقَّتۡ
Itapo chanika mbingu,
Tarayya :
وَأَذِنَتۡ لِرَبِّهَا وَحُقَّتۡ
Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapaswa kumsikiliza,
وَإِذَا ٱلۡأَرۡضُ مُدَّتۡ
Na ardhi itakapo tanuliwa,
وَأَلۡقَتۡ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتۡ
Na kuvitoa vilivyokuwa ndani yake, ikawa tupu,
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلۡإِنسَٰنُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدۡحٗا فَمُلَٰقِيهِ
Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta
فَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ
Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia,
فَسَوۡفَ يُحَاسَبُ حِسَابٗا يَسِيرٗا
Basi huyo atahesabiwa hisabu nyepesi,
وَيَنقَلِبُ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ مَسۡرُورٗا
Na arudi kwa watu wake na furaha
وَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ وَرَآءَ ظَهۡرِهِۦ
Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake,
فَسَوۡفَ يَدۡعُواْ ثُبُورٗا
Basi huyo ataomba kuteketea
وَيَصۡلَىٰ سَعِيرًا
Na ataingia Motoni
إِنَّهُۥ كَانَ فِيٓ أَهۡلِهِۦ مَسۡرُورًا
Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake
إِنَّهُۥ ظَنَّ أَن لَّن يَحُورَ
Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena
بَلَىٰٓۚ إِنَّ رَبَّهُۥ كَانَ بِهِۦ بَصِيرٗا
Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona!
فَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلشَّفَقِ
Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa,
وَٱلَّيۡلِ وَمَا وَسَقَ
Na kwa usiku na unavyo vikusanya,
وَٱلۡقَمَرِ إِذَا ٱتَّسَقَ
Na kwa mwezi unapo pevuka,
لَتَرۡكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٖ
Lazima mtapanda tabaka kwa tabaka!
فَمَا لَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ
Basi wana nini hawaamini?
وَإِذَا قُرِئَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡقُرۡءَانُ لَا يَسۡجُدُونَۤ۩
Na wanapo somewa Qur’ani hawasujudu?
بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُكَذِّبُونَ
Bali walio kufuru wanakanusha tu
وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا يُوعُونَ
Na Allah anajua wanayo yadhamiria
فَبَشِّرۡهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ
Basi wabashirie adhabu chungu!
إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ لَهُمۡ أَجۡرٌ غَيۡرُ مَمۡنُونِۭ
Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika