إِذَا ٱلشَّمۡسُ كُوِّرَتۡ
Jua litakapokunjwa kunjwa (na kupotea mwanga wake)
Tarayya :
وَإِذَا ٱلنُّجُومُ ٱنكَدَرَتۡ
Na nyota zitikapotiwa giza (zitakapozimwa nuru yake)
وَإِذَا ٱلۡجِبَالُ سُيِّرَتۡ
Na milima itakapoendeshwa (itakapondolewa)
وَإِذَا ٱلۡعِشَارُ عُطِّلَتۡ
Na ngamia wenye mimba pevu watakapotelekezwa
وَإِذَا ٱلۡوُحُوشُ حُشِرَتۡ
Na wanyama wa mwituni watakapokusanywa
وَإِذَا ٱلۡبِحَارُ سُجِّرَتۡ
Na bahari zitakapowashwa moto
وَإِذَا ٱلنُّفُوسُ زُوِّجَتۡ
Na roho zitakapounganishwa na viwiliwili vyao
وَإِذَا ٱلۡمَوۡءُۥدَةُ سُئِلَتۡ
Na mtoto wa kike aliyezikwa akiwa hai atakapoulizwa
بِأَيِّ ذَنۢبٖ قُتِلَتۡ
Ameuawa kosa gani?
وَإِذَا ٱلصُّحُفُ نُشِرَتۡ
Na sahifa (kurasa) za kurekodi (matendo ya waja) zitakapo kunjuliwa, [wakati wa kuhesabiwa watu]
وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ كُشِطَتۡ
Na mbingu itapo ondoshwa pahala pake
وَإِذَا ٱلۡجَحِيمُ سُعِّرَتۡ
Na Jahannamu itakapo chochewa
وَإِذَا ٱلۡجَنَّةُ أُزۡلِفَتۡ
Na Pepo ikasogezwa karibu
عَلِمَتۡ نَفۡسٞ مَّآ أَحۡضَرَتۡ
Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha
فَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلۡخُنَّسِ
Basi Naapa kwa sayari zinapo rejea nyuma, zinazotoweka (mchana na zinadhihirika usiku)
ٱلۡجَوَارِ ٱلۡكُنَّسِ
Zinazotembea na kujificha
وَٱلَّيۡلِ إِذَا عَسۡعَسَ
Na naapa kwa usiku unapo pungua giza lake
وَٱلصُّبۡحِ إِذَا تَنَفَّسَ
Na Naapa kwa asubuhi inapo pambazuka
إِنَّهُۥ لَقَوۡلُ رَسُولٖ كَرِيمٖ
Hakika hii (Qurani) bila shaka ni kauli (ameifikisha) Mjumbe mtukufu (Jibrili)
ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي ٱلۡعَرۡشِ مَكِينٖ
Mwenye nguvu na cheo kitukufu kwa (Allah) Anayemiliki ‘Arsh. [Kiti cha Enzi]
مُّطَاعٖ ثَمَّ أَمِينٖ
Anayetiiwa (na Malaika), mwaminifu huko (mbinguni)
وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجۡنُونٖ
Na wala huyu mwenzenu hana wazimu
وَلَقَدۡ رَءَاهُ بِٱلۡأُفُقِ ٱلۡمُبِينِ
Na hakika yeye alimwona [Jibrili] kwenye upeo wa macho ulio safi
وَمَا هُوَ عَلَى ٱلۡغَيۡبِ بِضَنِينٖ
Wala yeye si bakhili kwa [kuelezea mambo ya] ghaibu
وَمَا هُوَ بِقَوۡلِ شَيۡطَٰنٖ رَّجِيمٖ
Na hii (Qurani) si kauli ya shetani aliye fukuzwa kutoka kwenye rehema za Allah
فَأَيۡنَ تَذۡهَبُونَ
Basi mnakwenda wapi?
إِنۡ هُوَ إِلَّا ذِكۡرٞ لِّلۡعَٰلَمِينَ
Hii (Qurani) haikuwa isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu wote
لِمَن شَآءَ مِنكُمۡ أَن يَسۡتَقِيمَ
Kwa yule anaye taka miongoni mwenu kwenda sawa
وَمَا تَشَآءُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Allah Mola wa Walimwengu wote