وَٱلذَّـٰرِيَٰتِ ذَرۡوٗا
Ninaapa kwa upepo (mkali) unaopeperusha (kila kitu)
Tarayya :
فَٱلۡحَٰمِلَٰتِ وِقۡرٗا
Kisha (ninaapa) wa vile vibebavyo uzito (ikiwa ni pamoja na mawingu yanayobeba maji ya mvua)
فَٱلۡجَٰرِيَٰتِ يُسۡرٗا
Kisha (ninaapa) kwa (majahazi na vyombo vingine vizito vya majini) yenye kutembea (juu ya maji) kwa wepesi
فَٱلۡمُقَسِّمَٰتِ أَمۡرًا
Kisha (ninaapa) kwa (Malaika) wanaogawa mambo (majukumu waliyopewa na Allah)
إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٞ
(Kwamba) Hakika ilivyo ni kwamba, mnachoahidiwa ni kweli kabisa
وَإِنَّ ٱلدِّينَ لَوَٰقِعٞ
Na Hakika, malipo (Siku ya Kiyama) kwa yakini kabisa yatakuwepo
وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلۡحُبُكِ
Nina apa kwa mbingu yenye njia
إِنَّكُمۡ لَفِي قَوۡلٖ مُّخۡتَلِفٖ
(Kwamba) Hakika, nyinyi mmo katika zinazotofautiana.[1]
1- - Mara mseme Muhammad ni muongo, mara mchawi n.k.
يُؤۡفَكُ عَنۡهُ مَنۡ أُفِكَ
Huondolewa Humo Yule Anaye-ondolewa
قُتِلَ ٱلۡخَرَّـٰصُونَ
Wamelaaniwa Wakadhibishaji
ٱلَّذِينَ هُمۡ فِي غَمۡرَةٖ سَاهُونَ
Wale Ambao Wamezama Katika Ujinga Hali Ya Kujisahau
يَسۡـَٔلُونَ أَيَّانَ يَوۡمُ ٱلدِّينِ
Wanauliza Ni Lini Hiyo Siku Ya Malipo
يَوۡمَ هُمۡ عَلَى ٱلنَّارِ يُفۡتَنُونَ
Siku Hiyo Wao Katika Moto Watachomwa
ذُوقُواْ فِتۡنَتَكُمۡ هَٰذَا ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تَسۡتَعۡجِلُونَ
Onjeni Adhabu Yenu Hii Ambayo Mlikua Kwayo Mnaiharakisha
إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّـٰتٖ وَعُيُونٍ
Hakika Ya Wachamungu Watakua Ndani Ya Pepo Na Chemchem
ءَاخِذِينَ مَآ ءَاتَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُحۡسِنِينَ
Hali Wakichukua Yale Ambayo Aliyowapa Wao Bwana Wao Hakika Wao Walikua Kabla Ya Haya wakifanya mema
كَانُواْ قَلِيلٗا مِّنَ ٱلَّيۡلِ مَا يَهۡجَعُونَ
Walikuwa Sehemu Ndogo Ya Usiku Wanalala
وَبِٱلۡأَسۡحَارِ هُمۡ يَسۡتَغۡفِرُونَ
Na Usiku Wa Manane (Kabla ya Alfajiri) Wanafanya Istighifari
وَفِيٓ أَمۡوَٰلِهِمۡ حَقّٞ لِّلسَّآئِلِ وَٱلۡمَحۡرُومِ
Na Katika Mali Zao Kuna Fungu Kwa Ajili Ya Mwenye Kuomba Na Asiye omba
وَفِي ٱلۡأَرۡضِ ءَايَٰتٞ لِّلۡمُوقِنِينَ
Na Katika Ardhi Kuna Ishara Nyingi Kwa Walio Na Yakini
وَفِيٓ أَنفُسِكُمۡۚ أَفَلَا تُبۡصِرُونَ
Na Katika Nafsi Zenu Hivi Hamuoni?
وَفِي ٱلسَّمَآءِ رِزۡقُكُمۡ وَمَا تُوعَدُونَ
Na Katika Mbingu Rizki Yenu Na Yote Mnayoahidiwa
فَوَرَبِّ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ إِنَّهُۥ لَحَقّٞ مِّثۡلَ مَآ أَنَّكُمۡ تَنطِقُونَ
Naapa Kwa Bwana Wa Mbingu Na Ardhi Hakika Hilo Ni Haki Kama Ambavyo Nyinyi Mnavyotamka
هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ضَيۡفِ إِبۡرَٰهِيمَ ٱلۡمُكۡرَمِينَ
Je Imewafikia Habari Za Wageni Wa Ibrahimu Walio Wema (wanao heshimiwa?)
إِذۡ دَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَقَالُواْ سَلَٰمٗاۖ قَالَ سَلَٰمٞ قَوۡمٞ مُّنكَرُونَ
Pale Walipoingia Kwake Wakasema Salama, Akasema Salama nyinyi ni Watu nisio kujueni
فَرَاغَ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ فَجَآءَ بِعِجۡلٖ سَمِينٖ
Akaenda Kwa Ahli Yake Na Akaja Na Nyama Ya Ndama Aliye nona
فَقَرَّبَهُۥٓ إِلَيۡهِمۡ قَالَ أَلَا تَأۡكُلُونَ
Akawakaribisha na akasema Mbona Hamli?
فَأَوۡجَسَ مِنۡهُمۡ خِيفَةٗۖ قَالُواْ لَا تَخَفۡۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَٰمٍ عَلِيمٖ
Akahisi Kuwaogopa katika Nafsi Yake Kuhusu Wao, Wakasema Usiogope Na Wakampa Bishara Kwa Kijana mwenye elimu
فَأَقۡبَلَتِ ٱمۡرَأَتُهُۥ فِي صَرَّةٖ فَصَكَّتۡ وَجۡهَهَا وَقَالَتۡ عَجُوزٌ عَقِيمٞ
Ndipo Mkewe akawaelekea na huku akisema Hali Ya kupiga Kelele Na Kujipigapiga Usoni (kwa kustaajabu) Na Akasema Kikongwe Tasa!!
قَالُواْ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡعَلِيمُ
Wakasema Hivyo Ndivyo Alivyosema Bwana Wako Hakika Yeye Ni Mwingi Wa Hekima Na Mjuzi