Sura: AL-MAIDA 

Aya : 1

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَوۡفُواْ بِٱلۡعُقُودِۚ أُحِلَّتۡ لَكُم بَهِيمَةُ ٱلۡأَنۡعَٰمِ إِلَّا مَا يُتۡلَىٰ عَلَيۡكُمۡ غَيۡرَ مُحِلِّي ٱلصَّيۡدِ وَأَنتُمۡ حُرُمٌۗ إِنَّ ٱللَّهَ يَحۡكُمُ مَا يُرِيدُ

Enyi mlioamini, tekelezeni makubaliano[1]. Mmehalalishiwa (kula) wanyama howa[2] (wafugwao), isipokuwa tu wale (wanyama) mnaosomewa (kwenye Qur’ani na Suna kuwa ni haramu) bila ya kuhalalisha kuwinda mkiwa katika Ihramu (utekelezaji wa ibada ya Hija au Umrah). Hakika, Allah anahukumu atakayo


1- - Allah anatuamrisha kutekeleza, makubaliano na mikataba.


2- - Wanyama howa ni ngamia, ng’ombe, kondoo na mbuzi.


Sura: AL-MAIDA 

Aya : 2

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تُحِلُّواْ شَعَـٰٓئِرَ ٱللَّهِ وَلَا ٱلشَّهۡرَ ٱلۡحَرَامَ وَلَا ٱلۡهَدۡيَ وَلَا ٱلۡقَلَـٰٓئِدَ وَلَآ ءَآمِّينَ ٱلۡبَيۡتَ ٱلۡحَرَامَ يَبۡتَغُونَ فَضۡلٗا مِّن رَّبِّهِمۡ وَرِضۡوَٰنٗاۚ وَإِذَا حَلَلۡتُمۡ فَٱصۡطَادُواْۚ وَلَا يَجۡرِمَنَّكُمۡ شَنَـَٔانُ قَوۡمٍ أَن صَدُّوكُمۡ عَنِ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ أَن تَعۡتَدُواْۘ وَتَعَاوَنُواْ عَلَى ٱلۡبِرِّ وَٱلتَّقۡوَىٰۖ وَلَا تَعَاوَنُواْ عَلَى ٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡعُدۡوَٰنِۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۖ إِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ

Enyi mlioamini, msizivunjie heshima alama za (dini) ya Allah[1] wala Miezi Mitukufu[2] wala Hadiy[3] wala vigwe[4], wala wakusudiao Nyumba Takatifu[5] wakitafuta fadhila na radhi za Mola wao. Na mkishatoka (katika Ibada ya Hija au Umrah) basi windeni (mkitaka kufanya hivyo). Na wala kule kuwachukia watu kwa kuwa walikuzuieni kufika Msikiti Mtukufu kusikupelekeeni kuwafanyia uadui (wa kuwaua na mfano wa hilo). Na saidianeni katika wema na ucha Mungu, na msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Allah. Hakika, Allah ni Mkali sana wa kuadhibu


1- - Alama za dini ya Allah ni zile ibada kubwa kama Hija, Umra, Swala, Funga n.k.


2- - Miezi Mitukufu ni minne: Dhul-qaada, Dhulhija, Muharram na Rajab.


3- - Hadiyu ni wanyama wanaopelekwa Makka kwa kuchinjwa katika ibada ya Hija.


4- - Vigwe ni kamba za utambulisho anayofungwa mnyama shingoni ili kumtambulisha kuwa anapelekwa Makkah kwa kuchinjwa katika ibada ya Hija.


5- - Hawa ni wale Waislamu wanaokwenda Makka kwa makusudi ya kufanya ibada ya Hija au Umra.


Sura: AL-MAIDA 

Aya : 3

حُرِّمَتۡ عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَيۡتَةُ وَٱلدَّمُ وَلَحۡمُ ٱلۡخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ لِغَيۡرِ ٱللَّهِ بِهِۦ وَٱلۡمُنۡخَنِقَةُ وَٱلۡمَوۡقُوذَةُ وَٱلۡمُتَرَدِّيَةُ وَٱلنَّطِيحَةُ وَمَآ أَكَلَ ٱلسَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيۡتُمۡ وَمَا ذُبِحَ عَلَى ٱلنُّصُبِ وَأَن تَسۡتَقۡسِمُواْ بِٱلۡأَزۡلَٰمِۚ ذَٰلِكُمۡ فِسۡقٌۗ ٱلۡيَوۡمَ يَئِسَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن دِينِكُمۡ فَلَا تَخۡشَوۡهُمۡ وَٱخۡشَوۡنِۚ ٱلۡيَوۡمَ أَكۡمَلۡتُ لَكُمۡ دِينَكُمۡ وَأَتۡمَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ نِعۡمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ ٱلۡإِسۡلَٰمَ دِينٗاۚ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ فِي مَخۡمَصَةٍ غَيۡرَ مُتَجَانِفٖ لِّإِثۡمٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Mmeharamishiwa (kula) mzoga[1] na damu na nyama ya nguruwe na (mnyama) aliyechinjwa pasina (kutajwa jina la) Allah na (mnyama) aliyekufa kwa kusongeka koo (kujinyonga) na aliyekufa kwa kupigwa na aliyekufa kwa kuporomoka na aliyekufa kwa kupigwa pembe (na mwenzake) na aliyeliwa (kwa kushambuliwa) na mnyama mkali ila (mliyemuwahi akiwa hai) mkamchinja. Na (pia mmeharamishiwa kula nyama ya mnyama) aliyechinjwa katika (sehem yalipo) masanamu.[2] Na (mmeharamishiwa) kutaka kujua mambo yaliyopangwa (na Allah ikiwemo kupiga ramli na mfano wa hilo) kwa kutumia mbao. Ilivyo ni kwamba hayo (yote) ni uovu. Leo waliokufuru wameikatia tamaa dini yenu, basi msiwaogope (isipokuwa) niogopeni Mimi. Leo nimekukamilishieni dini yenu na kukutimizieni neema yangu na nimeuchagua Uislamu uwe dini yenu. Na mwenye kushikwa na dhiki ya njaa kali pasipo na kukusudia dhambi (anaruhusiwa kula hivyo vilivyoharamishwa kwa sababu) hakika, Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa huruma


1- - Mzoga ni mnyama aliyekufa mwenyewe au amechinjwa bila ya kufuata taratibu za sheria ya Kiislamu; kibudu, nyamafu.


2- - Mnyama aliyechinjwa katika sehemu za masanamu, mizimu, makaburini nk. Ni haramu kula nyama yake.


Sura: AL-MAIDA 

Aya : 4

يَسۡـَٔلُونَكَ مَاذَآ أُحِلَّ لَهُمۡۖ قُلۡ أُحِلَّ لَكُمُ ٱلطَّيِّبَٰتُ وَمَا عَلَّمۡتُم مِّنَ ٱلۡجَوَارِحِ مُكَلِّبِينَ تُعَلِّمُونَهُنَّ مِمَّا عَلَّمَكُمُ ٱللَّهُۖ فَكُلُواْ مِمَّآ أَمۡسَكۡنَ عَلَيۡكُمۡ وَٱذۡكُرُواْ ٱسۡمَ ٱللَّهِ عَلَيۡهِۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلۡحِسَابِ

Wanakuuliza: Wamehalalishiwa (kula) nini? Sema: Mmehalalishiwa (kula) vilivyo vizuri (ambavyo havikukatazwa) na mlichowafunza Wanyama na ndege wakali (kukiwinda) mkiwa mmewafunza aliyokufunzeni Allah (taratibu za kuwinda). Basi kuleni kile walichokukamatieni. Na tajeni jina la Allah juu ya hilo (la mnapowatuma wanyama wa kuwinda). Na muogopeni Allah. Hakika, Allah ni Mwepesi sana wa kuhesabu



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 5

ٱلۡيَوۡمَ أُحِلَّ لَكُمُ ٱلطَّيِّبَٰتُۖ وَطَعَامُ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ حِلّٞ لَّكُمۡ وَطَعَامُكُمۡ حِلّٞ لَّهُمۡۖ وَٱلۡمُحۡصَنَٰتُ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ وَٱلۡمُحۡصَنَٰتُ مِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِكُمۡ إِذَآ ءَاتَيۡتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحۡصِنِينَ غَيۡرَ مُسَٰفِحِينَ وَلَا مُتَّخِذِيٓ أَخۡدَانٖۗ وَمَن يَكۡفُرۡ بِٱلۡإِيمَٰنِ فَقَدۡ حَبِطَ عَمَلُهُۥ وَهُوَ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ

Leo mmehalalishiwa vilivyo vizuri. Na chakula cha waliopewa Kitabu ni halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao. Na (mmehalalishiwa kuoa) wanawake waumini waliohifadhiwa na wanawake waliohifadhiwa katika waliopewa Kitabu kabla yenu mtakapowapa malipo (mahari) yao, mkikusudia kujihifadhi (na) sio wenye kukusudia uzinzi wala kuwaweka (wanawake hao) kinyumba. Na yeyote anayekataa kuamini, bila shaka amali zake (njema) zimeporomoka (zimepotea bure) na yeye Akhera atakuwa miongoni mwa wenye hasara



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 6

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا قُمۡتُمۡ إِلَى ٱلصَّلَوٰةِ فَٱغۡسِلُواْ وُجُوهَكُمۡ وَأَيۡدِيَكُمۡ إِلَى ٱلۡمَرَافِقِ وَٱمۡسَحُواْ بِرُءُوسِكُمۡ وَأَرۡجُلَكُمۡ إِلَى ٱلۡكَعۡبَيۡنِۚ وَإِن كُنتُمۡ جُنُبٗا فَٱطَّهَّرُواْۚ وَإِن كُنتُم مَّرۡضَىٰٓ أَوۡ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوۡ جَآءَ أَحَدٞ مِّنكُم مِّنَ ٱلۡغَآئِطِ أَوۡ لَٰمَسۡتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَلَمۡ تَجِدُواْ مَآءٗ فَتَيَمَّمُواْ صَعِيدٗا طَيِّبٗا فَٱمۡسَحُواْ بِوُجُوهِكُمۡ وَأَيۡدِيكُم مِّنۡهُۚ مَا يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيَجۡعَلَ عَلَيۡكُم مِّنۡ حَرَجٖ وَلَٰكِن يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمۡ وَلِيُتِمَّ نِعۡمَتَهُۥ عَلَيۡكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ

Enyi mlioamini, mnaposimama kwenda kuswali[1], basi (tawadheni) osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka viwikoni na pakeni (maji) vichwa vyenu na (osheni) miguu yenu mpaka vifundoni[2]. Na mkiwa wenye Janaba basi jitwaharisheni (kwa kuoga au kutayamamu ikishindikana kuoga). Na mkiwa wagonjwa au mpo safarini au mmoja wenu ametoka msalani au mmegusana (mmejamiiana) na wanawake (wake zenu)[3] na hamkupata maji, basi tayamamuni (kusudieni) mchanga ulio safi[4] na mpake nyuso zenu na mikono yenu kwa mchanga huo[5]. Allah hataki kukuwekeeni tabu yoyote (uzito na usumbufu kwa kulazimisha kujitwaharisha kwa maji wakati maji hayapo au haiwezekani kuyatumia kwasababu ya ugonjwa au baridi kali); bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake kwenu ili mpate kushukuru.[6]


1- - Hii ina maana hata kwa anayeswali kwa kuketi au kwa kulala ujumbe na utaratibu huu unamhusu pia.


2- - Kwenye Aya hii kuna visomo vikuu viwili vinavyokubalika: “Arjulakum” kwa Nasbu. Na kisomo cha pili ni “Arjulikum” kwa Jarri. Hii inamaanisha kwamba, kwa mujibu wa Qur’an na Suna sahihi za Mtume wa Allah uoshaji wa miguu una hukumu za aina mbili: (a) Kama miguu ikiwa wazi (haijavikwa kitu) faradhi yake ni kuoshwa kwa maji. (b) Kama miguu imevikwa khofu/soksi faradhi yake ni kupakwa maji.


3- - Muradi wa kugusana hapa ni kujamiiana. Kugusana tu kwa Ngozi na Ngozi hakulazimishi kutawadha.


4- - Kitendo hiki cha kutumia mchanga ulio safi na kupaka vumbi lake usoni na mikononi kinaitwa Tayamamu katika sheria ya Kiislamu.


5- - Kwa pigo la kwanza pakeni usoni na kwa pigo la pili pakeni mikononi.


6- - Aya hapa inaonesha kuwa ni lazima Muislamu kila anapotaka kuswali atawadhe. Lakini ulazima huu ni kwa yule ambaye hana Udhu. Ama mtu mwenye Udhu halazimiki kutawadha, lakini ni jambo zuri kama
atatawadha tena.


Sura: AL-MAIDA 

Aya : 7

وَٱذۡكُرُواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَمِيثَٰقَهُ ٱلَّذِي وَاثَقَكُم بِهِۦٓ إِذۡ قُلۡتُمۡ سَمِعۡنَا وَأَطَعۡنَاۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Na kumbukeni neema za Allah kwenu (kwa kuwaongoa kuwa Waislamu) na makubaliano yake aliyoingia nanyi, pale mliposema: Tumesikia na tumetii. Na mcheni Allah. Hakika Allah mjuzi mno wa yaliyomo vifuani



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 8

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُونُواْ قَوَّـٰمِينَ لِلَّهِ شُهَدَآءَ بِٱلۡقِسۡطِۖ وَلَا يَجۡرِمَنَّكُمۡ شَنَـَٔانُ قَوۡمٍ عَلَىٰٓ أَلَّا تَعۡدِلُواْۚ ٱعۡدِلُواْ هُوَ أَقۡرَبُ لِلتَّقۡوَىٰۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ

Enyi miloamini, kuweni wasimamizi (wa haki) kwa ajili ya Allah, mtoao ushahidi kwa uadilifu. Na kuwachukia (watu) kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu (kwa watu wote). Hilo ndilo lililo karibu zaidi (kufikisha) kwenye uchamungu. Na mcheni Allah. Hakika, Allah anayajua mnayoyatenda



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 9

وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَٰتِ لَهُم مَّغۡفِرَةٞ وَأَجۡرٌ عَظِيمٞ

Allah amewaahidi walioamini na kutenda mema (kwamba) watapata msamaha na malipo makubwa sana



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 10

وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآ أُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَحِيمِ

Na waliokufuru na kuzikanusha Aya zetu (tulizoziteremsha kwa Mitume wetu), hao ndio watu wa Motoni



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 11

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ إِذۡ هَمَّ قَوۡمٌ أَن يَبۡسُطُوٓاْ إِلَيۡكُمۡ أَيۡدِيَهُمۡ فَكَفَّ أَيۡدِيَهُمۡ عَنكُمۡۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ

Enyi mlioamini, kumbukeni neema ya Allah kwenu pale watu (Makureish na Wayahudi) walipodhamiria kukunyoosheeni mikono yao (na kutaka kumuua Mtume na Swahaba) (Allah) akaizuia mikono yao isikufikieni. Na mcheni Allah. Na Allah tu wamtegemee waumini



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 12

۞وَلَقَدۡ أَخَذَ ٱللَّهُ مِيثَٰقَ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ وَبَعَثۡنَا مِنۡهُمُ ٱثۡنَيۡ عَشَرَ نَقِيبٗاۖ وَقَالَ ٱللَّهُ إِنِّي مَعَكُمۡۖ لَئِنۡ أَقَمۡتُمُ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَيۡتُمُ ٱلزَّكَوٰةَ وَءَامَنتُم بِرُسُلِي وَعَزَّرۡتُمُوهُمۡ وَأَقۡرَضۡتُمُ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنٗا لَّأُكَفِّرَنَّ عَنكُمۡ سَيِّـَٔاتِكُمۡ وَلَأُدۡخِلَنَّكُمۡ جَنَّـٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۚ فَمَن كَفَرَ بَعۡدَ ذَٰلِكَ مِنكُمۡ فَقَدۡ ضَلَّ سَوَآءَ ٱلسَّبِيلِ

Na kwa yakini kabisa, Allah alifunga ahadi na Wana wa Israil, na tukatuma miongoni mwao viongozi kumi na mbili (ili wawafundishe utekelezaji wa ahadi hiyo ya Allah) na Allah akasema: Kwa yakini mimi niko pamoja nanyi. Kwa yakini kabisa, kama mkisimamisha Swala na mkitoa Zaka na mkiwaamini Mitume wangu na mkiwapa nguvu (mkiwaunga mkono) na mkimkopesha Allah mkopo mzuri, bila shaka yoyote nitakufutieni maovu yenu na nitakuingizeni katika Pepo zipitazo mito mbele yake. Basi atakayekufuru miongoni mwenu baada ya (makubaliano) hayo, bila shaka amepotea njia ya sawa



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 13

فَبِمَا نَقۡضِهِم مِّيثَٰقَهُمۡ لَعَنَّـٰهُمۡ وَجَعَلۡنَا قُلُوبَهُمۡ قَٰسِيَةٗۖ يُحَرِّفُونَ ٱلۡكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِۦ وَنَسُواْ حَظّٗا مِّمَّا ذُكِّرُواْ بِهِۦۚ وَلَا تَزَالُ تَطَّلِعُ عَلَىٰ خَآئِنَةٖ مِّنۡهُمۡ إِلَّا قَلِيلٗا مِّنۡهُمۡۖ فَٱعۡفُ عَنۡهُمۡ وَٱصۡفَحۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Basi kwa sababu ya kuvunja kwao makubaliano yao, tuliwalaani na kuzifanya ngumu nyoyo zao; wanayapotosha maneno ya (Allah)[1] katika mahali pake na wameacha sehemu (kubwa) ya yale waliyokumbushwa. Na bado unaendelea kupata habari za khiyana yao isipokuwa wachache miongoni mwao. Basi wasamehe na wapuuze. Hakika, Allah anawapenda wafanyao mazuri


1- - Yaliyomo katika Torati na Injili.


Sura: AL-MAIDA 

Aya : 14

وَمِنَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّا نَصَٰرَىٰٓ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَهُمۡ فَنَسُواْ حَظّٗا مِّمَّا ذُكِّرُواْ بِهِۦ فَأَغۡرَيۡنَا بَيۡنَهُمُ ٱلۡعَدَاوَةَ وَٱلۡبَغۡضَآءَ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ وَسَوۡفَ يُنَبِّئُهُمُ ٱللَّهُ بِمَا كَانُواْ يَصۡنَعُونَ

Na kwa wale waliosema: “Sisi ni Wanaswara (Wakristo)”, tulichukua ahadi yao, basi wakaacha sehemu (kubwa) ya yale waliyokumbushwa. Kwa sababu hiyo, tukawashakizia uadui baina yao na bughudha mpaka Siku ya Kiama, na punde Allah atawaambia yale waliyokuwa wanayafanya



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 15

يَـٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ قَدۡ جَآءَكُمۡ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمۡ كَثِيرٗا مِّمَّا كُنتُمۡ تُخۡفُونَ مِنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَيَعۡفُواْ عَن كَثِيرٖۚ قَدۡ جَآءَكُم مِّنَ ٱللَّهِ نُورٞ وَكِتَٰبٞ مُّبِينٞ

Enyi Watu wa Kitabu, kwa hakika kabisa, amekujieni Mtume wetu (Muhammad) akikuwekeeni wazi mengi mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu (Taurati na Injili) na akisamehe mengi. Bila shaka, imekujiieni nuru kutoka kwa Allah na Kitabu kinachobainisha



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 16

يَهۡدِي بِهِ ٱللَّهُ مَنِ ٱتَّبَعَ رِضۡوَٰنَهُۥ سُبُلَ ٱلسَّلَٰمِ وَيُخۡرِجُهُم مِّنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ بِإِذۡنِهِۦ وَيَهۡدِيهِمۡ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Kwa (Kitabu) hicho Allah anamuongoza anayefuata radhi zake katika njia za amani na anawatoa katika viza (na) kuwapeleka kwenye nuru kwa idhini yake, na anawaongoza kwenye njia iliyonyooka



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 17

لَّقَدۡ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡمَسِيحُ ٱبۡنُ مَرۡيَمَۚ قُلۡ فَمَن يَمۡلِكُ مِنَ ٱللَّهِ شَيۡـًٔا إِنۡ أَرَادَ أَن يُهۡلِكَ ٱلۡمَسِيحَ ٱبۡنَ مَرۡيَمَ وَأُمَّهُۥ وَمَن فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗاۗ وَلِلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَاۚ يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Kwa yakini kabisa, wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allah (Mungu) ndio Masihi bin Mariamu.” Sema: “Ni nani anayemiliki kuzuia jambo lolote litokalo kwa Allah akitaka kumuangamiza Masihi Mwana wa Mariamu na mama yake na wote waliomo ardhini (duniani)? Na ufalme wa mbinguni na ardhini na vilivyomo kati yake ni wa Allah (tu peke yake); anaumba atakacho. Na Allah ni Muweza wa kila kitu



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 18

وَقَالَتِ ٱلۡيَهُودُ وَٱلنَّصَٰرَىٰ نَحۡنُ أَبۡنَـٰٓؤُاْ ٱللَّهِ وَأَحِبَّـٰٓؤُهُۥۚ قُلۡ فَلِمَ يُعَذِّبُكُم بِذُنُوبِكُمۖ بَلۡ أَنتُم بَشَرٞ مِّمَّنۡ خَلَقَۚ يَغۡفِرُ لِمَن يَشَآءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَآءُۚ وَلِلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَاۖ وَإِلَيۡهِ ٱلۡمَصِيرُ

Na Wayahudi na Wanaswara (Wakristo) walisema: “Sisi ni Wana wa Allah (Mungu) na vipenzi vyake”. Sema: “Basi ni kwa nini anakuadhibuni kwa dhambi zenu? Bali nyinyi ni watu (tu) miongoni mwa (watu wengine) aliowaumba. (Allah) Anamsamehe amtakaye (anapotubu) na anamuadhibu amtakaye (asipotubu). Na ni wa Allah tu ufalme wa mbinguni na ardhini na vilivyomo baina yake, na marejeo ni kwake tu



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 19

يَـٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ قَدۡ جَآءَكُمۡ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمۡ عَلَىٰ فَتۡرَةٖ مِّنَ ٱلرُّسُلِ أَن تَقُولُواْ مَا جَآءَنَا مِنۢ بَشِيرٖ وَلَا نَذِيرٖۖ فَقَدۡ جَآءَكُم بَشِيرٞ وَنَذِيرٞۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Enyi Watu wa Kitabu, bila shaka amekujieni Mtume wetu (Muhammad), akikubainishieni (ujumbe wa Allah) katika wakati usiokuwa na Mitume, ili msije kusema: “Hakutujia mtoaji wa habari njema wala muonyaji.” Kwa hakika kabisa, amekujieni Mtoaji habari njema na Muonyaji. Na Allah ni Muweza wa kila kitu



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 20

وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِۦ يَٰقَوۡمِ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ إِذۡ جَعَلَ فِيكُمۡ أَنۢبِيَآءَ وَجَعَلَكُم مُّلُوكٗا وَءَاتَىٰكُم مَّا لَمۡ يُؤۡتِ أَحَدٗا مِّنَ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Na (kumbukeni) Musa alipowaambia watu wake: “Enyi watu wangu, kumbukeni neema za Allah kwenu; alipofanya kwenu Manabii na akakufanyeni wafalme na akakupeni (mambo) ambayo hakumpa yeyote katika walimwengu (wote wa zama zenu)



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 21

يَٰقَوۡمِ ٱدۡخُلُواْ ٱلۡأَرۡضَ ٱلۡمُقَدَّسَةَ ٱلَّتِي كَتَبَ ٱللَّهُ لَكُمۡ وَلَا تَرۡتَدُّواْ عَلَىٰٓ أَدۡبَارِكُمۡ فَتَنقَلِبُواْ خَٰسِرِينَ

“Enyi watu wangu, Ingieni katika Ardhi Takatifu (Baytulmaqdis) ambayo Allah amekuandikieni na msirudi nyuma (kupigana na Wakanani) mtakuwa wenye kula hasara (mkifanya hivyo)



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 22

قَالُواْ يَٰمُوسَىٰٓ إِنَّ فِيهَا قَوۡمٗا جَبَّارِينَ وَإِنَّا لَن نَّدۡخُلَهَا حَتَّىٰ يَخۡرُجُواْ مِنۡهَا فَإِن يَخۡرُجُواْ مِنۡهَا فَإِنَّا دَٰخِلُونَ

Wakasema: Ewe Musa, hakika humo kuna watu majabari[1], na sisi hatutaingia humo mpaka watoke humo (na watukabidhi mji kwa amani). Wakitoka humo, basi sisi bila ya shaka tutaingia


1- - Watu wenye miili mikubwa, wababe na madhalimu.


Sura: AL-MAIDA 

Aya : 23

قَالَ رَجُلَانِ مِنَ ٱلَّذِينَ يَخَافُونَ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمَا ٱدۡخُلُواْ عَلَيۡهِمُ ٱلۡبَابَ فَإِذَا دَخَلۡتُمُوهُ فَإِنَّكُمۡ غَٰلِبُونَۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَتَوَكَّلُوٓاْ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Watu wawili miongoni mwa wale waogopao (kuhalifu amri za Allah na Mtume wake) ambao Allah amewaneemesha walisema: Wavamieni kupitia kwenye huo mlango; maana mtakapowavamia (kupitia hapo mlangoni), kwa yakini nyinyi mtashinda. Na mtegemeeni Allah tu ikiwa nyinyi ni waumini



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 24

قَالُواْ يَٰمُوسَىٰٓ إِنَّا لَن نَّدۡخُلَهَآ أَبَدٗا مَّا دَامُواْ فِيهَا فَٱذۡهَبۡ أَنتَ وَرَبُّكَ فَقَٰتِلَآ إِنَّا هَٰهُنَا قَٰعِدُونَ

Wakasema: “Ewe Musa, sisi hatutaingia humo kamwe madamu wao bado wamo humo. Basi nenda wewe na Mola wako mkapigane, sisi ni wenye kuketi hapa (hatuendi kokote).”



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 25

قَالَ رَبِّ إِنِّي لَآ أَمۡلِكُ إِلَّا نَفۡسِي وَأَخِيۖ فَٱفۡرُقۡ بَيۡنَنَا وَبَيۡنَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡفَٰسِقِينَ

(Musa) Akasema: (Ewe) Mola wangu, hakika mimi similiki isipokuwa nafsi yangu na ndugu yangu; basi tutenganishe na hawa watu mafasiki (waovu)



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 26

قَالَ فَإِنَّهَا مُحَرَّمَةٌ عَلَيۡهِمۡۛ أَرۡبَعِينَ سَنَةٗۛ يَتِيهُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ فَلَا تَأۡسَ عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡفَٰسِقِينَ

(Allah) Akasema: “Basi wame-haramishiwa (ardhi) hiyo kwa muda wa miaka arobaini; wakitangatanga ardhini. Basi usiwasikitikie watu mafasiki (waovu)



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 27

۞وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ ٱبۡنَيۡ ءَادَمَ بِٱلۡحَقِّ إِذۡ قَرَّبَا قُرۡبَانٗا فَتُقُبِّلَ مِنۡ أَحَدِهِمَا وَلَمۡ يُتَقَبَّلۡ مِنَ ٱلۡأٓخَرِ قَالَ لَأَقۡتُلَنَّكَۖ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ ٱللَّهُ مِنَ ٱلۡمُتَّقِينَ

Na wasomee, kwa haki, habari za wana wawili wa Adamu walipotoa sadaka, basi ikakubaliwa ya mmoja wao, na ya mwingine haikukubaliwa. (Aliyekataliwa sadaka yake) Aka-sema: Kwa Yakini kabisa, nitakuua. (Yule aliyekubaliwa sadaka yake) Akasema: Ilivyo ni kwamba, Allah anawakubalia wacha Mungu[1]


1- - Hapa hakuyasema haya kumwambia ndugu yake kwa lengo la majigambo na majivuno. Lakini aliyasema hayo kwa lengo la kumshawishi ndugu yake aache uovu na amuelekee Allah kwa unyenyekevu ili akubaliwe ibada zake.


Sura: AL-MAIDA 

Aya : 28

لَئِنۢ بَسَطتَ إِلَيَّ يَدَكَ لِتَقۡتُلَنِي مَآ أَنَا۠ بِبَاسِطٖ يَدِيَ إِلَيۡكَ لِأَقۡتُلَكَۖ إِنِّيٓ أَخَافُ ٱللَّهَ رَبَّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Ukininyooshea mkono wako ili kuniua, mimi sitakunyooshea mkono wangu nikuue. Kwa hakika, mimi ninamuogopa Allah, Mola wa walimwengu wote



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 29

إِنِّيٓ أُرِيدُ أَن تَبُوٓأَ بِإِثۡمِي وَإِثۡمِكَ فَتَكُونَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلنَّارِۚ وَذَٰلِكَ جَزَـٰٓؤُاْ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Mimi ninataka ubebe dhambi zangu na dhambi zako ili uwe miongoni mwa watu wa motoni. Na hayo ndio malipo ya madhalimu



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 30

فَطَوَّعَتۡ لَهُۥ نَفۡسُهُۥ قَتۡلَ أَخِيهِ فَقَتَلَهُۥ فَأَصۡبَحَ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ

Basi nafsi yake ikamshawishi kumuua ndugu yake na akamuua na akajikuta ni miongoni mwa waliokula hasara