Sura: AL-HUJURAAT 

Aya : 1

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تُقَدِّمُواْ بَيۡنَ يَدَيِ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٞ

Enyi ambao mmeamini, msitangulize mbele ya Allah na Mtume wake na mcheni Allah. Hakika, Allah ni Mwenye kusikia sana, Mwenye kujua vilivyo (mambo yote).[1]


1- - Aya hii inawafundisha Waislamu adabu muhimu sana mbele ya viongozi wao. Wanatakiwa kutotangulia na kulikatia shauri jambo lolote la kidini na la kidunia bila ya maelekezo. Na amesema Albaidhwaawiy: “Maana ya Aya hii ni kwamba Waislamu wanatakiwa wasikate shauri ya jambo lolote lile kabla ya Allah na Mtume wake kulitolea hukumu jambo hilo”.


Sura: AL-HUJURAAT 

Aya : 2

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَرۡفَعُوٓاْ أَصۡوَٰتَكُمۡ فَوۡقَ صَوۡتِ ٱلنَّبِيِّ وَلَا تَجۡهَرُواْ لَهُۥ بِٱلۡقَوۡلِ كَجَهۡرِ بَعۡضِكُمۡ لِبَعۡضٍ أَن تَحۡبَطَ أَعۡمَٰلُكُمۡ وَأَنتُمۡ لَا تَشۡعُرُونَ

Enyi ambao mmeamini, msinyanyue sauti zenu juu ya sauti ya Nabii, wala msidhihirishe kwake kwa kauli (msimtolee sauti) kama udhihirishaji wa baadhi yenu kwa baadhi (kama mnavyotoleana sauti) ili yasiharibike (yasifutwe) matendo yenu na ilihali hamjui



Sura: AL-HUJURAAT 

Aya : 3

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَغُضُّونَ أَصۡوَٰتَهُمۡ عِندَ رَسُولِ ٱللَّهِ أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ٱمۡتَحَنَ ٱللَّهُ قُلُوبَهُمۡ لِلتَّقۡوَىٰۚ لَهُم مَّغۡفِرَةٞ وَأَجۡرٌ عَظِيمٌ

Hakika wale ambao wanapunguza sauti zao mbele ya mtume wa Allah, hao ndio ambao Allah amekunjua nyoyo zao kwa ucha Mungu wanastahiki msamaha na malipo makubwa



Sura: AL-HUJURAAT 

Aya : 4

إِنَّ ٱلَّذِينَ يُنَادُونَكَ مِن وَرَآءِ ٱلۡحُجُرَٰتِ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡقِلُونَ

Hakika ambao wanaokuita kutoka nyuma ya vyumba, wengi wao hawajui



Sura: AL-HUJURAAT 

Aya : 5

وَلَوۡ أَنَّهُمۡ صَبَرُواْ حَتَّىٰ تَخۡرُجَ إِلَيۡهِمۡ لَكَانَ خَيۡرٗا لَّهُمۡۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na laiti wao wengesubiri hadi utoke kwao ingekua kheri kwao, na Allah ni mwingi wa kusamehe mwingi wa upole



Sura: AL-HUJURAAT 

Aya : 6

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِن جَآءَكُمۡ فَاسِقُۢ بِنَبَإٖ فَتَبَيَّنُوٓاْ أَن تُصِيبُواْ قَوۡمَۢا بِجَهَٰلَةٖ فَتُصۡبِحُواْ عَلَىٰ مَا فَعَلۡتُمۡ نَٰدِمِينَ

Enyi ambao mmeamini, endapo atakujieni (mtu) fasiki kwa habari yoyote basi fanyeni uhakiki msije mkawalenga (mkawahusisha) watu (na jambo lisilokuwa sahihi) kwa kutokujua na mkawa wenye kujuta kwa hilo mlilolitenda.[1]


1- - Imepokewa kwa Anas (Allah amuwiye radhi) akisema kuwa: “Hakika Mtume wa Allah (Rehema na amani zimshukie) alimtuma Al-walid bin Uqbaah kwenda kwa Harith bin Dhwirari kwa ajili ya kuchukua Zaka ambazo amezikusanya kutoka kwa watu wake. Na Alwalid alipokarabia kwenye mji wao, aliogopa. Kwa hiyo alirejea kwa Mtume na kumwambia: Ewe Mtume wa Allah, hakika wale watu wameritadi na wamekataa kutoa Zaka. Basi Maswhaba wakakusudia kutoka ili wawaendee na kuwapiga, ndio Allah akaiteremsha Aya hii ya 6 (ya Sura hii)”. Angalia maelezo ya Hadithi hii kwa upana katika Muhtasari wa Ibnikathiir, juzuu ya 3, ukurasa wa 358. Hadithi hii wameipokea Mashekhe wawili; Bukhari na Muslim, Allah awarehemu.


Sura: AL-HUJURAAT 

Aya : 7

وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ فِيكُمۡ رَسُولَ ٱللَّهِۚ لَوۡ يُطِيعُكُمۡ فِي كَثِيرٖ مِّنَ ٱلۡأَمۡرِ لَعَنِتُّمۡ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ حَبَّبَ إِلَيۡكُمُ ٱلۡإِيمَٰنَ وَزَيَّنَهُۥ فِي قُلُوبِكُمۡ وَكَرَّهَ إِلَيۡكُمُ ٱلۡكُفۡرَ وَٱلۡفُسُوقَ وَٱلۡعِصۡيَانَۚ أُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلرَّـٰشِدُونَ

Na eleweni hakika yupo kwenu mtume wa Allah lau atawakubalia katika mengi miongoni mwa mambo itawapata shida lakini Allah amewapendezeshea kwenu imani na akaipamba hiyo kwenye nyoyo zenu na amechukia kwenu ukafiri na uovu na uasi hao ndio wenye kuongoka



Sura: AL-HUJURAAT 

Aya : 8

فَضۡلٗا مِّنَ ٱللَّهِ وَنِعۡمَةٗۚ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ

Ni Fadhila kutoka kwa Allah na neema na Allah ni mjuzi mno na mwingi wa hekima



Sura: AL-HUJURAAT 

Aya : 9

وَإِن طَآئِفَتَانِ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٱقۡتَتَلُواْ فَأَصۡلِحُواْ بَيۡنَهُمَاۖ فَإِنۢ بَغَتۡ إِحۡدَىٰهُمَا عَلَى ٱلۡأُخۡرَىٰ فَقَٰتِلُواْ ٱلَّتِي تَبۡغِي حَتَّىٰ تَفِيٓءَ إِلَىٰٓ أَمۡرِ ٱللَّهِۚ فَإِن فَآءَتۡ فَأَصۡلِحُواْ بَيۡنَهُمَا بِٱلۡعَدۡلِ وَأَقۡسِطُوٓاْۖ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُقۡسِطِينَ

Na endapo makundi mawili yamepigana basi wasuluhisheni kati yao na endapo litaasi moja ya makundi hayo juu ya lingine basi lipigeni ambalo linaasi hadi lirudi kwenye amri ya Allah na endapo litarudi basi wasuluhisheni kati yao kiuadilifu na fanyeni usawa hakika Allah anapenda wenye kutenda usawa



Sura: AL-HUJURAAT 

Aya : 10

إِنَّمَا ٱلۡمُؤۡمِنُونَ إِخۡوَةٞ فَأَصۡلِحُواْ بَيۡنَ أَخَوَيۡكُمۡۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ

Hakika waumini ni ndugu basi suluhishaneni kwenye udugu wenu na mumche Allah ili mpate kurehemewa



Sura: AL-HUJURAAT 

Aya : 11

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا يَسۡخَرۡ قَوۡمٞ مِّن قَوۡمٍ عَسَىٰٓ أَن يَكُونُواْ خَيۡرٗا مِّنۡهُمۡ وَلَا نِسَآءٞ مِّن نِّسَآءٍ عَسَىٰٓ أَن يَكُنَّ خَيۡرٗا مِّنۡهُنَّۖ وَلَا تَلۡمِزُوٓاْ أَنفُسَكُمۡ وَلَا تَنَابَزُواْ بِٱلۡأَلۡقَٰبِۖ بِئۡسَ ٱلِٱسۡمُ ٱلۡفُسُوقُ بَعۡدَ ٱلۡإِيمَٰنِۚ وَمَن لَّمۡ يَتُبۡ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ

Enyi ambao mmeamini wasicheze shere watu miongoni mwa watu huenda wakawa bora kuliko wao, wala wanawake kwa wanawake huenda wakawa bora kuliko wao wala msizidharau nafsi zenu wala msipeane majina mabaya ya uovu baada ya imani, na yeyote asiye tubu basi hao ndio madhalimu



Sura: AL-HUJURAAT 

Aya : 12

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱجۡتَنِبُواْ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلظَّنِّ إِنَّ بَعۡضَ ٱلظَّنِّ إِثۡمٞۖ وَلَا تَجَسَّسُواْ وَلَا يَغۡتَب بَّعۡضُكُم بَعۡضًاۚ أَيُحِبُّ أَحَدُكُمۡ أَن يَأۡكُلَ لَحۡمَ أَخِيهِ مَيۡتٗا فَكَرِهۡتُمُوهُۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ تَوَّابٞ رَّحِيمٞ

Enyi ambao mmeamini jiepusheni sana na dhana hakika baadhi ya dhana ni dhambi, na msipekuwe pekuwe wala kusengenya baadhi yenu kwa baadhi, hivi anapenda mmoja wenu ale nyama ya ndugu yake maiti?! Na mmelichukia hilo basi mcheni Allah hakika Allah ni mwingi wa kusamehe mwingi wa rehema



Sura: AL-HUJURAAT 

Aya : 13

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنَّا خَلَقۡنَٰكُم مِّن ذَكَرٖ وَأُنثَىٰ وَجَعَلۡنَٰكُمۡ شُعُوبٗا وَقَبَآئِلَ لِتَعَارَفُوٓاْۚ إِنَّ أَكۡرَمَكُمۡ عِندَ ٱللَّهِ أَتۡقَىٰكُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٞ

Enyi watu tumewaumbeni wanaume na wanawake na tumewafanyeni mataifa na makabila ili mutambuane hakika mbora zaidi wenu kwa Allah ni mcha Mungu zaidi kwenu hakika Allah ni mjuzi mno mwenye habari nyingi



Sura: AL-HUJURAAT 

Aya : 14

۞قَالَتِ ٱلۡأَعۡرَابُ ءَامَنَّاۖ قُل لَّمۡ تُؤۡمِنُواْ وَلَٰكِن قُولُوٓاْ أَسۡلَمۡنَا وَلَمَّا يَدۡخُلِ ٱلۡإِيمَٰنُ فِي قُلُوبِكُمۡۖ وَإِن تُطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ لَا يَلِتۡكُم مِّنۡ أَعۡمَٰلِكُمۡ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ

Walisema warabu tumeamini, sema hamjaamini lakini sema tumesilimu na bado haijaingia imani kwenye nyoyo zenu, na endapo mtamtii Allah na mtume wake hatowapunguzia kwenye malipo yenu chochote hakika Allah ni mwingi wakusamehe mwingi wa rehema



Sura: AL-HUJURAAT 

Aya : 15

إِنَّمَا ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ثُمَّ لَمۡ يَرۡتَابُواْ وَجَٰهَدُواْ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۚ أُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلصَّـٰدِقُونَ

Hakika waumini ni wale tu waliomuamini Allah na mtume wake kisha hawakuogopa, na wakapigana kwa mali zao na nafsi zao katika njia ya Allah hao ndio wenye kusadikisha



Sura: AL-HUJURAAT 

Aya : 16

قُلۡ أَتُعَلِّمُونَ ٱللَّهَ بِدِينِكُمۡ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ

Sema hivi mnamueleza Allah dini yenu na Allah anaelewa vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini, na Allah juu ya kila kitu ni mjuzi



Sura: AL-HUJURAAT 

Aya : 17

يَمُنُّونَ عَلَيۡكَ أَنۡ أَسۡلَمُواْۖ قُل لَّا تَمُنُّواْ عَلَيَّ إِسۡلَٰمَكُمۖ بَلِ ٱللَّهُ يَمُنُّ عَلَيۡكُمۡ أَنۡ هَدَىٰكُمۡ لِلۡإِيمَٰنِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Wanajigamba kwako kua wamesilimu, sema: Msijigambe juu ya kusilimu kwenu, bali Allah anajigamba juu yenu kwa kukuongozeni kwenye imani endapo mtakua wa kweli



Sura: AL-HUJURAAT 

Aya : 18

إِنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ غَيۡبَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَٱللَّهُ بَصِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ

Hakika Allah anavijua visivyoonekana mbingni na ardhini, na Allah anayaona yote mnayofanya