حمٓ
Haamiim
Tarayya :
وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ
Nina apa kwa Kitabu kinacho bainisha
إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ فِي لَيۡلَةٖ مُّبَٰرَكَةٍۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ
Hakika, tumekiteremsha (kitabu hiki cha Qur’ani) katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi tumekuwa waonyaji
فِيهَا يُفۡرَقُ كُلُّ أَمۡرٍ حَكِيمٍ
Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hekima
أَمۡرٗا مِّنۡ عِندِنَآۚ إِنَّا كُنَّا مُرۡسِلِينَ
Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma
رَحۡمَةٗ مِّن رَّبِّكَۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ
Ni rehema kutoka kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ndiye tu Mwenye kusikia sana, Mwenye kujua
رَبِّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَآۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyopo baina yake, ikiwa nyinyi mna yakini
لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۖ رَبُّكُمۡ وَرَبُّ ءَابَآئِكُمُ ٱلۡأَوَّلِينَ
Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha- Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo
بَلۡ هُمۡ فِي شَكّٖ يَلۡعَبُونَ
Lakini wao wanacheza katika shaka
فَٱرۡتَقِبۡ يَوۡمَ تَأۡتِي ٱلسَّمَآءُ بِدُخَانٖ مُّبِينٖ
Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapoleta moshi ulio dhahiri
يَغۡشَى ٱلنَّاسَۖ هَٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٞ
Utakaowafunika watu: Hii ni adhabu chungu!
رَّبَّنَا ٱكۡشِفۡ عَنَّا ٱلۡعَذَابَ إِنَّا مُؤۡمِنُونَ
Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini
أَنَّىٰ لَهُمُ ٱلذِّكۡرَىٰ وَقَدۡ جَآءَهُمۡ رَسُولٞ مُّبِينٞ
Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwishawafikia Mtume mwenye kubainisha
ثُمَّ تَوَلَّوۡاْ عَنۡهُ وَقَالُواْ مُعَلَّمٞ مَّجۡنُونٌ
Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu
إِنَّا كَاشِفُواْ ٱلۡعَذَابِ قَلِيلًاۚ إِنَّكُمۡ عَآئِدُونَ
Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile!
يَوۡمَ نَبۡطِشُ ٱلۡبَطۡشَةَ ٱلۡكُبۡرَىٰٓ إِنَّا مُنتَقِمُونَ
Siku tutakayo yashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa
۞وَلَقَدۡ فَتَنَّا قَبۡلَهُمۡ قَوۡمَ فِرۡعَوۡنَ وَجَآءَهُمۡ رَسُولٞ كَرِيمٌ
Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu
أَنۡ أَدُّوٓاْ إِلَيَّ عِبَادَ ٱللَّهِۖ إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ
Akasema: Nipeni waja wa Allah; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu
وَأَن لَّا تَعۡلُواْ عَلَى ٱللَّهِۖ إِنِّيٓ ءَاتِيكُم بِسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٖ
Na msimfanyie kiburi Allah; hakika mimi nitakuleteeni uthibitisho ulio wazi
وَإِنِّي عُذۡتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُمۡ أَن تَرۡجُمُونِ
Nami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe
وَإِن لَّمۡ تُؤۡمِنُواْ لِي فَٱعۡتَزِلُونِ
Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami
فَدَعَا رَبَّهُۥٓ أَنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ قَوۡمٞ مُّجۡرِمُونَ
Ndipo akamwomba Mola wake Mlezi: Hakika watu hawa ni wakosefu
فَأَسۡرِ بِعِبَادِي لَيۡلًا إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ
Allah akasema: Basi nenda na waja wangu usiku. Kwa yakini mtafuatwa
وَٱتۡرُكِ ٱلۡبَحۡرَ رَهۡوًاۖ إِنَّهُمۡ جُندٞ مُّغۡرَقُونَ
Na iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao hao ni jeshi litakalo zamishwa
كَمۡ تَرَكُواْ مِن جَنَّـٰتٖ وَعُيُونٖ
Mabustani mangapi, na chemchem ngapi waliziacha!
وَزُرُوعٖ وَمَقَامٖ كَرِيمٖ
Na mimea na vyeo vitukufu!
وَنَعۡمَةٖ كَانُواْ فِيهَا فَٰكِهِينَ
Na neema walizokuwa wakiji-stareheshea!
كَذَٰلِكَۖ وَأَوۡرَثۡنَٰهَا قَوۡمًا ءَاخَرِينَ
Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe
فَمَا بَكَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلسَّمَآءُ وَٱلۡأَرۡضُ وَمَا كَانُواْ مُنظَرِينَ
Hazikuwalilia mbingu wala ardhi, wala hawakupewa muhula
وَلَقَدۡ نَجَّيۡنَا بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ مِنَ ٱلۡعَذَابِ ٱلۡمُهِينِ
Na bila ya shaka tuliwaokoa Wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha