Sura: AL-HUMAZAH 

Aya : 1

وَيۡلٞ لِّكُلِّ هُمَزَةٖ لُّمَزَةٍ

Olewake kila safihi, msengenyaji!



Sura: AL-HUMAZAH 

Aya : 2

ٱلَّذِي جَمَعَ مَالٗا وَعَدَّدَهُۥ

Aliye kusanya mali na kuyahisabu



Sura: AL-HUMAZAH 

Aya : 3

يَحۡسَبُ أَنَّ مَالَهُۥٓ أَخۡلَدَهُۥ

Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele!



Sura: AL-HUMAZAH 

Aya : 4

كَلَّاۖ لَيُنۢبَذَنَّ فِي ٱلۡحُطَمَةِ

la hasha! Atavurumishwa katika moto hutama



Sura: AL-HUMAZAH 

Aya : 5

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡحُطَمَةُ

Na nani atakujuvya ni nini moto wa hutama?



Sura: AL-HUMAZAH 

Aya : 6

نَارُ ٱللَّهِ ٱلۡمُوقَدَةُ

Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa



Sura: AL-HUMAZAH 

Aya : 7

ٱلَّتِي تَطَّلِعُ عَلَى ٱلۡأَفۡـِٔدَةِ

Ambao unapanda nyoyoni



Sura: AL-HUMAZAH 

Aya : 8

إِنَّهَا عَلَيۡهِم مُّؤۡصَدَةٞ

Hakika huo utafungiwa nao



Sura: AL-HUMAZAH 

Aya : 9

فِي عَمَدٖ مُّمَدَّدَةِۭ

Kwenye nguzo zilio nyooshwa