Sura: ATTAKAATHUR

Aya : 1

أَلۡهَىٰكُمُ ٱلتَّكَاثُرُ

Kumekushughulisheni kutafuta wingi



Sura: ATTAKAATHUR

Aya : 2

حَتَّىٰ زُرۡتُمُ ٱلۡمَقَابِرَ

Mpaka mje makaburini!



Sura: ATTAKAATHUR

Aya : 3

كَلَّا سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ

Sivyo hivyo! Mtakuja kujua!



Sura: ATTAKAATHUR

Aya : 4

ثُمَّ كَلَّا سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ

Tena sivyo hivyo! Mtakuja kujua!



Sura: ATTAKAATHUR

Aya : 5

كَلَّا لَوۡ تَعۡلَمُونَ عِلۡمَ ٱلۡيَقِينِ

Sivyo hivyo! Lau mngelijua kujua kwa yakini,



Sura: ATTAKAATHUR

Aya : 6

لَتَرَوُنَّ ٱلۡجَحِيمَ

Basi bila ya shaka yoyote mtaiona Jahanamu!



Sura: ATTAKAATHUR

Aya : 7

ثُمَّ لَتَرَوُنَّهَا عَيۡنَ ٱلۡيَقِينِ

Tena, bila ya shaka yoyote, mtaiona kwa jicho la yakini



Sura: ATTAKAATHUR

Aya : 8

ثُمَّ لَتُسۡـَٔلُنَّ يَوۡمَئِذٍ عَنِ ٱلنَّعِيمِ

Tena bila ya shaka yoyote mtaulizwa siku hiyo juu ya neema