Sura: YUSUF 

Aya : 91

قَالُواْ تَٱللَّهِ لَقَدۡ ءَاثَرَكَ ٱللَّهُ عَلَيۡنَا وَإِن كُنَّا لَخَٰطِـِٔينَ

Walisema: Tunaapa kwa Allah (kwamba), hakika Allah amekufadhilisha wewe (amekufanya wewe bora) kuliko sisi, na hakika kabisa sisi tulikuwa wakosefu



Sura: YUSUF 

Aya : 92

قَالَ لَا تَثۡرِيبَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡيَوۡمَۖ يَغۡفِرُ ٱللَّهُ لَكُمۡۖ وَهُوَ أَرۡحَمُ ٱلرَّـٰحِمِينَ

(Yusuf) Alisema: Leo hakuna lawama juu yenu. Allah atakusameheni, naye ni Mwenye huruma kuliko wenye huruma wote



Sura: YUSUF 

Aya : 93

ٱذۡهَبُواْ بِقَمِيصِي هَٰذَا فَأَلۡقُوهُ عَلَىٰ وَجۡهِ أَبِي يَأۡتِ بَصِيرٗا وَأۡتُونِي بِأَهۡلِكُمۡ أَجۡمَعِينَ

Nendeni na kanzu yangu hii na mkaitupie usoni kwa Baba yangu, (akiipata harufu yangu tu atapona na) ataona na nileteeni familia yenu yote



Sura: YUSUF 

Aya : 94

وَلَمَّا فَصَلَتِ ٱلۡعِيرُ قَالَ أَبُوهُمۡ إِنِّي لَأَجِدُ رِيحَ يُوسُفَۖ لَوۡلَآ أَن تُفَنِّدُونِ

Na msafara ulipoondoka tu (Misri), Baba yao alisema (kuwaambia aliokuwa nao): Hakika, mimi kwa yakini kabisa nanusa harufu ya Yusuf, lau kama hamtaniona mpuuzi



Sura: YUSUF 

Aya : 95

قَالُواْ تَٱللَّهِ إِنَّكَ لَفِي ضَلَٰلِكَ ٱلۡقَدِيمِ

Walisema: Tunaapa kwa Allah, hakika wewe bado kabisa ungali katika upotevu wako wa kale (wa kumpenda Yusuf)



Sura: YUSUF 

Aya : 96

فَلَمَّآ أَن جَآءَ ٱلۡبَشِيرُ أَلۡقَىٰهُ عَلَىٰ وَجۡهِهِۦ فَٱرۡتَدَّ بَصِيرٗاۖ قَالَ أَلَمۡ أَقُل لَّكُمۡ إِنِّيٓ أَعۡلَمُ مِنَ ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ

Basi alipofika mbashiri na akaitupa kanzu usoni kwake na kwasababu hiyo, akarejea kuona, alisema: Je, sikukuambieni kuwa mimi ninajua kwa Allah msiyoyajua?



Sura: YUSUF 

Aya : 97

قَالُواْ يَـٰٓأَبَانَا ٱسۡتَغۡفِرۡ لَنَا ذُنُوبَنَآ إِنَّا كُنَّا خَٰطِـِٔينَ

Walisema: Ewe Baba yetu, tuombee (kwa Allah) msamaha kwa dhambi zetu. Kwa hakika sisi tulikuwa wakosaji



Sura: YUSUF 

Aya : 98

قَالَ سَوۡفَ أَسۡتَغۡفِرُ لَكُمۡ رَبِّيٓۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ

Alisema: Nitakuombeeni msa-maha kwa Mola wangu Mlezi. Hakika, Yeye (Allah) ndiye tu Msamehevu, Mwenye kurehemu



Sura: YUSUF 

Aya : 99

فَلَمَّا دَخَلُواْ عَلَىٰ يُوسُفَ ءَاوَىٰٓ إِلَيۡهِ أَبَوَيۡهِ وَقَالَ ٱدۡخُلُواْ مِصۡرَ إِن شَآءَ ٱللَّهُ ءَامِنِينَ

Basi walipoingia kwa Yusuf aliwakumbatia wazazi wake na alisema: Ingieni Misri, Inshaa-Allah, mkiwa katika amani



Sura: YUSUF 

Aya : 100

وَرَفَعَ أَبَوَيۡهِ عَلَى ٱلۡعَرۡشِ وَخَرُّواْ لَهُۥ سُجَّدٗاۖ وَقَالَ يَـٰٓأَبَتِ هَٰذَا تَأۡوِيلُ رُءۡيَٰيَ مِن قَبۡلُ قَدۡ جَعَلَهَا رَبِّي حَقّٗاۖ وَقَدۡ أَحۡسَنَ بِيٓ إِذۡ أَخۡرَجَنِي مِنَ ٱلسِّجۡنِ وَجَآءَ بِكُم مِّنَ ٱلۡبَدۡوِ مِنۢ بَعۡدِ أَن نَّزَغَ ٱلشَّيۡطَٰنُ بَيۡنِي وَبَيۡنَ إِخۡوَتِيٓۚ إِنَّ رَبِّي لَطِيفٞ لِّمَا يَشَآءُۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡحَكِيمُ

Na akawapandisha wazazi wake kwenye kiti cha enzi, na wote wakaporomoka kumsujudia.[1] Na (Yusuf) alisema: Ewe Baba yangu, hii ndiyo tafsiri ya ile ndoto yangu pale zamani. Na Allah ameijaalia (ndoto hiyo) kuwa ya kweli. Na (Allah) amenifanyia mazuri mno kwasababu alinitoa gerezani na amekuleteni kutoka jangwani baada ya shetani kuchochea uhasama baina yangu na baina ya ndugu zangu. Hakika, Mola wangu Mlezi ni Muungwana kwa ayatakayo. Kwa hakika, Yeye (Allah) ndiye Mjuzi, Mwenye hekima


1- - Huu ulikuwa utaratibu wa wakati huo wa kusalimia viongozi kwa kusujudu.


Sura: YUSUF 

Aya : 101

۞رَبِّ قَدۡ ءَاتَيۡتَنِي مِنَ ٱلۡمُلۡكِ وَعَلَّمۡتَنِي مِن تَأۡوِيلِ ٱلۡأَحَادِيثِۚ فَاطِرَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ أَنتَ وَلِيِّۦ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۖ تَوَفَّنِي مُسۡلِمٗا وَأَلۡحِقۡنِي بِٱلصَّـٰلِحِينَ

(Kisha Yusuf akaomba akasema): Ewe Mola wangu Mlezi, kwa hakika umenipa sehemu ya ufalme na umenifundisha sehemu ya tafsiri ya matukio (ndoto). (Ewe) Muumba wa mbingu na ardhi, Wewe ndiye Mlinzi wangu duniani na Akhera. Nifishe nikiwa Muislamu na nikutanishe na wenye kutenda mema



Sura: YUSUF 

Aya : 102

ذَٰلِكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلۡغَيۡبِ نُوحِيهِ إِلَيۡكَۖ وَمَا كُنتَ لَدَيۡهِمۡ إِذۡ أَجۡمَعُوٓاْ أَمۡرَهُمۡ وَهُمۡ يَمۡكُرُونَ

Hizo (habari zilizotajwa kuhusu Yusuf) ni sehemu ya habari za Ghaibu tulizokufunulia (ewe Muhammad) na hukuwa pamoja nao wakati (ndugu wa Yusuf) walipo azimia kwa pamoja shauri lao (la kumdhuru Yusuf) na ilhali wao wanafanya hila



Sura: YUSUF 

Aya : 103

وَمَآ أَكۡثَرُ ٱلنَّاسِ وَلَوۡ حَرَصۡتَ بِمُؤۡمِنِينَ

Na watu wengi sana si wenye kuamini nahataukijitahidi



Sura: YUSUF 

Aya : 104

وَمَا تَسۡـَٔلُهُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۚ إِنۡ هُوَ إِلَّا ذِكۡرٞ لِّلۡعَٰلَمِينَ

Na (wewe) huwaombi ujira wowote juu ya hilo (la kuifikisha hii Qur’ani). Haikuwa hiyo (Qur’ani) isipokuwa tu ni ukumbusho kwa walimwengu wote



Sura: YUSUF 

Aya : 105

وَكَأَيِّن مِّنۡ ءَايَةٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ يَمُرُّونَ عَلَيۡهَا وَهُمۡ عَنۡهَا مُعۡرِضُونَ

Na (kuna) ishara ngapi katika mbingu na ardhi wanazozipitia, na hali ya kuwa wanazipuuza?



Sura: YUSUF 

Aya : 106

وَمَا يُؤۡمِنُ أَكۡثَرُهُم بِٱللَّهِ إِلَّا وَهُم مُّشۡرِكُونَ

Na wengi wao hawamuamini Allah isipokuwa tu wakiwa washirikina



Sura: YUSUF 

Aya : 107

أَفَأَمِنُوٓاْ أَن تَأۡتِيَهُمۡ غَٰشِيَةٞ مِّنۡ عَذَابِ ٱللَّهِ أَوۡ تَأۡتِيَهُمُ ٱلسَّاعَةُ بَغۡتَةٗ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ

Je, hivi wamejiaminisha kuwa haitowajia adhabu ya Allah ya kuwagubika au hakitawafikia Kiyama kwa ghafla na hali hawatambui?



Sura: YUSUF 

Aya : 108

قُلۡ هَٰذِهِۦ سَبِيلِيٓ أَدۡعُوٓاْ إِلَى ٱللَّهِۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا۠ وَمَنِ ٱتَّبَعَنِيۖ وَسُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Sema: Hii ndiyo njia yangu; ninalingania (ninahubiri) kwa Allah kwa kujua, mimi na wanaonifuata. Na Allah ametakasika na mimi siomiongoni mwa washirikina



Sura: YUSUF 

Aya : 109

وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ إِلَّا رِجَالٗا نُّوحِيٓ إِلَيۡهِم مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡقُرَىٰٓۗ أَفَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۗ وَلَدَارُ ٱلۡأٓخِرَةِ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Na hatukutuma kabla yako isipokuwa (Mitume) wanaume tunaowafunulia (tunaowashushia Wahyi) miongoni mwa watu wa mijini. Je, hivi hawatembei katika ardhi wakaona jinsi ulivyokuwa mwisho wa waliokuwa kabla yao? Na hakika, nyumba ya Akhera ni bora kwa wanaomcha Allah. Basi hamtumii akili?



Sura: YUSUF 

Aya : 110

حَتَّىٰٓ إِذَا ٱسۡتَيۡـَٔسَ ٱلرُّسُلُ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُمۡ قَدۡ كُذِبُواْ جَآءَهُمۡ نَصۡرُنَا فَنُجِّيَ مَن نَّشَآءُۖ وَلَا يُرَدُّ بَأۡسُنَا عَنِ ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ

(Na hatukutuma kabla yako isipokuwa (Mitume) wanaume tunaowafunulia (tunaowashushia Wahyi) Mpaka Mitume (hao) walipokata tamaa (ya watu wao kutoamini) na wakadhani kuwa wamekadhibishwa (wamepingwa), hapo ikawajia nusura yetu natukawaokoa tuwatakao. Na adhabu yetu kali hairudishwi (haizuiliki) kwa watu waovu



Sura: YUSUF 

Aya : 111

لَقَدۡ كَانَ فِي قَصَصِهِمۡ عِبۡرَةٞ لِّأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِۗ مَا كَانَ حَدِيثٗا يُفۡتَرَىٰ وَلَٰكِن تَصۡدِيقَ ٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَتَفۡصِيلَ كُلِّ شَيۡءٖ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ

Kwa hakika kabisa, katika simulizi zao (hao Mitume) kuna mazingatio kwa wenye akili. Haikuwa (hii Qur’an ni) maneno yanayozushwa lakini ni usadikisho (uthibitisho) wa (maandiko matakatifu) yaliyokuwepo kabla yake (Taurati na Injili) na ni ufafanuzi wa kila kitu na ni muongozo na rehema kwa watu wanaoamini