قَالُواْ رَبَّنَا مَن قَدَّمَ لَنَا هَٰذَا فَزِدۡهُ عَذَابٗا ضِعۡفٗا فِي ٱلنَّارِ
Waseme: Mola wetu Mlezi! Aliye tusababishia haya mzidishie adhabu mara mbili Motoni
Tarayya :
وَقَالُواْ مَا لَنَا لَا نَرَىٰ رِجَالٗا كُنَّا نَعُدُّهُم مِّنَ ٱلۡأَشۡرَارِ
Watasema: Tuna nini hata hatuwaoni wale watu ambao tukiwahesabu ndio katika waovu?
أَتَّخَذۡنَٰهُمۡ سِخۡرِيًّا أَمۡ زَاغَتۡ عَنۡهُمُ ٱلۡأَبۡصَٰرُ
Tulikosea tulipo wafanyia mas-khara, au macho yetu tu hayawaoni?
إِنَّ ذَٰلِكَ لَحَقّٞ تَخَاصُمُ أَهۡلِ ٱلنَّارِ
Hakika hayo bila ya shaka ndiyo makhasimiano ya watu wa Motoni
قُلۡ إِنَّمَآ أَنَا۠ مُنذِرٞۖ وَمَا مِنۡ إِلَٰهٍ إِلَّا ٱللَّهُ ٱلۡوَٰحِدُ ٱلۡقَهَّارُ
Sema: Hakika mimi ni mwonyaji tu; na hapana mungu ila Allah Mmoja, Mwenye nguvu,
رَبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡغَفَّـٰرُ
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake, Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe
قُلۡ هُوَ نَبَؤٌاْ عَظِيمٌ
Sema: Hii ni habari kubwa kabisa
أَنتُمۡ عَنۡهُ مُعۡرِضُونَ
Ambayo nyinyi mnaipuuza
مَا كَانَ لِيَ مِنۡ عِلۡمِۭ بِٱلۡمَلَإِ ٱلۡأَعۡلَىٰٓ إِذۡ يَخۡتَصِمُونَ
Sikuwa na elimu ya mambo ya viumbe wakuu watukufu walipokuwa wakishindana
إِن يُوحَىٰٓ إِلَيَّ إِلَّآ أَنَّمَآ أَنَا۠ نَذِيرٞ مُّبِينٌ
Haikufunuliwa kwangu isipo kuwa ya kwamba hakika mimi ni mwonyaji dhahiri
إِذۡ قَالَ رَبُّكَ لِلۡمَلَـٰٓئِكَةِ إِنِّي خَٰلِقُۢ بَشَرٗا مِّن طِينٖ
Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitaumba mtu kutokana na udongo
فَإِذَا سَوَّيۡتُهُۥ وَنَفَخۡتُ فِيهِ مِن رُّوحِي فَقَعُواْ لَهُۥ سَٰجِدِينَ
Na nitakapo mkamilisha na kumpulizia roho inayo tokana nami, basi muangukieni kwa kumtii
فَسَجَدَ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ كُلُّهُمۡ أَجۡمَعُونَ
Basi Malaika wakatii wote pamoja
إِلَّآ إِبۡلِيسَ ٱسۡتَكۡبَرَ وَكَانَ مِنَ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Isipo kuwa Iblisi; alijivuna na akawa katika makafiri
قَالَ يَـٰٓإِبۡلِيسُ مَا مَنَعَكَ أَن تَسۡجُدَ لِمَا خَلَقۡتُ بِيَدَيَّۖ أَسۡتَكۡبَرۡتَ أَمۡ كُنتَ مِنَ ٱلۡعَالِينَ
Allah akamwambia: Ewe Iblisi! Kipi kilicho kuzuia kumtii yule niliye muumba kwa mikono yangu? Je! Umejiona mkubwa, au umekuwa katika wakuu kweli?
قَالَ أَنَا۠ خَيۡرٞ مِّنۡهُ خَلَقۡتَنِي مِن نَّارٖ وَخَلَقۡتَهُۥ مِن طِينٖ
Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo
قَالَ فَٱخۡرُجۡ مِنۡهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٞ
Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umelaanika
وَإِنَّ عَلَيۡكَ لَعۡنَتِيٓ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلدِّينِ
Na hakika laana yangu itakuwa juu yako mpaka Siku ya Malipo
قَالَ رَبِّ فَأَنظِرۡنِيٓ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ
Akasema: Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watayo fufuliwa viumbe
قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ ٱلۡمُنظَرِينَ
Allah akasema: Basi umekwisha kuwa miongoni mwa walio pewa muhula,
إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡوَقۡتِ ٱلۡمَعۡلُومِ
Mpaka siku ya wakati maalumu
قَالَ فَبِعِزَّتِكَ لَأُغۡوِيَنَّهُمۡ أَجۡمَعِينَ
Akasema (Iblisi): Naapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote,
إِلَّا عِبَادَكَ مِنۡهُمُ ٱلۡمُخۡلَصِينَ
Isipo kuwa wale waja wako miongoni mwao walio chaguliwa
قَالَ فَٱلۡحَقُّ وَٱلۡحَقَّ أَقُولُ
Akasema: Haki! Na haki ninaisema
لَأَمۡلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكَ وَمِمَّن تَبِعَكَ مِنۡهُمۡ أَجۡمَعِينَ
Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa wewe na kwa hao wote wenye kukufuata miongoni mwao
قُلۡ مَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٖ وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلۡمُتَكَلِّفِينَ
Sema (Ewe Mtume): Sikuombeni ujira juu ya haya, wala mimi si katika wadanganyifu
إِنۡ هُوَ إِلَّا ذِكۡرٞ لِّلۡعَٰلَمِينَ
Hayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu wote
وَلَتَعۡلَمُنَّ نَبَأَهُۥ بَعۡدَ حِينِۭ
Na bila ya shaka mtajua khabari zake baada ya muda