Sura: AL-MAIDA 

Aya : 31

فَبَعَثَ ٱللَّهُ غُرَابٗا يَبۡحَثُ فِي ٱلۡأَرۡضِ لِيُرِيَهُۥ كَيۡفَ يُوَٰرِي سَوۡءَةَ أَخِيهِۚ قَالَ يَٰوَيۡلَتَىٰٓ أَعَجَزۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِثۡلَ هَٰذَا ٱلۡغُرَابِ فَأُوَٰرِيَ سَوۡءَةَ أَخِيۖ فَأَصۡبَحَ مِنَ ٱلنَّـٰدِمِينَ

Basi hapo Allah akampeleka kunguru anayefukua ardhini ili amuoneshe namna ya kusitiri (kuzika) mwili wa nduguye. Akasema: “Ole wangu! Hivi nimeshindwa kuwa kama huyu kunguru nikasitiri mwili wa ndugu yangu?”. Basi akawa ni miongoni mwa wenye kujuta



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 32

مِنۡ أَجۡلِ ذَٰلِكَ كَتَبۡنَا عَلَىٰ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ أَنَّهُۥ مَن قَتَلَ نَفۡسَۢا بِغَيۡرِ نَفۡسٍ أَوۡ فَسَادٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ ٱلنَّاسَ جَمِيعٗا وَمَنۡ أَحۡيَاهَا فَكَأَنَّمَآ أَحۡيَا ٱلنَّاسَ جَمِيعٗاۚ وَلَقَدۡ جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُنَا بِٱلۡبَيِّنَٰتِ ثُمَّ إِنَّ كَثِيرٗا مِّنۡهُم بَعۡدَ ذَٰلِكَ فِي ٱلۡأَرۡضِ لَمُسۡرِفُونَ

Kwa sababu ya hayo[1], tume-waandikia (tumewafaradhishia) Wana wa Israil ya kwamba, aliyeua nafsi (ya mtu) bila ya (yeye kuua) nafsi au kufanya uovu katika nchi, basi ni kama ameua watu wote. Na mwenye kuihuisha (kuiokoa nafsi isife) ni kama ameokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja za wazi, kisha wengi miongoni mwao baada ya hayo wakawa wenye kufanya yaliyovuka mipaka katika ardhi


1- - Kosa la mauaji yaliyofanywa na mmoja wa watoto wa Mtume Adamu.


Sura: AL-MAIDA 

Aya : 33

إِنَّمَا جَزَـٰٓؤُاْ ٱلَّذِينَ يُحَارِبُونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَيَسۡعَوۡنَ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَسَادًا أَن يُقَتَّلُوٓاْ أَوۡ يُصَلَّبُوٓاْ أَوۡ تُقَطَّعَ أَيۡدِيهِمۡ وَأَرۡجُلُهُم مِّنۡ خِلَٰفٍ أَوۡ يُنفَوۡاْ مِنَ ٱلۡأَرۡضِۚ ذَٰلِكَ لَهُمۡ خِزۡيٞ فِي ٱلدُّنۡيَاۖ وَلَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Kwa hakika kabisa, malipo ya wale wanaopigana vita na Allah na Mtume wake[1] na wanakwenda kasi katika kufanya uharibifu duniani ni kuuawa bila ya huruma au kusulubiwa au kukatwa katwa mikono yao na miguu yao kwa kupishana au kutolewa katika nchi (na kupelekwa uhamishoni). Hiyo ni kwa sababu wanastahiki hizaya (fedheha) duniani, na huko Akhera watapata adhabu kubwa mno


1- - Kinachokusudiwa hapa ni kuupiga vita Uislamu na Waislamu.


Sura: AL-MAIDA 

Aya : 34

إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ مِن قَبۡلِ أَن تَقۡدِرُواْ عَلَيۡهِمۡۖ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Isipokuwa wale waliotubu kabla hamjawatia nguvuni. Basi jueni kwamba, kwa hakika Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 35

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱبۡتَغُوٓاْ إِلَيۡهِ ٱلۡوَسِيلَةَ وَجَٰهِدُواْ فِي سَبِيلِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ

Enyi miloamini, mcheni Allah na tafuteni Wasila (njia) ya kumfikia[1], na pambaneni katika njia (dini) yake ili mfaulu


1- - Wasila walivyoieleza wanachuoni ni kila aina ya ibada aliyoianisha Mtume, Allah amshushie rehema na amani. Ibada zilizoainishwa na Mtume, Allah amshushie rehema na amani, ndizo zinazomfanya Muislamu awe karibu na Allah.


Sura: AL-MAIDA 

Aya : 36

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَوۡ أَنَّ لَهُم مَّا فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا وَمِثۡلَهُۥ مَعَهُۥ لِيَفۡتَدُواْ بِهِۦ مِنۡ عَذَابِ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ مَا تُقُبِّلَ مِنۡهُمۡۖ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Hakika ya wale waliokufuru, lau kama wangekuwa na yote yaliyomo duniani na mengine kama hayo ili watoe fidia ya kuepukana na adhabu ya Siku ya Kiyama, wasingekubaliwa, na watapata adhabu iumizayo



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 37

يُرِيدُونَ أَن يَخۡرُجُواْ مِنَ ٱلنَّارِ وَمَا هُم بِخَٰرِجِينَ مِنۡهَاۖ وَلَهُمۡ عَذَابٞ مُّقِيمٞ

Wanataka watoke Motoni na hawatatoka humo, na watakuwa na adhabu ya kudumu



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 38

وَٱلسَّارِقُ وَٱلسَّارِقَةُ فَٱقۡطَعُوٓاْ أَيۡدِيَهُمَا جَزَآءَۢ بِمَا كَسَبَا نَكَٰلٗا مِّنَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٞ

Na mwizi mwanaume na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao, ikiwa ni malipo ya waliyoyachuma (waliyoyatenda) (na) ni adhabu ifundishayo kutoka kwa Allah. Na Allah ni Mwenye nguvu kubwa, Mwenye hekima



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 39

فَمَن تَابَ مِنۢ بَعۡدِ ظُلۡمِهِۦ وَأَصۡلَحَ فَإِنَّ ٱللَّهَ يَتُوبُ عَلَيۡهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٌ

Basi mwenye kutubu baada ya kudhulumu kwake na akatengeneza (akarekebisha tabia zake), basi Allah hupokea toba yake. Hakika, Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 40

أَلَمۡ تَعۡلَمۡ أَنَّ ٱللَّهَ لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ يُعَذِّبُ مَن يَشَآءُ وَيَغۡفِرُ لِمَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Hivi hujui ya kwamba, ni wa Allah tu ufalme wa mbinguni na ardhini? Anamuadhibu amtakaye na anamsamehe amtakaye. Na Allah ni Muweza wa kila kitu



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 41

۞يَـٰٓأَيُّهَا ٱلرَّسُولُ لَا يَحۡزُنكَ ٱلَّذِينَ يُسَٰرِعُونَ فِي ٱلۡكُفۡرِ مِنَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِأَفۡوَٰهِهِمۡ وَلَمۡ تُؤۡمِن قُلُوبُهُمۡۛ وَمِنَ ٱلَّذِينَ هَادُواْۛ سَمَّـٰعُونَ لِلۡكَذِبِ سَمَّـٰعُونَ لِقَوۡمٍ ءَاخَرِينَ لَمۡ يَأۡتُوكَۖ يُحَرِّفُونَ ٱلۡكَلِمَ مِنۢ بَعۡدِ مَوَاضِعِهِۦۖ يَقُولُونَ إِنۡ أُوتِيتُمۡ هَٰذَا فَخُذُوهُ وَإِن لَّمۡ تُؤۡتَوۡهُ فَٱحۡذَرُواْۚ وَمَن يُرِدِ ٱللَّهُ فِتۡنَتَهُۥ فَلَن تَمۡلِكَ لَهُۥ مِنَ ٱللَّهِ شَيۡـًٔاۚ أُوْلَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ لَمۡ يُرِدِ ٱللَّهُ أَن يُطَهِّرَ قُلُوبَهُمۡۚ لَهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا خِزۡيٞۖ وَلَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٞ

Ewe Mtume, wasikusononeshe wale wanaokimbilia ukafiri, ambao wamesema kwa vinywa vyao kwamba: Tumeamini na ilhali nyoyo zao hazijaamini, na (pia wasikusononeshe) waliojiita Waya-hudi, wasikilizaji sana wa uwongo (na kuukubali), wasikilizaji sana wa watu wengine wasiofika kwako (kwa kujifunza dini), wanapotosha maneno katika mahali pake, wanasema: Mkipewa hiki basi kipokeeni, na msipopewa tahadharini[1]. Na mtu ambaye Allah anataka kumtahini, katu huwezi kuwa na mamlaka ya jambo lolote (la kumkinga) dhidi ya Allah. Hao ndio ambao Allah hakutaka kuzitakasa nyoyo zao. Wana hizaya duniani, na Akhera watakuwa na adhabu kubwa mno


1- - Hapa Aya inaelezea tabia ya hovyo ya Wayahudi. Imamu Muslim, Allah amrehemu, amepokea Hadithi iliyonukuliwa na Swahaba Albaraa bin Azib, Allah amuwie radhi, kwamba, Wayahudi walikuwa na sheria ya mzinzi kupigwa mawe hadi kufa. Lakini kwakuwa Mabwana wakubwa wengi wa Kiyahudi walitumbukia katika janga la uzinzi waliibadilisha hukumu hiyo na badala yake wakawa wanampaka masizi usoni kama adhabu mbadala ya kupigwa mawe hadi kufa. Mtume, Allah amshushie rehema na amani, aliwakosoa na kuwarudisha kwenye adhabu ya kupigwa mawe hadi kufa na alimshukuru Allah kwa kumuwezesha kuihuisha na kuirudisha sheria ambayo Wayahudi waliificha.


Sura: AL-MAIDA 

Aya : 42

سَمَّـٰعُونَ لِلۡكَذِبِ أَكَّـٰلُونَ لِلسُّحۡتِۚ فَإِن جَآءُوكَ فَٱحۡكُم بَيۡنَهُمۡ أَوۡ أَعۡرِضۡ عَنۡهُمۡۖ وَإِن تُعۡرِضۡ عَنۡهُمۡ فَلَن يَضُرُّوكَ شَيۡـٔٗاۖ وَإِنۡ حَكَمۡتَ فَٱحۡكُم بَيۡنَهُم بِٱلۡقِسۡطِۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُقۡسِطِينَ

(Hao ni) Wasikilizaji sana wa uwongo, walaji sana wa haramu. Basi wakikujia, wahukumu baina yao au wapuuze[1]. Na ukiwapuuza, katu hawatakudhuru kitu chochote. Na ukihukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu. Hakika, Allah anawapenda waadilifu


1- - Amri hii ya kupuuza imefutwa kwa Aya ya 49 ya Sura hii hii ya Almaida (5) inayolazimisha kutekelezwa kwa hukumu bila ya kuwa na hiari ya kupuuza.


Sura: AL-MAIDA 

Aya : 43

وَكَيۡفَ يُحَكِّمُونَكَ وَعِندَهُمُ ٱلتَّوۡرَىٰةُ فِيهَا حُكۡمُ ٱللَّهِ ثُمَّ يَتَوَلَّوۡنَ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَۚ وَمَآ أُوْلَـٰٓئِكَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na inakuwaje wanakufanya wewe hakimu na ilhali wanayo Taurati yenye hukumu za Allah kisha baada ya hayo wanageuka? Na hao si waumini (wa kweli wa Utume wako wala kitabu chao)



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 44

إِنَّآ أَنزَلۡنَا ٱلتَّوۡرَىٰةَ فِيهَا هُدٗى وَنُورٞۚ يَحۡكُمُ بِهَا ٱلنَّبِيُّونَ ٱلَّذِينَ أَسۡلَمُواْ لِلَّذِينَ هَادُواْ وَٱلرَّبَّـٰنِيُّونَ وَٱلۡأَحۡبَارُ بِمَا ٱسۡتُحۡفِظُواْ مِن كِتَٰبِ ٱللَّهِ وَكَانُواْ عَلَيۡهِ شُهَدَآءَۚ فَلَا تَخۡشَوُاْ ٱلنَّاسَ وَٱخۡشَوۡنِ وَلَا تَشۡتَرُواْ بِـَٔايَٰتِي ثَمَنٗا قَلِيلٗاۚ وَمَن لَّمۡ يَحۡكُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَٰفِرُونَ

Hakika, sisi tumeiteremsha Taurati (ambayo) ndani yake kuna muongozo na nuru. Wanahukumu kwayo Manabii ambao wamejisalimisha (kwa Allah) wakiwahukumu Wayahudi. Na pia (wanahukumu kwa Taurati hiyo) wachamungu (wa Kiyahudi) na wanazuoni (wa Kiyahudi), kwa sababu ya kitabu cha Allah walichotakiwa kukilinda na wakawa mashahidi juu ya hilo. Basi msiwaogope watu na niogopeni Mimi. Na msinunue (msibadilishe) Aya zangu kwa thamani chache. Na wasiohukumu kwa (sheria) aliyoiteremsha Allah, basi hao ndio makafiri[1]


1- - Aya hapa inawahusu wenye mamlaka ya utekelezaji wa hukumu na sio kila mtu anahusika. Pia baadhi ya watu wanaichukua Aya hii kwamba ni hoja ya kumtuhumu kuwa ni kafiri kila atendaye dhambi. Watu wa Suna (Ahlu Sunna Wal Jamaa) wanamhesabu mtu ni kafiri endapo atayakataa yaliyomo ndani ya Qur’ani kwa moyo wake na mdomo wake. Ama anayeamini kwa moyo wake na kutamka kwa mdomo wake kwamba yaliyomo ndani ya Qur’ani ni maneno ya Allah na ni sahihi ila tu hatekelezi kwa vitendo huyu haingii katika hukumu ya ukafiri.


Sura: AL-MAIDA 

Aya : 45

وَكَتَبۡنَا عَلَيۡهِمۡ فِيهَآ أَنَّ ٱلنَّفۡسَ بِٱلنَّفۡسِ وَٱلۡعَيۡنَ بِٱلۡعَيۡنِ وَٱلۡأَنفَ بِٱلۡأَنفِ وَٱلۡأُذُنَ بِٱلۡأُذُنِ وَٱلسِّنَّ بِٱلسِّنِّ وَٱلۡجُرُوحَ قِصَاصٞۚ فَمَن تَصَدَّقَ بِهِۦ فَهُوَ كَفَّارَةٞ لَّهُۥۚ وَمَن لَّمۡ يَحۡكُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ

Na humo (ndani ya Taurati) tumewaandikia ya kwamba, roho kwa roho na jicho kwa jicho na pua kwa pua na sikio kwa sikio na jino kwa jino na majeraha ni kisasi. Basi atakayetoa sadaka (ya kusamehe haki yake kulipa kisasi) hiyo ni kafara yake (ya madhambi yake). Na wasiohukumu kwa (sheria) aliyoiteremsha Allah, basi hao ndio madhalimu



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 46

وَقَفَّيۡنَا عَلَىٰٓ ءَاثَٰرِهِم بِعِيسَى ٱبۡنِ مَرۡيَمَ مُصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيۡهِ مِنَ ٱلتَّوۡرَىٰةِۖ وَءَاتَيۡنَٰهُ ٱلۡإِنجِيلَ فِيهِ هُدٗى وَنُورٞ وَمُصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيۡهِ مِنَ ٱلتَّوۡرَىٰةِ وَهُدٗى وَمَوۡعِظَةٗ لِّلۡمُتَّقِينَ

Na tuliwafuatishia kwa (ku-wapelekea) Issa bin Mariamu akiisadikisha Taurati iliyokuwepo kabla yake, na tukampa Injili (ambayo) ndani yake kuna muon-gozo na nuru na ikisadikisha Taurati iliyokuwepo kabla yake na ni muongozo na mawaidha kwa wacha Mungu



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 47

وَلۡيَحۡكُمۡ أَهۡلُ ٱلۡإِنجِيلِ بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فِيهِۚ وَمَن لَّمۡ يَحۡكُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡفَٰسِقُونَ

Na wahukumu Watu wa Injili kwa sheria alizoziteremsha Allah humo. Na wasiohukumu kwa (sheria) aliyoiteremsha Allah basi hao ndio waovu



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 48

وَأَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ بِٱلۡحَقِّ مُصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيۡهِ مِنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَمُهَيۡمِنًا عَلَيۡهِۖ فَٱحۡكُم بَيۡنَهُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُۖ وَلَا تَتَّبِعۡ أَهۡوَآءَهُمۡ عَمَّا جَآءَكَ مِنَ ٱلۡحَقِّۚ لِكُلّٖ جَعَلۡنَا مِنكُمۡ شِرۡعَةٗ وَمِنۡهَاجٗاۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَعَلَكُمۡ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ وَلَٰكِن لِّيَبۡلُوَكُمۡ فِي مَآ ءَاتَىٰكُمۡۖ فَٱسۡتَبِقُواْ ٱلۡخَيۡرَٰتِۚ إِلَى ٱللَّهِ مَرۡجِعُكُمۡ جَمِيعٗا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ فِيهِ تَخۡتَلِفُونَ

Na tumekuteremshia Kitabu kwa haki kikisadikisha vitabu vilivyokuwepo kabla yake na kikivitawala. Basi hukumu baina yao kwa (sheria) aliyokuteremshia Allah, na usifuate utashi wa nafsi zao ukaacha haki iliyokujia. Kila kundi katika nyinyi tumeliwekea sharia na njia. Na lau Allah angelitaka angekufanyeni (nyote) umma mmoja, lakini (amefanya hivyo) ili akujaribuni katika aliyokupeni. Basi shindaneni kwa mambo ya kheri. Kwa Allah tu ndio marejeo yenu nyote, na atakuambieni yale mliyokuwa mkitofautiana



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 49

وَأَنِ ٱحۡكُم بَيۡنَهُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَلَا تَتَّبِعۡ أَهۡوَآءَهُمۡ وَٱحۡذَرۡهُمۡ أَن يَفۡتِنُوكَ عَنۢ بَعۡضِ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ إِلَيۡكَۖ فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَٱعۡلَمۡ أَنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُصِيبَهُم بِبَعۡضِ ذُنُوبِهِمۡۗ وَإِنَّ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلنَّاسِ لَفَٰسِقُونَ

Na hukumu baina yao kwa (sheria) aliyoiteremsha Allah, na usifuate utashi wa nafsi zao, na jihadhari nao wasije kukufitini[1] ukaacha baadhi ya aliyokuteremshia Allah. Na wakigeuka, basi jua kwamba, hakika Allah anataka kuwaadhibu kwa (sababu ya) baadhi ya dhambi zao. Na kwa hakika kabisa watu wengi ni waovu


1- - Kukupotosha na kujikuta unafuata na kutekeleza wayatakayo wao.


Sura: AL-MAIDA 

Aya : 50

أَفَحُكۡمَ ٱلۡجَٰهِلِيَّةِ يَبۡغُونَۚ وَمَنۡ أَحۡسَنُ مِنَ ٱللَّهِ حُكۡمٗا لِّقَوۡمٖ يُوقِنُونَ

Je, ni hukumu za Kijahiliya tu wanazozitaka? Na ni nani mwenye sheria nzuri zaidi kuliko Allah, kwa watu wenye yakini?



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 51

۞يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُواْ ٱلۡيَهُودَ وَٱلنَّصَٰرَىٰٓ أَوۡلِيَآءَۘ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلِيَآءُ بَعۡضٖۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمۡ فَإِنَّهُۥ مِنۡهُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Enyi mlioamini, msiwafanye Wayahudi na Wanaswara marafiki wa ndani. Wao ni marafiki wa ndani wa wao kwa wao. Na yeyote mwenye kufanya urafiki nao wa ndani miongoni mwenu, basi huyo ni katika wao. Hakika, Allah hawaongoi watu madhalimu



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 52

فَتَرَى ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ يُسَٰرِعُونَ فِيهِمۡ يَقُولُونَ نَخۡشَىٰٓ أَن تُصِيبَنَا دَآئِرَةٞۚ فَعَسَى ٱللَّهُ أَن يَأۡتِيَ بِٱلۡفَتۡحِ أَوۡ أَمۡرٖ مِّنۡ عِندِهِۦ فَيُصۡبِحُواْ عَلَىٰ مَآ أَسَرُّواْ فِيٓ أَنفُسِهِمۡ نَٰدِمِينَ

Basi utawaona ambao ndani ya nyoyo zao kuna maradhi (ya unafiki) wanawakimbilia (Wayahudi na makafiri kwa jumla na kujipendekeza kwao) wakisema: Tunahofu yasije kutupata masaibu (matatizo) yanayojirudia. Basi huenda Allah akaleta ukombozi au jambo jingine kutoka kwake na kwa sababu hiyo wakawa wenye kujuta kwa sababu ya waliyoyaficha katika nafsi zao



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 53

وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَهَـٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ أَقۡسَمُواْ بِٱللَّهِ جَهۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡ إِنَّهُمۡ لَمَعَكُمۡۚ حَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡ فَأَصۡبَحُواْ خَٰسِرِينَ

Na walioamini wanasema: Hivi hawa ndio wale walioapa kwa ukomo wa viapo vyao kwamba wao, kwa yakini kabisa, wapo pamoja nanyi? Vitendo vyao vimepotea bure, na, kwasababu hiyo, wamekuwa wenye hasara



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 54

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَن يَرۡتَدَّ مِنكُمۡ عَن دِينِهِۦ فَسَوۡفَ يَأۡتِي ٱللَّهُ بِقَوۡمٖ يُحِبُّهُمۡ وَيُحِبُّونَهُۥٓ أَذِلَّةٍ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ يُجَٰهِدُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوۡمَةَ لَآئِمٖۚ ذَٰلِكَ فَضۡلُ ٱللَّهِ يُؤۡتِيهِ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٌ

Enyi mlioamini, yeyote ataka-yeritadi miongoni mwenu kwa kuiacha Dini yake (ya Uislamu), basi Allah ataleta watu anaowapenda nao wanampenda, wanyenyekevu mno kwa waumini (wenzao) na wenye nguvu sana mbele ya makafiri, wanapigania Jihadi katika Njia ya Allah, na hawaogopi lawama za mwenye kulaumu. Hizo ni fadhila za Allah humpa amtakaye. Na Allah ni Mkunjufu, Mwenye kujua sana



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 55

إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱلَّذِينَ يُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَهُمۡ رَٰكِعُونَ

Hakika ilivyo ni kwamba, Mwandani wenu ni Allah na Mtume wake na walioamini, ambao wanasimamisha Swala na wanatoa Zaka na ilhali ni wanyenyekevu



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 56

وَمَن يَتَوَلَّ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فَإِنَّ حِزۡبَ ٱللَّهِ هُمُ ٱلۡغَٰلِبُونَ

Na yeyote anayemfanya Mwandani Allah na Mtume wake na walioamini, basi hakika kundi la Allah ndilo lenye kushinda



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 57

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُواْ ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ دِينَكُمۡ هُزُوٗا وَلَعِبٗا مِّنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِكُمۡ وَٱلۡكُفَّارَ أَوۡلِيَآءَۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Enyi mlioamini, msiwafanye marafiki wa ndani wale walioifanyia kejeli na dhihaka Dini yenu ikiwa ni pamoja[1] na wale waliopewa Kitabu kabla yenu na makafiri (wengine). Na mcheni Allah kama nyinyi ni waumini (wa kweli)


1- - Hapa Aya inafundisha kuwa inaposomwa Adhana watu wanatakiwa waiheshimu nembo hii ya Uislamu. Kuipuuza Adhana ni dalili ya kutokuwa na ukomavu wa busara na akili kwa mujibu wa Aya hii. Kwa makusudi tunawapongeza wote wanaoheshimu nembo hii.


Sura: AL-MAIDA 

Aya : 58

وَإِذَا نَادَيۡتُمۡ إِلَى ٱلصَّلَوٰةِ ٱتَّخَذُوهَا هُزُوٗا وَلَعِبٗاۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَوۡمٞ لَّا يَعۡقِلُونَ

Na mnapoita (watu) kwenye Swala wanaifanyia masihara na mchezo. Hiyo ni kwa sababu wao ni watu wasiotumia akili



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 59

قُلۡ يَـٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ هَلۡ تَنقِمُونَ مِنَّآ إِلَّآ أَنۡ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيۡنَا وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبۡلُ وَأَنَّ أَكۡثَرَكُمۡ فَٰسِقُونَ

Sema: Enyi Watu wa Kitabu, hivi mnatunyanyasa kwa sababu tu tumemuamini Allah na tuliyo-teremshiwa na yaliyoteremshwa kabla, na kwamba wengi wenu ni waovu?



Sura: AL-MAIDA 

Aya : 60

قُلۡ هَلۡ أُنَبِّئُكُم بِشَرّٖ مِّن ذَٰلِكَ مَثُوبَةً عِندَ ٱللَّهِۚ مَن لَّعَنَهُ ٱللَّهُ وَغَضِبَ عَلَيۡهِ وَجَعَلَ مِنۡهُمُ ٱلۡقِرَدَةَ وَٱلۡخَنَازِيرَ وَعَبَدَ ٱلطَّـٰغُوتَۚ أُوْلَـٰٓئِكَ شَرّٞ مَّكَانٗا وَأَضَلُّ عَن سَوَآءِ ٱلسَّبِيلِ

Sema: Je, nikuambieni yule aliye na malipo mabaya zaidi kuliko hayo mbele ya Allah? Ni yule aliyelaaniwa na kukasirikiwa na Allah kuwafanya miongoni mwao nyani na nguruwe na waabudu Twaghuti. Hao ndio wenye mahali pabaya mno na wamepotea kabisa njia ya sawa