Sura: YUSUF 

Aya : 31

فَلَمَّا سَمِعَتۡ بِمَكۡرِهِنَّ أَرۡسَلَتۡ إِلَيۡهِنَّ وَأَعۡتَدَتۡ لَهُنَّ مُتَّكَـٔٗا وَءَاتَتۡ كُلَّ وَٰحِدَةٖ مِّنۡهُنَّ سِكِّينٗا وَقَالَتِ ٱخۡرُجۡ عَلَيۡهِنَّۖ فَلَمَّا رَأَيۡنَهُۥٓ أَكۡبَرۡنَهُۥ وَقَطَّعۡنَ أَيۡدِيَهُنَّ وَقُلۡنَ حَٰشَ لِلَّهِ مَا هَٰذَا بَشَرًا إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا مَلَكٞ كَرِيمٞ

Basi (mke wa mheshimiwa) aliposikia vitimbi vyao (na wanavyomshutumu) aliwatumia mwaliko na akawaandalia mito ya kuegemea na kila mmoja wao akampa kisu na akasema (kumwambia Yusuf:) Tokeza mbele yao. Basi (wale wanawake) walipomuona (Yusuf) tu walimuona (Yusufu) ni habari kubwa mno na walijikatakata mikono yao na kusema (kwa mshangao): Allah apishe mbali! Huyu (kijana) si binadamu. Hakuwa huyu (kijana) isipokuwa ni Malaika mtukufu



Sura: YUSUF 

Aya : 32

قَالَتۡ فَذَٰلِكُنَّ ٱلَّذِي لُمۡتُنَّنِي فِيهِۖ وَلَقَدۡ رَٰوَدتُّهُۥ عَن نَّفۡسِهِۦ فَٱسۡتَعۡصَمَۖ وَلَئِن لَّمۡ يَفۡعَلۡ مَآ ءَامُرُهُۥ لَيُسۡجَنَنَّ وَلَيَكُونٗا مِّنَ ٱلصَّـٰغِرِينَ

(Yule mke wa mheshimiwa) akasema: Basi huyo ndiye yule mliyenilaumu kwasababu yake! Na kwakweli mimi nilimtongoza bila ya ridhaa yake na alikataa (katakata). Na (nilimwambia kuwa) asipofanya ninacho muamuru basi hapana shaka atafungwa tu gerezani na atakuwa miongoni mwa watu duni kabisa



Sura: YUSUF 

Aya : 33

قَالَ رَبِّ ٱلسِّجۡنُ أَحَبُّ إِلَيَّ مِمَّا يَدۡعُونَنِيٓ إِلَيۡهِۖ وَإِلَّا تَصۡرِفۡ عَنِّي كَيۡدَهُنَّ أَصۡبُ إِلَيۡهِنَّ وَأَكُن مِّنَ ٱلۡجَٰهِلِينَ

(Yusuf) Alisema: “Ewe Mola wangu Mlezi, napenda zaidi kufungwa gerezani kuliko hili (hawa wanawake) wanaloniitia. Na usiponiondoshea vitimbi vyao (hawa wanawake) mimi nitavutika kwao na nitakuwa miongoni mwa wajinga



Sura: YUSUF 

Aya : 34

فَٱسۡتَجَابَ لَهُۥ رَبُّهُۥ فَصَرَفَ عَنۡهُ كَيۡدَهُنَّۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Basi Mola wake Mlezi alimuitikia (dua yake), na akamuondoshea vitimbi vyao. Hakika Yeye (Allah) ndiye Msikivu (na) Mjuzi



Sura: YUSUF 

Aya : 35

ثُمَّ بَدَا لَهُم مِّنۢ بَعۡدِ مَا رَأَوُاْ ٱلۡأٓيَٰتِ لَيَسۡجُنُنَّهُۥ حَتَّىٰ حِينٖ

Kisha ikawadhihirikia (Mheshimiwa na wasaidizi wake) baada ya kuona ishara mbalimbali (za kutohusika kwa Yusuf) kuwa wamfunge kwa muda[1]


1- - Iliamuliwa kwamba, Yusuf afungwe kwa muda usiojulikana ili gumzo la kutaka kubaka liishe na kadhia hii ya kashfa isahaulike.


Sura: YUSUF 

Aya : 36

وَدَخَلَ مَعَهُ ٱلسِّجۡنَ فَتَيَانِۖ قَالَ أَحَدُهُمَآ إِنِّيٓ أَرَىٰنِيٓ أَعۡصِرُ خَمۡرٗاۖ وَقَالَ ٱلۡأٓخَرُ إِنِّيٓ أَرَىٰنِيٓ أَحۡمِلُ فَوۡقَ رَأۡسِي خُبۡزٗا تَأۡكُلُ ٱلطَّيۡرُ مِنۡهُۖ نَبِّئۡنَا بِتَأۡوِيلِهِۦٓۖ إِنَّا نَرَىٰكَ مِنَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Na wakaingia gerezani pamoja naye vijana wawili. Mmoja wao alisema: Hakika, mimi nimeota nakamua (zabibu ili kutengeneza) pombe. Na mwingine akasema: Mimi nimeota nimebeba mkate kichwani kwangu (ambao) ndege wanaula. Hebu tuambie tafsiri yake, kwani sisi tunakuona wewe ni katika wenye kufanya mazuri (ikiwemo kutafsiri vizuri ndoto)



Sura: YUSUF 

Aya : 37

قَالَ لَا يَأۡتِيكُمَا طَعَامٞ تُرۡزَقَانِهِۦٓ إِلَّا نَبَّأۡتُكُمَا بِتَأۡوِيلِهِۦ قَبۡلَ أَن يَأۡتِيَكُمَاۚ ذَٰلِكُمَا مِمَّا عَلَّمَنِي رَبِّيٓۚ إِنِّي تَرَكۡتُ مِلَّةَ قَوۡمٖ لَّا يُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَهُم بِٱلۡأٓخِرَةِ هُمۡ كَٰفِرُونَ

(Yusuf) Alisema: Hakitakufikieni chakula chochote mtakachopewa (na Mfalme) ila tu nitakwambieni tafsiri yake kabla hakijakufikieni. Haya ni katika yale aliyonifundisha Mola wangu Mlezi. Hakika, mimi niliacha mila (dini) za watu wasiomuamini Allah na wasioiamini Akhera



Sura: YUSUF 

Aya : 38

وَٱتَّبَعۡتُ مِلَّةَ ءَابَآءِيٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَۚ مَا كَانَ لَنَآ أَن نُّشۡرِكَ بِٱللَّهِ مِن شَيۡءٖۚ ذَٰلِكَ مِن فَضۡلِ ٱللَّهِ عَلَيۡنَا وَعَلَى ٱلنَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَشۡكُرُونَ

Na nilifuata mila (dini) ya Baba zangu, Ibrahim na Is-hak na Yakubu. Sisi hatukuwa na haki ya kumshirikisha Allah kwa chochote. Hayo ni katika fadhila za Allah kwetu na kwa watu (wengine) lakini watu wengi sana hawashukuru



Sura: YUSUF 

Aya : 39

يَٰصَٰحِبَيِ ٱلسِّجۡنِ ءَأَرۡبَابٞ مُّتَفَرِّقُونَ خَيۡرٌ أَمِ ٱللَّهُ ٱلۡوَٰحِدُ ٱلۡقَهَّارُ

Enyi swahiba zangu wawili wafungwa (mlio gerezani): Je, mabwana (Miungu) wengi tofauti tofauti ni bora au Allah Mmoja, Mwenye nguvu kubwa?



Sura: YUSUF 

Aya : 40

مَا تَعۡبُدُونَ مِن دُونِهِۦٓ إِلَّآ أَسۡمَآءٗ سَمَّيۡتُمُوهَآ أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلۡطَٰنٍۚ إِنِ ٱلۡحُكۡمُ إِلَّا لِلَّهِ أَمَرَ أَلَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّآ إِيَّاهُۚ ذَٰلِكَ ٱلدِّينُ ٱلۡقَيِّمُ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ

(Nyinyi) Hamuabudu badala yake (Allah) ila majina tu mliyoyaita nyinyi na Baba zenu (kuwa ni Miungu). Allah hakuyateremshia majina hayo hoja yoyote. Hapana hukumu ila ya Allah tu. Ameamrisha msimuabudu yeyote isipokuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo Dini sahihi lakini watu wengi hawajui



Sura: YUSUF 

Aya : 41

يَٰصَٰحِبَيِ ٱلسِّجۡنِ أَمَّآ أَحَدُكُمَا فَيَسۡقِي رَبَّهُۥ خَمۡرٗاۖ وَأَمَّا ٱلۡأٓخَرُ فَيُصۡلَبُ فَتَأۡكُلُ ٱلطَّيۡرُ مِن رَّأۡسِهِۦۚ قُضِيَ ٱلۡأَمۡرُ ٱلَّذِي فِيهِ تَسۡتَفۡتِيَانِ

Enyi wafungwa wenzangu wawili (hii hapa tafsiri ya ndoto zenu). Ama mmoja wenu (muhudumu atarejea kazini na) atamnywesha bwana wake ulevi. Na ama mwengine atasulubiwa (mpaka kufa), na ndege watadonoa kichwa chake. Ilikwishakatwa hukumu ya hilo jambo mlilokuwa mnaliulizia



Sura: YUSUF 

Aya : 42

وَقَالَ لِلَّذِي ظَنَّ أَنَّهُۥ نَاجٖ مِّنۡهُمَا ٱذۡكُرۡنِي عِندَ رَبِّكَ فَأَنسَىٰهُ ٱلشَّيۡطَٰنُ ذِكۡرَ رَبِّهِۦ فَلَبِثَ فِي ٱلسِّجۡنِ بِضۡعَ سِنِينَ

Na (Yusuf) alimwambia yule aliyehisi kuwa atasalimika katika wale (wafungwa) wawili (kwamba): Nikumbuke kwa bwana wako (na umwambie nimefungwa bila hatia). Lakini Shetani alimsahaulisha kumtaja kwa bwana wake. Basi (Yusuf) alikaa gerezani miaka kadhaa



Sura: YUSUF 

Aya : 43

وَقَالَ ٱلۡمَلِكُ إِنِّيٓ أَرَىٰ سَبۡعَ بَقَرَٰتٖ سِمَانٖ يَأۡكُلُهُنَّ سَبۡعٌ عِجَافٞ وَسَبۡعَ سُنۢبُلَٰتٍ خُضۡرٖ وَأُخَرَ يَابِسَٰتٖۖ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلۡمَلَأُ أَفۡتُونِي فِي رُءۡيَٰيَ إِن كُنتُمۡ لِلرُّءۡيَا تَعۡبُرُونَ

Na (siku moja) mfalme (Mkuu wa Misri) alisema: Hakika mimi nimeota ng’ombe saba wanene wanaliwa na ng’ombe saba waliokonda. Na (nimeota) mashuke saba mabichi na mengine makavu. Enyi wakuu, niambieni maana ya ndoto yangu, ikiwa nyinyi mnaweza kufasiri ndoto



Sura: YUSUF 

Aya : 44

قَالُوٓاْ أَضۡغَٰثُ أَحۡلَٰمٖۖ وَمَا نَحۡنُ بِتَأۡوِيلِ ٱلۡأَحۡلَٰمِ بِعَٰلِمِينَ

Walisema: Hizi ni ndoto za hovyo, na wala sisi sio wenye kujua kutafsiri ndoto za aina hii



Sura: YUSUF 

Aya : 45

وَقَالَ ٱلَّذِي نَجَا مِنۡهُمَا وَٱدَّكَرَ بَعۡدَ أُمَّةٍ أَنَا۠ أُنَبِّئُكُم بِتَأۡوِيلِهِۦ فَأَرۡسِلُونِ

Na alisema yule (mhudumu) aliyenusurika kati ya wale (wafungwa) wawili na alikumbuka (kuwa alitumwa na Yusuf) baada ya muda: Mimi nitakwambieni tafsiri yake (kwa kumuuliza mjuzi). Basi nitumeni (nikamuulize mjuzi)



Sura: YUSUF 

Aya : 46

يُوسُفُ أَيُّهَا ٱلصِّدِّيقُ أَفۡتِنَا فِي سَبۡعِ بَقَرَٰتٖ سِمَانٖ يَأۡكُلُهُنَّ سَبۡعٌ عِجَافٞ وَسَبۡعِ سُنۢبُلَٰتٍ خُضۡرٖ وَأُخَرَ يَابِسَٰتٖ لَّعَلِّيٓ أَرۡجِعُ إِلَى ٱلنَّاسِ لَعَلَّهُمۡ يَعۡلَمُونَ

(Baada ya kutumwa alikwenda kwa Yusuf na kumwambia): Ewe Yusuf, mkweli sana, tupe Fatwa kuhusu maana ya ng’ombe saba wanene kuliwa na ng’ombe saba waliokonda. Na (tupe Fatwa ya) mashuke saba mabichi na mengine makavu, ili nirejee kwa watu wapate kujua (hadhi yako ili utoke)



Sura: YUSUF 

Aya : 47

قَالَ تَزۡرَعُونَ سَبۡعَ سِنِينَ دَأَبٗا فَمَا حَصَدتُّمۡ فَذَرُوهُ فِي سُنۢبُلِهِۦٓ إِلَّا قَلِيلٗا مِّمَّا تَأۡكُلُونَ

(Yusuf) Alisema: Mtalima miaka saba mfululizo[1]. Mtakachovuna kiacheni katika mashuke yake, isipokuwa kidogo mtakachokula


1- - Na hii ndio tafsiri ya ng’ombe saba walionona na mashuke saba mabichi


Sura: YUSUF 

Aya : 48

ثُمَّ يَأۡتِي مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ سَبۡعٞ شِدَادٞ يَأۡكُلۡنَ مَا قَدَّمۡتُمۡ لَهُنَّ إِلَّا قَلِيلٗا مِّمَّا تُحۡصِنُونَ

Kisha baada ya miaka saba itakuja miaka (mingine) ya shida[1] (ambapo watu) watakula kile walichokihifadhi isipokuwa kidogo mlichokihifadhi (kwa ajili ya mbegu)


1- - Na hii ndio tafsiri ya wale ng’ombe waliokondeana


Sura: YUSUF 

Aya : 49

ثُمَّ يَأۡتِي مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ عَامٞ فِيهِ يُغَاثُ ٱلنَّاسُ وَفِيهِ يَعۡصِرُونَ

Kisha itakuja baada ya hapo (miaka saba ya neema) mwaka (ambao) katika mwaka huo watu wataokolewa (kwa kuletewa mvua ya neema) na katika mwaka huo watakamua (yale mazao yakamuliwayo)



Sura: YUSUF 

Aya : 50

وَقَالَ ٱلۡمَلِكُ ٱئۡتُونِي بِهِۦۖ فَلَمَّا جَآءَهُ ٱلرَّسُولُ قَالَ ٱرۡجِعۡ إِلَىٰ رَبِّكَ فَسۡـَٔلۡهُ مَا بَالُ ٱلنِّسۡوَةِ ٱلَّـٰتِي قَطَّعۡنَ أَيۡدِيَهُنَّۚ إِنَّ رَبِّي بِكَيۡدِهِنَّ عَلِيمٞ

Na mfalme alisema: Nileteeni huyo (Yusuf). Basi mjumbe alipomjia (Yusuf) alisema: Rejea kwa bwana wako na muulize: Vipi kadhia ya wale wanawake waliojikatakata mikono yao? Hakika, Mola wangu Mlezi anazijua vyema hila zao



Sura: YUSUF 

Aya : 51

قَالَ مَا خَطۡبُكُنَّ إِذۡ رَٰوَدتُّنَّ يُوسُفَ عَن نَّفۡسِهِۦۚ قُلۡنَ حَٰشَ لِلَّهِ مَا عَلِمۡنَا عَلَيۡهِ مِن سُوٓءٖۚ قَالَتِ ٱمۡرَأَتُ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡـَٰٔنَ حَصۡحَصَ ٱلۡحَقُّ أَنَا۠ رَٰوَدتُّهُۥ عَن نَّفۡسِهِۦ وَإِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ

(Mfalme) Alisema (akiwauliza wale wanawake): Mlikuwa na kadhia gani mlipomtongoza Yusuf bila ya ridhaa yake? Walisema: “Allah apishe mbali! Sisi hatukujua baya lolote kwake”. Mke wa Mheshimiwa alisema: Sasa haki imedhihiri (acha niseme kweli). Mimi ndiye niliyemtongoza (Yusuf) bila ya ridhaa yake na hakika yeye ni katika wakweli



Sura: YUSUF 

Aya : 52

ذَٰلِكَ لِيَعۡلَمَ أَنِّي لَمۡ أَخُنۡهُ بِٱلۡغَيۡبِ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي كَيۡدَ ٱلۡخَآئِنِينَ

(Yusuf alisema): Hayo (nimeyaombea ufafanuzi) ili (Mheshimiwa) apate kujua ya kwamba mimi sikudhamiria kumfanyia khiyana wakati hayupo na ya kwamba Allah haziongozi hila za watu wenye khiyana



Sura: YUSUF 

Aya : 53

۞وَمَآ أُبَرِّئُ نَفۡسِيٓۚ إِنَّ ٱلنَّفۡسَ لَأَمَّارَةُۢ بِٱلسُّوٓءِ إِلَّا مَا رَحِمَ رَبِّيٓۚ إِنَّ رَبِّي غَفُورٞ رَّحِيمٞ

(Yusuf aliendelea kusema) Nami siisafishi nafsi yangu (sijitoi lawamani). Kwa hakika nafsi inaamrisha mno maovu, isipokuwa ile tu aliyoirehemu Mola wangu Mlezi. Hakika, Mola wangu Mlezi ni Msamehevu, mwingi wa rehema



Sura: YUSUF 

Aya : 54

وَقَالَ ٱلۡمَلِكُ ٱئۡتُونِي بِهِۦٓ أَسۡتَخۡلِصۡهُ لِنَفۡسِيۖ فَلَمَّا كَلَّمَهُۥ قَالَ إِنَّكَ ٱلۡيَوۡمَ لَدَيۡنَا مَكِينٌ أَمِينٞ

Na mfalme alisema: Nileteeni, awe msaidizi wangu binafsi. Basi (mfalme) alipomsemeza (Yusuf alibaini kipawa chake na) alinena: Hakika wewe leo umemakinika kwetu na umeaminika



Sura: YUSUF 

Aya : 55

قَالَ ٱجۡعَلۡنِي عَلَىٰ خَزَآئِنِ ٱلۡأَرۡضِۖ إِنِّي حَفِيظٌ عَلِيمٞ

(Yusuf) Alisema: Nifanye mtunza hazina za nchi. Kwani hakika mimi ni (mshika hazina) mlinzi mahiri sana, mjuzi sana



Sura: YUSUF 

Aya : 56

وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي ٱلۡأَرۡضِ يَتَبَوَّأُ مِنۡهَا حَيۡثُ يَشَآءُۚ نُصِيبُ بِرَحۡمَتِنَا مَن نَّشَآءُۖ وَلَا نُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Na kama hivyo tulimmakinisha Yusuf (na kumpa cheo katika nchi); akawa anakaa humo popote anapopenda. Tunamfikishia rehema zetu tumtakaye, na hatupotezi malipo ya wafanyao mazuri



Sura: YUSUF 

Aya : 57

وَلَأَجۡرُ ٱلۡأٓخِرَةِ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَكَانُواْ يَتَّقُونَ

Na kwa hakika kabisa, malipo ya Akhera ni bora zaidi kwa walioamini na wakawa wanamcha Allah



Sura: YUSUF 

Aya : 58

وَجَآءَ إِخۡوَةُ يُوسُفَ فَدَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَعَرَفَهُمۡ وَهُمۡ لَهُۥ مُنكِرُونَ

Na walikuja (wale) ndugu wa Yusuf na wakaingia kwake; akawajua na wao hawakumjua



Sura: YUSUF 

Aya : 59

وَلَمَّا جَهَّزَهُم بِجَهَازِهِمۡ قَالَ ٱئۡتُونِي بِأَخٖ لَّكُم مِّنۡ أَبِيكُمۡۚ أَلَا تَرَوۡنَ أَنِّيٓ أُوفِي ٱلۡكَيۡلَ وَأَنَا۠ خَيۡرُ ٱلۡمُنزِلِينَ

Na alipowatimizia mahitaji yao (ya shehena ya chakula) alisema: (mtakapokuja mara nyingine) Nileteeni ndugu yenu kwa (upande wa) Baba yenu. Je, hamuoni ya kwamba mimi ninatimiza kipimo, nami ni mbora wa wakarimu?



Sura: YUSUF 

Aya : 60

فَإِن لَّمۡ تَأۡتُونِي بِهِۦ فَلَا كَيۡلَ لَكُمۡ عِندِي وَلَا تَقۡرَبُونِ

Na msiponiletea (ndugu yenu wa Baba mmoja) basi (mjue) hampati kipimo chochote kwangu na wala msinisogelee