سوره: AL-INFITWAAR 

آيه : 1

إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنفَطَرَتۡ

Mbingu itakapo chanika,



سوره: AL-INFITWAAR 

آيه : 2

وَإِذَا ٱلۡكَوَاكِبُ ٱنتَثَرَتۡ

Na nyota zitakapo tawanyika,



سوره: AL-INFITWAAR 

آيه : 3

وَإِذَا ٱلۡبِحَارُ فُجِّرَتۡ

Na bahari zitakapo pasuliwa,



سوره: AL-INFITWAAR 

آيه : 4

وَإِذَا ٱلۡقُبُورُ بُعۡثِرَتۡ

Na makaburi yatakapo fukuliwa,



سوره: AL-INFITWAAR 

آيه : 5

عَلِمَتۡ نَفۡسٞ مَّا قَدَّمَتۡ وَأَخَّرَتۡ

Hapo kila nafsi itajua ilichotanguliza, na ilicho bakisha nyuma



سوره: AL-INFITWAAR 

آيه : 6

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلۡإِنسَٰنُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ ٱلۡكَرِيمِ

Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu?



سوره: AL-INFITWAAR 

آيه : 7

ٱلَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّىٰكَ فَعَدَلَكَ

Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha,



سوره: AL-INFITWAAR 

آيه : 8

فِيٓ أَيِّ صُورَةٖ مَّا شَآءَ رَكَّبَكَ

Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga



سوره: AL-INFITWAAR 

آيه : 9

كَلَّا بَلۡ تُكَذِّبُونَ بِٱلدِّينِ

Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo



سوره: AL-INFITWAAR 

آيه : 10

وَإِنَّ عَلَيۡكُمۡ لَحَٰفِظِينَ

Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu,



سوره: AL-INFITWAAR 

آيه : 11

كِرَامٗا كَٰتِبِينَ

Waandishi wenye hishima,



سوره: AL-INFITWAAR 

آيه : 12

يَعۡلَمُونَ مَا تَفۡعَلُونَ

Wanayajua mnayo yatenda



سوره: AL-INFITWAAR 

آيه : 13

إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ لَفِي نَعِيمٖ

Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema,



سوره: AL-INFITWAAR 

آيه : 14

وَإِنَّ ٱلۡفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٖ

Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni;



سوره: AL-INFITWAAR 

آيه : 15

يَصۡلَوۡنَهَا يَوۡمَ ٱلدِّينِ

Wataingia humo Siku ya Malipo



سوره: AL-INFITWAAR 

آيه : 16

وَمَا هُمۡ عَنۡهَا بِغَآئِبِينَ

Na hawatoacha kuwamo humo



سوره: AL-INFITWAAR 

آيه : 17

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ

Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?



سوره: AL-INFITWAAR 

آيه : 18

ثُمَّ مَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ

Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?



سوره: AL-INFITWAAR 

آيه : 19

يَوۡمَ لَا تَمۡلِكُ نَفۡسٞ لِّنَفۡسٖ شَيۡـٔٗاۖ وَٱلۡأَمۡرُ يَوۡمَئِذٖ لِّلَّهِ

(Ni) Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu