سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 1

وَٱلۡمُرۡسَلَٰتِ عُرۡفٗا

Nina apa kwa pepo zitumwazo kwa mfuatano



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 2

فَٱلۡعَٰصِفَٰتِ عَصۡفٗا

Kisha zinazovuma kwa kasi!



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 3

وَٱلنَّـٰشِرَٰتِ نَشۡرٗا

Na kwa pepo zinazotawanya (mawingu na mvua)



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 4

فَٱلۡفَٰرِقَٰتِ فَرۡقٗا

Kisha Nina apa kwa (Malaika) wanaopambanua haki na batili



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 5

فَٱلۡمُلۡقِيَٰتِ ذِكۡرًا

Kisha kwa (Malaika) wanaopeleka Wahyi (kwa Mtume)



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 6

عُذۡرًا أَوۡ نُذۡرًا

Kwa ajili ya kuondosha udhuru au kwa ajili ya kuonya



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 7

إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَٰقِعٞ

Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatatokea tu!



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 8

فَإِذَا ٱلنُّجُومُ طُمِسَتۡ

Basi pale nyota zitakapofutiliwa mbali mwanga wake



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 9

وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ فُرِجَتۡ

Na mbingu zitakapo pasuliwa, (au zitakapo funguliwa)



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 10

وَإِذَا ٱلۡجِبَالُ نُسِفَتۡ

Na milima itakapo peperushwa



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 11

وَإِذَا ٱلرُّسُلُ أُقِّتَتۡ

Na Mitume watakapo wekewa wakati wao



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 12

لِأَيِّ يَوۡمٍ أُجِّلَتۡ

Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 13

لِيَوۡمِ ٱلۡفَصۡلِ

Kwa ajili ya Siku ya hukumu na kutenganisha



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 14

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِ

Na nini kitakachokujulisha Siku ya hukumu na kutenganisha?



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 15

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha!



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 16

أَلَمۡ نُهۡلِكِ ٱلۡأَوَّلِينَ

Je, kwani Hatukuangamiza watu walio tangulia?



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 17

ثُمَّ نُتۡبِعُهُمُ ٱلۡأٓخِرِينَ

Kisha Tukawafuatilishia watu wengineo?



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 18

كَذَٰلِكَ نَفۡعَلُ بِٱلۡمُجۡرِمِينَ

Hivyo ndivyo Tunavyo wafanya wakosefu!



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 19

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha!



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 20

أَلَمۡ نَخۡلُقكُّم مِّن مَّآءٖ مَّهِينٖ

Kwani hatukukuumbeni kwa maji dhalili (manii)?



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 21

فَجَعَلۡنَٰهُ فِي قَرَارٖ مَّكِينٍ

Kisha Tukayaweka katika mahali pa kutulia, madhubuti?



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 22

إِلَىٰ قَدَرٖ مَّعۡلُومٖ

Mpaka muda maalumu?



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 23

فَقَدَرۡنَا فَنِعۡمَ ٱلۡقَٰدِرُونَ

Tukakadiria na Sisi ni wazuri walioje wa kukadiria



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 24

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 25

أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ كِفَاتًا

Je, kwani Hatukufanya ardhi kuwa ni chombo cha kukusanya?



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 26

أَحۡيَآءٗ وَأَمۡوَٰتٗا

Walio hai na maiti (na waliokufa)?



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 27

وَجَعَلۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ شَٰمِخَٰتٖ وَأَسۡقَيۡنَٰكُم مَّآءٗ فُرَاتٗا

Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tuna-kunywesheni maji matamu?



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 28

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 29

ٱنطَلِقُوٓاْ إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ

(wataambiwa:) Nendeni kwenye adhabu mliyokuwa mkiikanusha!



سوره: ALMURSALAAT 

آيه : 30

ٱنطَلِقُوٓاْ إِلَىٰ ظِلّٖ ذِي ثَلَٰثِ شُعَبٖ

Nendeni kwenye kivuli chenye sehemu tatu!