سوره: AL-HADIID

آيه : 1

سَبَّحَ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Vimemsabihi (vimemtakasa) Allah na kumtukuza vyote vilivyomo katika mbingu na ardhi na yeye tu ndiye Mwenye nguvu kubwa, Mwenye hekima sana



سوره: AL-HADIID

آيه : 2

لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Ni Wake pekee ufalme wa mbingu na ardhi. Anahuisha na anafisha. Na yeye Muweza wa kila kitu



سوره: AL-HADIID

آيه : 3

هُوَ ٱلۡأَوَّلُ وَٱلۡأٓخِرُ وَٱلظَّـٰهِرُ وَٱلۡبَاطِنُۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٌ

Yeye ndiye wa mwanzo na ndiye wa mwisho na mjuzi wa mambo ya dhahiri na ya siri na yeye ni Mjuzi sana wa kila kitu



سوره: AL-HADIID

آيه : 4

هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ يَعۡلَمُ مَا يَلِجُ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا يَخۡرُجُ مِنۡهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ وَمَا يَعۡرُجُ فِيهَاۖ وَهُوَ مَعَكُمۡ أَيۡنَ مَا كُنتُمۡۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ

Yeye Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Akawa juu (Istawaa)[1] ya ‘Arsh, Anajua yale yanayoingia ardhini, na yale yatokayo humo, na yale yanayoteremka kutoka mbinguni, na yale yanayopanda humo, Naye Yu Pamoja nanyi popote mlipo. Na Allah ni Mwenye kuona yote myatendayo


1- - Faida: Maana ya Istawaa: Yuko juu kabisa kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah. {Rejea Tanbihi (2: 29)}.


سوره: AL-HADIID

آيه : 5

لَّهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَإِلَى ٱللَّهِ تُرۡجَعُ ٱلۡأُمُورُ

Ni Wake Pekee ufalme wa mbingu na ardhi, kwa Allah Pekee yanarejeshwa mambo yote



سوره: AL-HADIID

آيه : 6

يُولِجُ ٱلَّيۡلَ فِي ٱلنَّهَارِ وَيُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِي ٱلَّيۡلِۚ وَهُوَ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Anauingiza usiku katika mchana, na Anaingiza mchana katika usiku, Naye ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani



سوره: AL-HADIID

آيه : 7

ءَامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَأَنفِقُواْ مِمَّا جَعَلَكُم مُّسۡتَخۡلَفِينَ فِيهِۖ فَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنكُمۡ وَأَنفَقُواْ لَهُمۡ أَجۡرٞ كَبِيرٞ

Muaminini Allah na Mtume Wake, na toeni kutokana na yale Aliyokufanyieni kuwa ni waangalizi kwayo. Basi wale walioamini miongoni mwenu, na wakatoa, watapata ujira mkubwa



سوره: AL-HADIID

آيه : 8

وَمَا لَكُمۡ لَا تُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلرَّسُولُ يَدۡعُوكُمۡ لِتُؤۡمِنُواْ بِرَبِّكُمۡ وَقَدۡ أَخَذَ مِيثَٰقَكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Na mna nini nyinyi hamu-muamini Allah, na hali yakuwa Mtume anakuiteni ili mumua-mini Bwana wenu, na hali Amekwi-shachukua ahadi yenu mkiwa nyinyi ni Waumini



سوره: AL-HADIID

آيه : 9

هُوَ ٱلَّذِي يُنَزِّلُ عَلَىٰ عَبۡدِهِۦٓ ءَايَٰتِۭ بَيِّنَٰتٖ لِّيُخۡرِجَكُم مِّنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ بِكُمۡ لَرَءُوفٞ رَّحِيمٞ

Yeye Ndiye Yule Anayemte-remshia mja Wake Aya zinazo bainisha ili Akutoeni katika giza na kukuingizeni kwenye Nuru. Na hakika Allah kwenu ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu



سوره: AL-HADIID

آيه : 10

وَمَا لَكُمۡ أَلَّا تُنفِقُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلِلَّهِ مِيرَٰثُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ لَا يَسۡتَوِي مِنكُم مَّنۡ أَنفَقَ مِن قَبۡلِ ٱلۡفَتۡحِ وَقَٰتَلَۚ أُوْلَـٰٓئِكَ أَعۡظَمُ دَرَجَةٗ مِّنَ ٱلَّذِينَ أَنفَقُواْ مِنۢ بَعۡدُ وَقَٰتَلُواْۚ وَكُلّٗا وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ

Na mna nini hata hamtoi katika njia ya Allah, na hali urithi wa mbingu na ardhi ni wa Allah Pekee. Hawi sawa miongoni mwenu aliyetoa kabla ya Ushindi (wa Makkah) na akapigana. Hao watapata daraja kuu kabisa kuliko wale waliotoa baadae na wakapigana. Na wote Allaah Amewaahidi malipo mazuri kabisa. Na Allah kwa yale myatendayo ni Mwenye khabari nayo



سوره: AL-HADIID

آيه : 11

مَّن ذَا ٱلَّذِي يُقۡرِضُ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنٗا فَيُضَٰعِفَهُۥ لَهُۥ وَلَهُۥٓ أَجۡرٞ كَرِيمٞ

Nani ambaye atamkopesha Allah mkopo mzuri kisha (Allah) Amuongezee maradufu na apate malipo mazuri



سوره: AL-HADIID

آيه : 12

يَوۡمَ تَرَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ يَسۡعَىٰ نُورُهُم بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَبِأَيۡمَٰنِهِمۖ بُشۡرَىٰكُمُ ٱلۡيَوۡمَ جَنَّـٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ

Siku utakayowaona Waumini wa kiume na Waumini wa kike, nuru zao zinakimbilia mbele yao na kuliani kwao; (wataambiwa): Bishara njema kwenu leo! Ya pepo zipitazo chini yake mito, ni wenye kukaa humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa



سوره: AL-HADIID

آيه : 13

يَوۡمَ يَقُولُ ٱلۡمُنَٰفِقُونَ وَٱلۡمُنَٰفِقَٰتُ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱنظُرُونَا نَقۡتَبِسۡ مِن نُّورِكُمۡ قِيلَ ٱرۡجِعُواْ وَرَآءَكُمۡ فَٱلۡتَمِسُواْ نُورٗاۖ فَضُرِبَ بَيۡنَهُم بِسُورٖ لَّهُۥ بَابُۢ بَاطِنُهُۥ فِيهِ ٱلرَّحۡمَةُ وَظَٰهِرُهُۥ مِن قِبَلِهِ ٱلۡعَذَابُ

Siku wanafiki wa kiume na wanafiki wa kike watakapowaambia wale walioamini: Tungojeeni, tupate mwangaza kutokana na nuru yenu! (Wataambiwa): Rudini nyuma yenu, na mtafute huko nuru (yenu)! Kisha utawekwa ukuta baina yao wenye mlango, ndani mna rahma na nje kwa upande wake wa mbele mna adhabu



سوره: AL-HADIID

آيه : 14

يُنَادُونَهُمۡ أَلَمۡ نَكُن مَّعَكُمۡۖ قَالُواْ بَلَىٰ وَلَٰكِنَّكُمۡ فَتَنتُمۡ أَنفُسَكُمۡ وَتَرَبَّصۡتُمۡ وَٱرۡتَبۡتُمۡ وَغَرَّتۡكُمُ ٱلۡأَمَانِيُّ حَتَّىٰ جَآءَ أَمۡرُ ٱللَّهِ وَغَرَّكُم بِٱللَّهِ ٱلۡغَرُورُ

(Wanafiki) Watawaita Waumini wawambie: Je, kwani hatukuwa pamoja nanyi? Watasema: Ndio! Lakini nyinyi mmezifitini nafsi zenu, na mkasitasita; na mkatia shaka, na yakakudanganyeni matamanio ya nafsi zenu, mpaka ikawajieni amri ya Allah (umauti) na akawadanganya kwa Allah mdanganyifu.(msimfuate Allah)



سوره: AL-HADIID

آيه : 15

فَٱلۡيَوۡمَ لَا يُؤۡخَذُ مِنكُمۡ فِدۡيَةٞ وَلَا مِنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْۚ مَأۡوَىٰكُمُ ٱلنَّارُۖ هِيَ مَوۡلَىٰكُمۡۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ

Basi leo haitochukuliwa kutoka kwenu fidia na wala kutoka kwa waliokufuru. Makazi yenu ni moto, hayo ndio yanayostahiki kwenu, na ni marejeo mabaya yalioje



سوره: AL-HADIID

آيه : 16

۞أَلَمۡ يَأۡنِ لِلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَن تَخۡشَعَ قُلُوبُهُمۡ لِذِكۡرِ ٱللَّهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ ٱلۡحَقِّ وَلَا يَكُونُواْ كَٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلُ فَطَالَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡأَمَدُ فَقَسَتۡ قُلُوبُهُمۡۖ وَكَثِيرٞ مِّنۡهُمۡ فَٰسِقُونَ

Je, haujafika wakati kwa walioamini kwamba zinyenyekee nyoyo zao kwa kumuabudu Allah na yale yaliyoteremka ya haki, na wala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu kabla ya hapo, na ukarefuka juu yao muda, kisha zikawa ngumu nyoyo zao? Na wengi miongoni mwao ni mafasiki



سوره: AL-HADIID

آيه : 17

ٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ يُحۡيِ ٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ مَوۡتِهَاۚ قَدۡ بَيَّنَّا لَكُمُ ٱلۡأٓيَٰتِ لَعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ

Jueni kwamba Allah Anahuisha ardhi baada ya kufa kwake. Amekwishakubainishieni Aya (Ishara zake) ili mpate kutia akilini, (kuzingatia)



سوره: AL-HADIID

آيه : 18

إِنَّ ٱلۡمُصَّدِّقِينَ وَٱلۡمُصَّدِّقَٰتِ وَأَقۡرَضُواْ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنٗا يُضَٰعَفُ لَهُمۡ وَلَهُمۡ أَجۡرٞ كَرِيمٞ

Hakika wanaume watoao swadaqah na wanawake watoao swadaqah na wakamkopesha Allah mkopo mzuri, Atawazidishia maradufu, na watapa malipo mazuri



سوره: AL-HADIID

آيه : 19

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦٓ أُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلصِّدِّيقُونَۖ وَٱلشُّهَدَآءُ عِندَ رَبِّهِمۡ لَهُمۡ أَجۡرُهُمۡ وَنُورُهُمۡۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآ أُوْلَـٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَحِيمِ

Na wale waliomwamini Allah na Mtume Wake, hao ndio waliosadikisha na Mashahidi mbele ya Mola wao. Watapa ujira wao na nuru yao. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Aya Zetu hao ni watu wa motoni



سوره: AL-HADIID

آيه : 20

ٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّمَا ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا لَعِبٞ وَلَهۡوٞ وَزِينَةٞ وَتَفَاخُرُۢ بَيۡنَكُمۡ وَتَكَاثُرٞ فِي ٱلۡأَمۡوَٰلِ وَٱلۡأَوۡلَٰدِۖ كَمَثَلِ غَيۡثٍ أَعۡجَبَ ٱلۡكُفَّارَ نَبَاتُهُۥ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَىٰهُ مُصۡفَرّٗا ثُمَّ يَكُونُ حُطَٰمٗاۖ وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِ عَذَابٞ شَدِيدٞ وَمَغۡفِرَةٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَرِضۡوَٰنٞۚ وَمَا ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَآ إِلَّا مَتَٰعُ ٱلۡغُرُورِ

Jueni kwamba maisha ya dunia ni mchezo na pumbao na mapambo, na kufakharishana baina yenu na kushindana kwa wingi wa mali na watoto; ni kama mfano wa mvua inayowafurahisha wakulima mimea yake, kisha yananyweya, kisha utayaona yamepiga manjano, kisha yanakuwa mabua. Na Akhera kuna adhabu kali, na msamaha kutoka kwa Allah na radhi zake. Na uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni sterehe fupi za udanganyifu



سوره: AL-HADIID

آيه : 21

سَابِقُوٓاْ إِلَىٰ مَغۡفِرَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ وَجَنَّةٍ عَرۡضُهَا كَعَرۡضِ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ أُعِدَّتۡ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦۚ ذَٰلِكَ فَضۡلُ ٱللَّهِ يُؤۡتِيهِ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ ذُو ٱلۡفَضۡلِ ٱلۡعَظِيمِ

Kimbilieni kuomba msamaha kwa Mola wenu na Pepo (ambayo) upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, imeandaliwa kwa wale walio muamini Allah na Mtume Wake. Hiyo ni fadhila ya Allah, Humpa Amtakaye. Na Allah ni Mwenye fadhila kubwa



سوره: AL-HADIID

آيه : 22

مَآ أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا فِيٓ أَنفُسِكُمۡ إِلَّا فِي كِتَٰبٖ مِّن قَبۡلِ أَن نَّبۡرَأَهَآۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٞ

Hautokei msiba wowote katika ardhi au katika nafsi zenu isipokuwa umo katika Kitabu kabla hatuja utokezesha (hatujauumba). Hakika hayo kwa Allah ni mepesi



سوره: AL-HADIID

آيه : 23

لِّكَيۡلَا تَأۡسَوۡاْ عَلَىٰ مَا فَاتَكُمۡ وَلَا تَفۡرَحُواْ بِمَآ ءَاتَىٰكُمۡۗ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخۡتَالٖ فَخُورٍ

Ili msihuzunike juu ya yale yaliyo kuondokeeni na wala msifurahie kwa yale Aliyokupeni (Allah); na Allah Hapendi kila mwenye kujivuna, anaye jifakharisha



سوره: AL-HADIID

آيه : 24

ٱلَّذِينَ يَبۡخَلُونَ وَيَأۡمُرُونَ ٱلنَّاسَ بِٱلۡبُخۡلِۗ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡغَنِيُّ ٱلۡحَمِيدُ

Ambao wanaofanya ubakhili na wanaamrisha watu ubakhili. Na atakayekengeuka, basi hakika Allah Ndiye Mkwasi, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote



سوره: AL-HADIID

آيه : 25

لَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا رُسُلَنَا بِٱلۡبَيِّنَٰتِ وَأَنزَلۡنَا مَعَهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡمِيزَانَ لِيَقُومَ ٱلنَّاسُ بِٱلۡقِسۡطِۖ وَأَنزَلۡنَا ٱلۡحَدِيدَ فِيهِ بَأۡسٞ شَدِيدٞ وَمَنَٰفِعُ لِلنَّاسِ وَلِيَعۡلَمَ ٱللَّهُ مَن يَنصُرُهُۥ وَرُسُلَهُۥ بِٱلۡغَيۡبِۚ إِنَّ ٱللَّهَ قَوِيٌّ عَزِيزٞ

Kwa yakini Tuliwapeleka Mitume Wetu kwa hoja zilizo wazi wazi, na Tukateremsha pamoja nao Kitabu na Mizani (shariy’ah) ili watu wasimamie kwa uadilifu. Na Tukateremsha chuma chenye nguvu nyingi na manufaa kwa watu, na ili Allah Ajue nani atakayeinusuru (Dini Yake) na Mtume Wake hali ya kuwa ni ghaibu. Hakika Allah ni Mwenye nguvu zote, Mwenye kushinda



سوره: AL-HADIID

آيه : 26

وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا نُوحٗا وَإِبۡرَٰهِيمَ وَجَعَلۡنَا فِي ذُرِّيَّتِهِمَا ٱلنُّبُوَّةَ وَٱلۡكِتَٰبَۖ فَمِنۡهُم مُّهۡتَدٖۖ وَكَثِيرٞ مِّنۡهُمۡ فَٰسِقُونَ

Na hakika tulimpeleka Nuhu na Ibrahim na tukajaalia kwenye kizazi chao Mitume na Vitabu. Basi miongoni mwao kuna waliyoongoka na wengi kati yao mafasiki



سوره: AL-HADIID

آيه : 27

ثُمَّ قَفَّيۡنَا عَلَىٰٓ ءَاثَٰرِهِم بِرُسُلِنَا وَقَفَّيۡنَا بِعِيسَى ٱبۡنِ مَرۡيَمَ وَءَاتَيۡنَٰهُ ٱلۡإِنجِيلَۖ وَجَعَلۡنَا فِي قُلُوبِ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُ رَأۡفَةٗ وَرَحۡمَةٗۚ وَرَهۡبَانِيَّةً ٱبۡتَدَعُوهَا مَا كَتَبۡنَٰهَا عَلَيۡهِمۡ إِلَّا ٱبۡتِغَآءَ رِضۡوَٰنِ ٱللَّهِ فَمَا رَعَوۡهَا حَقَّ رِعَايَتِهَاۖ فَـَٔاتَيۡنَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنۡهُمۡ أَجۡرَهُمۡۖ وَكَثِيرٞ مِّنۡهُمۡ فَٰسِقُونَ

Kisha Tukafuatisha baada yao, Mitume Wetu, na Tukamfuatisha ‘Issa mwana wa Maryam, na Tukampa Injili. Na Tukaweka katika nyoyo za wale waliomfuata upole na rahmah. Na uruhubani (maisha ya utawa wa Mapadri); wameyaanzisha wao wenyewe Hatukuwawajibishia hayo juu yao, isipokuwa ni kutafuta radhi za Allah. Lakini hawakuufuata ipasavyo kuufuata. Basi Tukawapa wale walioamini miongoni mwao malipo yao, na wengi wao ni mafasiki



سوره: AL-HADIID

آيه : 28

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَءَامِنُواْ بِرَسُولِهِۦ يُؤۡتِكُمۡ كِفۡلَيۡنِ مِن رَّحۡمَتِهِۦ وَيَجۡعَل لَّكُمۡ نُورٗا تَمۡشُونَ بِهِۦ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Enyi walioamini! Mcheni Allah, na muaminini Mtume Wake. (Allah) Atakupeni sehemu mbili kati ya rahmah Zake, na Atakuwekeeni nuru mnatembea nayo, na Atakusameheni; na Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu



سوره: AL-HADIID

آيه : 29

لِّئَلَّا يَعۡلَمَ أَهۡلُ ٱلۡكِتَٰبِ أَلَّا يَقۡدِرُونَ عَلَىٰ شَيۡءٖ مِّن فَضۡلِ ٱللَّهِ وَأَنَّ ٱلۡفَضۡلَ بِيَدِ ٱللَّهِ يُؤۡتِيهِ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ ذُو ٱلۡفَضۡلِ ٱلۡعَظِيمِ

Ili wajue waliopewa Kitabu kwamba hawana uwezo wa chochote katika fadhila za Allah, na kwamba fadhila zimo Mkononi mwa Allah, Humpa Amtakaye, na Allah ni Mwenye fadhila kubwa