سوره: QAAF 

آيه : 1

قٓۚ وَٱلۡقُرۡءَانِ ٱلۡمَجِيدِ

Qaaf. Nina apa kwa Qur’ani Tukufu



سوره: QAAF 

آيه : 2

بَلۡ عَجِبُوٓاْ أَن جَآءَهُم مُّنذِرٞ مِّنۡهُمۡ فَقَالَ ٱلۡكَٰفِرُونَ هَٰذَا شَيۡءٌ عَجِيبٌ

Bali wamestaajabu kwamba amewajia muonyaji miongoni mwao, na kwa sababu hiyo makafiri wakasema: “Hili ni jambo la ajabu sana!



سوره: QAAF 

آيه : 3

أَءِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗاۖ ذَٰلِكَ رَجۡعُۢ بَعِيدٞ

Je, hivi tukifa na tukawa udongo (tutafufuliwa)? Kurejea huko kuko mbali sana”



سوره: QAAF 

آيه : 4

قَدۡ عَلِمۡنَا مَا تَنقُصُ ٱلۡأَرۡضُ مِنۡهُمۡۖ وَعِندَنَا كِتَٰبٌ حَفِيظُۢ

Hakika, sisi tumejua kila ambacho ardhi inakipunguza kwao[1] na tunacho Kitabu kinachohifadhi barabara


1- - Kinachokusudiwa hap ani kwamba, kwa Allah hakipotei kitu. Pamoja na kwamba, makafifiri katika Aya iliyopita kabla ya hii wanaona kwamba wakifa na kuzikwa miili yao inaoza ardhini na kwamba si jambo linalowezekana kurejea tena kwenye hali yao ya zamani, Allah anasema hilo kwake ni jepesi na hakuna kitakachopotea.


سوره: QAAF 

آيه : 5

بَلۡ كَذَّبُواْ بِٱلۡحَقِّ لَمَّا جَآءَهُمۡ فَهُمۡ فِيٓ أَمۡرٖ مَّرِيجٍ

Bali wameikadhibisha (wamei-pinga) haki ilipowajia. Basi wao wamo katika jambo la mkorogeko



سوره: QAAF 

آيه : 6

أَفَلَمۡ يَنظُرُوٓاْ إِلَى ٱلسَّمَآءِ فَوۡقَهُمۡ كَيۡفَ بَنَيۡنَٰهَا وَزَيَّنَّـٰهَا وَمَا لَهَا مِن فُرُوجٖ

Je, hawatazami mbingu juu yao, vipi Tumezijenga na Tumezipamba, na wala hazina mipasuko yoyote



سوره: QAAF 

آيه : 7

وَٱلۡأَرۡضَ مَدَدۡنَٰهَا وَأَلۡقَيۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ وَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوۡجِۭ بَهِيجٖ

Na ardhi Tumeitandaza na Tukaiwekea milima thabiti, na Tukaotesha humo kila aina ya mimea ya kupendeza



سوره: QAAF 

آيه : 8

تَبۡصِرَةٗ وَذِكۡرَىٰ لِكُلِّ عَبۡدٖ مُّنِيبٖ

Ni ufumbuzi wa macho na ukumbusho kwa kila mja mwenye kuelekea kwa Allah



سوره: QAAF 

آيه : 9

وَنَزَّلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ مُّبَٰرَكٗا فَأَنۢبَتۡنَا بِهِۦ جَنَّـٰتٖ وَحَبَّ ٱلۡحَصِيدِ

Na Tukateremsha kutoka mbinguni maji yaliyobarikiwa, kisha Tukaotesha kwayo mabustani na nafaka za kuvunwa



سوره: QAAF 

آيه : 10

وَٱلنَّخۡلَ بَاسِقَٰتٖ لَّهَا طَلۡعٞ نَّضِيدٞ

Na mitende mirefu yenye mashada (makole) ya matunda yenye kuzaa kwa wingi



سوره: QAAF 

آيه : 11

رِّزۡقٗا لِّلۡعِبَادِۖ وَأَحۡيَيۡنَا بِهِۦ بَلۡدَةٗ مَّيۡتٗاۚ كَذَٰلِكَ ٱلۡخُرُوجُ

Ili iwe ni riziki kwa waja wangu. Na Tukahuisha kwayo nchi iliyokufa, kama hivyo ndivyo utakavyokuwa ufufuaji



سوره: QAAF 

آيه : 12

كَذَّبَتۡ قَبۡلَهُمۡ قَوۡمُ نُوحٖ وَأَصۡحَٰبُ ٱلرَّسِّ وَثَمُودُ

Walikadhibisha kabla yao watu wa Nuhu na wakazi wa Ar-Rass na kina Thamud



سوره: QAAF 

آيه : 13

وَعَادٞ وَفِرۡعَوۡنُ وَإِخۡوَٰنُ لُوطٖ

Na kina Aad na Firaun na ndugu wa Lutwi



سوره: QAAF 

آيه : 14

وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡأَيۡكَةِ وَقَوۡمُ تُبَّعٖۚ كُلّٞ كَذَّبَ ٱلرُّسُلَ فَحَقَّ وَعِيدِ

Na wakaazi wa Machakani na watu wa Tubbaa, wote walikadhibisha Mitume. Basi onyo likathibitika juu yao



سوره: QAAF 

آيه : 15

أَفَعَيِينَا بِٱلۡخَلۡقِ ٱلۡأَوَّلِۚ بَلۡ هُمۡ فِي لَبۡسٖ مِّنۡ خَلۡقٖ جَدِيدٖ

Je, kwani Tulichoka kwa uumbaji wa kwanza? Bali wao wamo katika shaka juu ya uumbaji upya (kufufuliwa)



سوره: QAAF 

آيه : 16

وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ وَنَعۡلَمُ مَا تُوَسۡوِسُ بِهِۦ نَفۡسُهُۥۖ وَنَحۡنُ أَقۡرَبُ إِلَيۡهِ مِنۡ حَبۡلِ ٱلۡوَرِيدِ

Na kwa yakini Tumemuumba Mtu na Tunajua yale inayowaza nafsi yake, na Sisi Tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake



سوره: QAAF 

آيه : 17

إِذۡ يَتَلَقَّى ٱلۡمُتَلَقِّيَانِ عَنِ ٱلۡيَمِينِ وَعَنِ ٱلشِّمَالِ قَعِيدٞ

Pale wanapopokea wapokeaji wawili (Malaika) wanaokaa kuliani na kushotoni



سوره: QAAF 

آيه : 18

مَّا يَلۡفِظُ مِن قَوۡلٍ إِلَّا لَدَيۡهِ رَقِيبٌ عَتِيدٞ

Hatamki kauli yoyote isipokuwa anaye mchungaji aliyejitayarisha (kurekodi)



سوره: QAAF 

آيه : 19

وَجَآءَتۡ سَكۡرَةُ ٱلۡمَوۡتِ بِٱلۡحَقِّۖ ذَٰلِكَ مَا كُنتَ مِنۡهُ تَحِيدُ

Na uchungu wa mauti (wa kutoka roho) utakapomjia kwa haki. (Itasemwa): Hayo ndiyo yale uliyokuwa ukiyakimbia



سوره: QAAF 

آيه : 20

وَنُفِخَ فِي ٱلصُّورِۚ ذَٰلِكَ يَوۡمُ ٱلۡوَعِيدِ

Na litapulizwa baragumu. Hiyo ndio Siku ya miadi. (makamiano)



سوره: QAAF 

آيه : 21

وَجَآءَتۡ كُلُّ نَفۡسٖ مَّعَهَا سَآئِقٞ وَشَهِيدٞ

Na kila nafsi itakuja pamoja nayo mcungaji na shahidi



سوره: QAAF 

آيه : 22

لَّقَدۡ كُنتَ فِي غَفۡلَةٖ مِّنۡ هَٰذَا فَكَشَفۡنَا عَنكَ غِطَآءَكَ فَبَصَرُكَ ٱلۡيَوۡمَ حَدِيدٞ

(Aambiwe): Kwa yakini ulikuwa umeghafilika na haya! Basi Tumekuondoshea kifuniko chako (pazia lako), basi kuona kwako leo ni kukali



سوره: QAAF 

آيه : 23

وَقَالَ قَرِينُهُۥ هَٰذَا مَا لَدَيَّ عَتِيدٌ

Na Malaika wake aliyepewa jukumu atasema: Hii (rekodi) iliyoko kwangu imeshatayarishwa



سوره: QAAF 

آيه : 24

أَلۡقِيَا فِي جَهَنَّمَ كُلَّ كَفَّارٍ عَنِيدٖ

(Allaah Atasema): Mtupeni katika Jahannam kila kafiri, mkaidi!



سوره: QAAF 

آيه : 25

مَّنَّاعٖ لِّلۡخَيۡرِ مُعۡتَدٖ مُّرِيبٍ

Mzuiaji wa kheri, mwenye kuruka mipaka, mwenye kutia shaka



سوره: QAAF 

آيه : 26

ٱلَّذِي جَعَلَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَ فَأَلۡقِيَاهُ فِي ٱلۡعَذَابِ ٱلشَّدِيدِ

Ambaye amefanya mwabudiwa mwengine pamoja na Allah, basi mtupeni katika adhabu kali



سوره: QAAF 

آيه : 27

۞قَالَ قَرِينُهُۥ رَبَّنَا مَآ أَطۡغَيۡتُهُۥ وَلَٰكِن كَانَ فِي ضَلَٰلِۭ بَعِيدٖ

Shatani mwenzake atasema: Ee Mola wetu mlezi! Sikumpoteza mimi, bali yeye mwenyewe alikuwa katika upotofu wa mbali. (na haki)



سوره: QAAF 

آيه : 28

قَالَ لَا تَخۡتَصِمُواْ لَدَيَّ وَقَدۡ قَدَّمۡتُ إِلَيۡكُم بِٱلۡوَعِيدِ

(Allah) Atasema: Msigombane mbele yangu, na hali Nilikuleteeni onyo Langu!



سوره: QAAF 

آيه : 29

مَا يُبَدَّلُ ٱلۡقَوۡلُ لَدَيَّ وَمَآ أَنَا۠ بِظَلَّـٰمٖ لِّلۡعَبِيدِ

Haibadilishwi kauli Kwangu, Nami si mwenye kudhulumu waja wangu



سوره: QAAF 

آيه : 30

يَوۡمَ نَقُولُ لِجَهَنَّمَ هَلِ ٱمۡتَلَأۡتِ وَتَقُولُ هَلۡ مِن مَّزِيدٖ

Siku Tutakapoiambia Jahannam: Je, umeshajaa? Nayo itasema: Je, kuna ziada yoyote?