سوره: AL-QALAM 

آيه : 31

قَالُواْ يَٰوَيۡلَنَآ إِنَّا كُنَّا طَٰغِينَ

Wakasema: Ole wetu! Hakika sisi tumekuwa warukao mipaka



سوره: AL-QALAM 

آيه : 32

عَسَىٰ رَبُّنَآ أَن يُبۡدِلَنَا خَيۡرٗا مِّنۡهَآ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا رَٰغِبُونَ

Asaa Mola wetu akatubadilishia lilio bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi



سوره: AL-QALAM 

آيه : 33

كَذَٰلِكَ ٱلۡعَذَابُۖ وَلَعَذَابُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَكۡبَرُۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ

Kama hivyo ndivyo inakuwa adhabu (ya hapa duniani), bila shaka adhabu ya akhera ni kubwa zaidi, laiti wangalijua!



سوره: AL-QALAM 

آيه : 34

إِنَّ لِلۡمُتَّقِينَ عِندَ رَبِّهِمۡ جَنَّـٰتِ ٱلنَّعِيمِ

Hakika wachamungu watapata Kwa Mola wao Bustani za neema



سوره: AL-QALAM 

آيه : 35

أَفَنَجۡعَلُ ٱلۡمُسۡلِمِينَ كَٱلۡمُجۡرِمِينَ

Je, Tuwafanye Waislamu (watiifu) sawa Kama wahalifu?



سوره: AL-QALAM 

آيه : 36

مَا لَكُمۡ كَيۡفَ تَحۡكُمُونَ

Mmekuwaaje Nyinyi, Vipi mnahukumu?



سوره: AL-QALAM 

آيه : 37

أَمۡ لَكُمۡ كِتَٰبٞ فِيهِ تَدۡرُسُونَ

Au mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma?



سوره: AL-QALAM 

آيه : 38

إِنَّ لَكُمۡ فِيهِ لَمَا تَخَيَّرُونَ

Kwamba hakika Yatakuwamo Kwa ajili yenu mnayo yachagua (mnachopendelea)?



سوره: AL-QALAM 

آيه : 39

أَمۡ لَكُمۡ أَيۡمَٰنٌ عَلَيۡنَا بَٰلِغَةٌ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ إِنَّ لَكُمۡ لَمَا تَحۡكُمُونَ

Au je, mnavyo viapo juu yetu vinavyofika mpaka siku ya Kiyama ya kuwa ninyi mtapata mnayo yahukumu?



سوره: AL-QALAM 

آيه : 40

سَلۡهُمۡ أَيُّهُم بِذَٰلِكَ زَعِيمٌ

Waulize Hao: Ni nani miongoni mwao mdhamini wa hayo?



سوره: AL-QALAM 

آيه : 41

أَمۡ لَهُمۡ شُرَكَآءُ فَلۡيَأۡتُواْ بِشُرَكَآئِهِمۡ إِن كَانُواْ صَٰدِقِينَ

Au wanao washirika? Basi wawalete washirika wao wakiwa wanasema kweli



سوره: AL-QALAM 

آيه : 42

يَوۡمَ يُكۡشَفُ عَن سَاقٖ وَيُدۡعَوۡنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ فَلَا يَسۡتَطِيعُونَ

Siku ambayo yatakapokuwa mateso makali, na wataitwa kusujudu lakini hawataweza



سوره: AL-QALAM 

آيه : 43

خَٰشِعَةً أَبۡصَٰرُهُمۡ تَرۡهَقُهُمۡ ذِلَّةٞۖ وَقَدۡ كَانُواْ يُدۡعَوۡنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ وَهُمۡ سَٰلِمُونَ

Macho Yao yatainama chini, udhalilifu utawafunika. Na hali walikuwa wakiitwa wasujudu (kuswali duniani) walipokuwa wazima wa afya



سوره: AL-QALAM 

آيه : 44

فَذَرۡنِي وَمَن يُكَذِّبُ بِهَٰذَا ٱلۡحَدِيثِۖ سَنَسۡتَدۡرِجُهُم مِّنۡ حَيۡثُ لَا يَعۡلَمُونَ

Basi Niache na anayekadhibisha Maneno haya (Qurani hii) Tutawavuta pole pole adhabuni kwa namna wasiyoijua



سوره: AL-QALAM 

آيه : 45

وَأُمۡلِي لَهُمۡۚ إِنَّ كَيۡدِي مَتِينٌ

Na Ninawapa muda, hakika mpango Wangu ni Madhubuti



سوره: AL-QALAM 

آيه : 46

أَمۡ تَسۡـَٔلُهُمۡ أَجۡرٗا فَهُم مِّن مَّغۡرَمٖ مُّثۡقَلُونَ

Au unawaomba ujira, na wao wanaelemewa na gharama hiyo?



سوره: AL-QALAM 

آيه : 47

أَمۡ عِندَهُمُ ٱلۡغَيۡبُ فَهُمۡ يَكۡتُبُونَ

Au wanayo (elimu) ya ghaibu, basi wao wanaandika?



سوره: AL-QALAM 

آيه : 48

فَٱصۡبِرۡ لِحُكۡمِ رَبِّكَ وَلَا تَكُن كَصَاحِبِ ٱلۡحُوتِ إِذۡ نَادَىٰ وَهُوَ مَكۡظُومٞ

Basi subiri hukumu ya mola wako, wala usiwe kama sahibu wa nyangumi, alipomwita (Mola wake) na hali yeye alikuwa mwenye huzuni nyingi (Amebanwa na Dhiki)



سوره: AL-QALAM 

آيه : 49

لَّوۡلَآ أَن تَدَٰرَكَهُۥ نِعۡمَةٞ مِّن رَّبِّهِۦ لَنُبِذَ بِٱلۡعَرَآءِ وَهُوَ مَذۡمُومٞ

Kama isingeli mfikia neema kutoka kwa Mola wake, bila ya shaka angeli tupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa



سوره: AL-QALAM 

آيه : 50

فَٱجۡتَبَٰهُ رَبُّهُۥ فَجَعَلَهُۥ مِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ

Lakini mola wake alimchagua na akamfanya kuwa ni miongoni mwa watu wema



سوره: AL-QALAM 

آيه : 51

وَإِن يَكَادُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَيُزۡلِقُونَكَ بِأَبۡصَٰرِهِمۡ لَمَّا سَمِعُواْ ٱلذِّكۡرَ وَيَقُولُونَ إِنَّهُۥ لَمَجۡنُونٞ

Na walio kufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanapo sikia mawaidha, na wanasema: Hakika yeye ni



سوره: AL-QALAM 

آيه : 52

وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكۡرٞ لِّلۡعَٰلَمِينَ

Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote